SERIKALI YAKANUSHA SUKARI YA ZANZIBAR KUZUIWA KUUZWATANZANIA BARA
Serikali imekanusha taarifa
zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba imekizuia Kiwanda cha Sukari
Zanzibar,ZSFL kuuza Sukari yake Tanzania Bara.
Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abbas |
Akizungumza jana jijini Arusha,Mkurugenzi
wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan
Abbas amesema, kiwanda hicho kinapaswa kukidhi soko la Zanzibar la tani elfu 10
badala ya kulalamika kimezuiwa kuuza Sukari nje.
Dk.Abbas amesema mahitaji ya kawaida
Zanzibar ya sukari ni Tani elfu 17 mpaka elfu 20 kwa mwaka lakini kiwanda hicho
kina uwezo wa kuzalisha tani elfu 10 japo kwa sasa uzalishaji umeshuka hadi
tani elfu 8 hivyo kufanya Zanzibar kuwa na upungufu wa tani elfu 9 hadi elfu
12.
Mapema wiki hii,Kaimu Mkurugenzi Mkuu
Kiwanda hicho cha Sukari Zanzibar,Bi. Fatma Salum Ali,alisema kiwanda hicho
kinapata hasara ya zaidi ya shilingi laki tatu kwa kila tani moja ya Sukari
inayozalishwa kutokana na kushindwa kupata kibali cha kuuza Sukari Tanzania
Bara ambako kuna soko shindani kwa misingi ya gharama za uzalishaji na bei.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments