MWANAMKE ASIYEJULIKANA ATUPA MTOTO WA UMRI WA SIKU 1 KATIKA UWANJA MICHEZO
Mtoto
wa jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa na umri wa siku 1 ameokotwa akiwa hai katika uwanja wa Azimio Halmashauri ya manispaa ya Mpanda Mkoani
Katavi baada ya kutupwa na mwanamke
ambaye mpaka sasa hajafahamika majina wala makazi yake.
Mashuhuda
wa tukio wakilaani tukio hilo,wamesema mtoto huyo inasadikiwa alitupwa Ijumaa ya
Juni 8 mwaka huu majira ya mchana mpaka alipookotwa majira ya saa kumi jioni .
Hata
hivyo wananchi wilayani Mpanda wamesikitishwa na tukio hilo na kuomba hatua kali zichukuliwe dhidi ya mwanamke atakayebainika
kutenda unyama huo dhidi ya mtoto asiyekuwa na hatia.
Kwa
upande wake Afisa Ustawi wa jamii manispaa Redgunda Mayorwa amethibitisha
kupokea taarifa za mtoto huyo ambapo amesema jeshi la polisi wanaendelea na
uchunguzi wa tukio hilo ili kumpata na kumfikisha katika vyombo vya sheria
mwanamke aliyetenda unyama huo.
Aidha
ametoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali na jeshi la
Polisi kuhusiana na tukio hilo kwa kuwa kitendo cha kutupa mtoto hakina tija
kwa jamii na amewashauri wanawake kuwa kama hawawezi kuzaa basi watumie uzazi
wa Mpango kuliko kutesa mtoto.
Mtoto
huyo ambaye jina lake ni FURAHA kwa mjibu wa barua ya mwanamke huyo aliyoiacha
karibu na mtoto huyo alipokuwa amelazwa uwanjani,mpaka sasa yupo chini ya
uangalizi wa madaktari katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda.
Hilo
siyo tukio la kwanza kwa wanawake wa Manispaa ya Mpanda kutupa watoto huku
wahusika wakiwa hawakamatiki.
Mengi Zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments