WATOTO 2 WAMEPOTEA KATIKA MAZINGIRA TATANISHI MKOANI KATAVI
Na.Issack Gerald
WATOTO wawili wakazi wa kitongoji cha
Mnyaki B Rama na Vitisho wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 9 na 11
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,wamepotea katika mazingira ya
kutatanisha.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Mnyaki B
Bw.Alex Gezaho,amethibitisha kupotea kwa watoto hao Jumamosi iliyopita ambapo amesema,walikuwa
wakiwinda ndege pori kwa manati.
Kwa mjibu wa baadhi ya wakazi wa kitongoji
cha Mnyaki B,watoto hao ambao ni wanafunzi wa shule ya Msingi Mnyaki mmoja akisoma
darasa la pili na mwingine darasa la tatu ni miongoni mwa watoto watatu
waliokuwa wakiwinda ndege siku ya juzi walipopotea.
Watoto hao wawili wametajwa kuwa
walikuwa wakiishi kwa mama mmoja anayeishi katika kitongoji cha Mnyaki B ambaye
naye ametambulika kwa jina la mama Mwereza.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Mnyaki B
amesema,tukio kama hilo lilitokea miaka mitano iliyopita katika kitongoji hicho
ambapo mtoto wa kike alipotea katika mazingira ya kutatanisha na mpaka sasa hajapatikana.
Mbali na tukio hilo la kupotea kwa
watoto,matukio mengine ambayo yamekuwea yakitokea katika kijiji cha Mnyaki kwa
ujumla ni pamoja na matukio ya watu kuvamiwa usiku na kuporwa mali na fedha zao
huku wengine wakijeruhiwa kutokana na silaha sinazotumiwa na waharifu.
Habari
zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments