MATUKIO YA WIKI MKOANI KATAVI NA TANZANIA KWA UJUMLA DESEMBA 21-26,2015 NA P5 TANZANIA YA ISSACK GERALD BATHROMEO
NA.ISSACK GERALD BATHROMEO MAUAJI KATAVI Posted By: Issack Gerald | At: Monday, December 21, 2015 Na.Issack Gerald- Katavi Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la KAZIMIRI MASUMBUKO(49) MKAZI NA MKULIMA WA MISANGA aliuawa kwa kuchomwa kitu chenye ncha kali sehemu za mgongoni, mkononi, mkono wa kushoto na kidevuni na watu wasiofahamika Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo,Kmanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari,amesema tukio hilo limetokea jana Jumapili tarehe 20.12.2015 majira ya saa katika kitongoji cha Misanga Kata na Tarafa ya Mwese Wilayani Mpanda Mkoani Katavi. Kamanda Kidavashari amesema kuwa, siku ya tukio hilo,watuhumiwa wasiofahamika kwa sura wala idadi yao walifika nyumbani kwa marehemu wakakuvunja mlango na kuingia moja kwa moja hadi chumbani kwa marehemu na kumpeleka sebureni kwake kisha kutekeleza mauaji hayo na kutokomea kusikojulikana . Mpaka sasa chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika. Hata hivyo Upelelezi wa shauri hi...