RAIS MUGABE AMEMTUMBUA JIPU MAKAMU WAKE WA RAIS
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amemfuta kazi Makamu wake wa Rais Emmerson Mnangagwa. Emmerson Mnangagwa Kwa mjibu wa Waziri wa Habari wa Zimbabwe Simon Kahaya Moyo,Bw.Mnangagwa (75) ameachishwa kazi kwa madai kuwa alionyesha tabia za kukosa uzalendo na uaminifu hasa kwa Rais. Kufutwa kwake ni ishara kuwa mke wa rais Robert Muabe, Bi.Grace,atafuata nyayo za mumeme za kuwa rais wa Zimbabwe Siku ya Jumapili Bi.Grace Mugabe alitoa wito wa kutaka mumewe amfute kazi Mnangagwa. Bw.Mnangagwa ambaye ni mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi,amekuwa kwenye mstari wa mbele kumrithi Rais Mugabe. Kufutwa kwake kunakuja baada ya Rais Robert Mugabe(93)kutishia kumuachisha kazi Bw Mnangagwa, hatua ambayo imezua uvumi kuwa anataka mke wake kuchukua hatamu za kuliongoza taifa hilo. Akihutubia mkutano wa wanachama wa makanisa ya asili mji Harare siku ya Jumapili,Bi Mugabe alisema Bw Mugabe alimtaka Mnangagwa na wafuasi wake kumuonyesha uzalendo au afutwe kazi. Chama cha Zanu-PF kinataraj...