WATOZA USHURU PUNGUFU TA TANI 1 KUKIONA CHA MOTO,SERIKALI KUANZA KULIPA MISHAHARA YA WATUMISHI WA UMMA MWEZI HUU
Na.Issack Gerald
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh.John Magufuli ameviagiza vyombo vya ulinzi na Usalama nchini
kuwakamata watumishi na watoza ushuru wote nchini watakamtomtoza ushuru
mwananchi anayesafrisha mzigo usiozidi tani moja.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo
wakati akihutubia wananchi mjini Bukoba Mkoani Kagera ambapo alikuwa na
shughuli ya kuweka jiwe la msingi upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
Katika hatua nyingine,Rais Magufuli
amesema kuanzia mwezi huu serikali itaanza kulipa stahiki zote za wafanyakazi
wa umma wanazoidai serikali ikiwemo malimbikizo ya mishahara ambapo zaidi ya
shilingi bilioni 159 zimetengwa kwa ajili hiyo.
Rais magufuli amefanya ziara mkoani
Kagera kama mwendelezo wa ziara zake za kikazi katika maeneo mbalimbali hapa
nchini ambapo wiki iliyopita alifanya ziara katika mikoa ya Mwanza na Geita na
kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa mjibu wa rais Magufuli,keshokutwa
atakwenda Nchini Uganda kwa ajili ya kwenda kuweka jiwe la msingi ujenzi wa
bomba la mafuta linalojengwa kuanzia Uganda hadi Tanzania.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments