KUTOKA WILAYANI MLELE KATAVI -TUKIO LA NYUMBA KUCHOMWA MOTO
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama –Mlele Katavi
NYUMBA za wakazi ambazo idadi yake
haijafahamika eneo la Namba moja lililopo Kata na Tarafa ya Inyonga Wilayani
Mlele Mkoani Katavi,leo zimeteketezwa kwa moto na baadhi ya mali zilizokuwemo
kuteketezwa katika nyumba hizo.
Kwa mjibu wa baadhi ya wakazi ambao mali zao
zimeteketea ,wakizungumza na Mpanda Radio Kwa njia ya Simu kwa masikitiko
makubwa akiwemo Bi.Tatu Masanja
wamesema kuwa, tukio hilo ambalo wameliita la kushtukiza asubuhi ya leo,wamedai
limetekelezwa na askari Mkoani Katavi kuanzia majira ya asubuhi.
Wametaja
baadhi ya mali zao ambazo zimechomwa kwa moto mbali na nyumba zao kuwa ni
pamoja na Vyakula na mavazi huku watoto wakizagaa ovyo katika eneo hilo bila
wazazi wao baada ya wazazi kukimbilia kusikojulikana kufuatia wengine kupigwa
na askari hao.
Kwa upande
wake Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP damasi Nyanda,akizungumza na Mpanda
Radio Kwa njia ya Simu mchana wa leo,amesema hajapata taarifa ya utekelezwaji
wa tukio la uchomaji makazi ya watu na ameahidi kufutailia ukweli wa tukio
hilo.
Hata hivyo,Mkuu
wa Wilaya ya Mlele Bi.Rachel Kasanda ambaye pia ndiye mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama Wilayani Mlele amesema,hawezi kuzungumzia tukio hilo kwa kuwa
lipo nje ya mipaka yake ya utawala isipokuwa akaongeza kuwa anachofahamu
uchomaji wa nyumba hizo unafanywa na askari wa wanyama pori ili kuwaondoa
wavamizi wa maeneo ya hifadhi eneo hilo ambalo ameliita kuwa siyo makazi halali
ya watu bali ni hifadhi.
Hata hivyo juhudi za kuwatafuta TANAPA Mkoani Katavi zinaendelea ili kutolea ufafanuzi wa tukio hilo.
Hata hivyo juhudi za kuwatafuta TANAPA Mkoani Katavi zinaendelea ili kutolea ufafanuzi wa tukio hilo.
Tukio la
kuchomwa kawa makazi ya watu Mkoani Katavi siyo la mara ya kwanza ambapo tukio
linguine lilitekelezwa mwaka 2013 eneo la Luhafe lililopo makao makuu ya Wilaya
ya Tanganyika Kata ya Majalila wakati huo ikiwa Wilaya ya Mpanda ambapo wakazi wa
eneo hilo walidai kuchomewa nyumba na vyakula vyao pamoja na mali nyingine.
Endelea
kuwa nami kupata ukweli wa tukio hilo kwa undani zaidi.
Kwa maoni,ushauri au
ukiwa n ahabari yoyote,tutumie kupitia email ya Ofisi p5tanzania@gmail.com
Comments