Posts

Showing posts from September 23, 2016

KUTOKA WILAYANI MLELE KATAVI -TUKIO LA NYUMBA KUCHOMWA MOTO

Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama –Mlele Katavi NYUMBA za wakazi ambazo idadi yake haijafahamika eneo la Namba moja lililopo Kata na Tarafa ya Inyonga Wilayani Mlele Mkoani Katavi,leo zimeteketezwa kwa moto na baadhi ya mali zilizokuwemo kuteketezwa katika nyumba hizo. Kwa mjibu wa baadhi ya wakazi ambao mali zao zimeteketea ,wakizungumza na Mpanda Radio Kwa njia ya Simu kwa masikitiko makubwa akiwemo Bi.Tatu M asanja wamesema kuwa, tukio hilo ambalo wameliita la kushtukiza asubuhi ya leo,wamedai limetekelezwa na askari Mkoani Katavi kuanzia majira ya asubuhi. Wametaja baadhi ya mali zao ambazo zimechomwa kwa moto mbali na nyumba zao kuwa ni pamoja na Vyakula na mavazi huku watoto wakizagaa ovyo katika eneo hilo bila wazazi wao baada ya wazazi kukimbilia kusikojulikana kufuatia wengine kupigwa na askari hao. Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP damasi Nyanda,akizungumza na Mpanda Radio Kwa njia ya Simu mchana wa leo,amesema hajapata taarifa ya utekelezwaji wa...