RAIS MUGABE AMEMTUMBUA JIPU MAKAMU WAKE WA RAIS
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amemfuta kazi Makamu
wake wa Rais Emmerson Mnangagwa.
Emmerson Mnangagwa |
Kwa mjibu wa Waziri wa Habari wa Zimbabwe
Simon Kahaya Moyo,Bw.Mnangagwa (75) ameachishwa kazi kwa madai kuwa alionyesha
tabia za kukosa uzalendo na uaminifu hasa kwa Rais.
Kufutwa kwake ni ishara kuwa mke wa rais
Robert Muabe, Bi.Grace,atafuata nyayo za mumeme za kuwa rais wa Zimbabwe
Siku ya Jumapili Bi.Grace Mugabe alitoa
wito wa kutaka mumewe amfute kazi Mnangagwa.
Bw.Mnangagwa ambaye ni
mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi,amekuwa kwenye mstari wa mbele kumrithi Rais
Mugabe.
Kufutwa kwake kunakuja baada
ya Rais Robert Mugabe(93)kutishia kumuachisha kazi Bw Mnangagwa, hatua ambayo
imezua uvumi kuwa anataka mke wake kuchukua hatamu za kuliongoza taifa hilo.
Akihutubia mkutano wa wanachama wa
makanisa ya asili mji Harare siku ya Jumapili,Bi Mugabe alisema Bw Mugabe
alimtaka Mnangagwa na wafuasi wake kumuonyesha uzalendo au afutwe kazi.
Chama cha Zanu-PF kinatarajiwa kuifanyia
mabadiliko katiba yake wakati wa mkutano na kuweka nafasi mbili za makamu wa
rais,nafasi moja ikiwa ni ya mwanamke.
Nafasi hiyo inatarajiwa
kujazwa na Bi.Mugabe na kuongeza uwezekano wa kumrithi mume wake.
Habari zaidi ni P5TANZANIA
LIMITED
Comments