MATUKIO YA WIKI MKOANI KATAVI NA TANZANIA KWA UJUMLA DESEMBA 21-26,2015 NA P5 TANZANIA YA ISSACK GERALD BATHROMEO
NA.ISSACK GERALD BATHROMEO
Posted By:Issack Gerald | At:Monday, December
21, 2015
Na.Issack Gerald- Katavi
Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la KAZIMIRI
MASUMBUKO(49) MKAZI NA MKULIMA WA MISANGA aliuawa kwa kuchomwa kitu chenye ncha
kali sehemu za mgongoni, mkononi, mkono wa kushoto na kidevuni na watu
wasiofahamika
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo,Kmanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari,amesema
tukio hilo limetokea jana Jumapili tarehe 20.12.2015 majira ya saa katika
kitongoji cha Misanga Kata na Tarafa ya Mwese Wilayani Mpanda Mkoani Katavi.
Kamanda
Kidavashari amesema kuwa, siku ya tukio hilo,watuhumiwa wasiofahamika kwa sura
wala idadi yao walifika nyumbani kwa marehemu wakakuvunja mlango na kuingia
moja kwa moja hadi chumbani kwa marehemu na kumpeleka sebureni kwake kisha
kutekeleza mauaji hayo na kutokomea kusikojulikana .
Mpaka
sasa chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika. Hata hivyo Upelelezi wa shauri
hili unaendelea kwa kufanya msako kwa kushirikiana na wakazi wa kata ya Misanga
kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma
inayowakabili.
Wakati
huo huo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi anatoa agizo kwa wananchi kuachana na
vitendo vya kujichukulia sheria mikononi dhidi ya migogoro ya kijamii miongoni
mwao, badala yake wajenge tabia ya kuheshimu na kutumia mamlaka za kisheria
katika kutafuta ufumbuzi.
Amesisitiza
kuwa ataendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale watakaoendelea
kubainika kukiuka maagizo hayo kutokana na visingizio mbalimbali.
Posted By:Issack Gerald
| At:Monday, December 21, 2015
Na.Issack Gerald- Katavi
Jeshi
la Polisi Mkoani Katavi linawashikilia watu wawili akiwemo ASHURA MSAGUSI(30) Karani wa chuo cha
Maendeleo Msaginya Mkazi wa Kata ya Makanyagio na AISHA SUNGURA (28) Mkazi wa mtaa wa Mji wa Zamani
kwa tuhuma za shambulio la mwili.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo,Kmanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri
Kidavashari,alisema kuwa tukio hilo limetokea Mnamo tarehe 17.12.2015 majira ya
saa 5 asubuhi katika Mji wa Zamani Kata na Tarafa ya Kashaulili Wilayani Mpanda Mkoani Katavi.
Alimtaja
aliyeshambuliwa kuwa ni JENEROZA ROBA(60 Mkazi wa Nsemulwa kwa Mkumbo ambapo
alishambuliwa kwa kupingwa ngumi sehemu
mbalimbali za mwili wake na kusababishiwa maumivu makali.
Kamanda
Kidavashari alisema kuwa,siku ya tukio inasemekana kuwa mtuhumiwa ASHURA
MSAGUSI alijifanya kupandisha mashetani na kuanza kumtaja Mtendewa JENEROZA
ROBA kuwa anajihusisha na shughuli za uchawi ambazo zinaathiri familia zao.
Kitendo hicho cha kupandisha mashetani kilimshawishi AISHA SUNGURA na hivyo kuungana na ASHURA MSAGUSI
na kuanza kumshambulia mtendewa.
Watuhumiwa
wote wawili ambao wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano
zaidi na wanatarajia kufikishwa mahakamani baada ya Upelelezi kukamilika.
Kufuati
matukio ya kujichukulia sheria mkononi,Kamanda wa Polisi anatoa onyo wa watu
wenye matukio hayo,ambapo amesema ataendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa
wale watakaoendelea kubainika kukiuka maagizo hayo kutokana na visingizio
mbalimbali.
Posted By:Issack Gerald
| At:Monday, December 21, 2015
Na.Agness Mnubi-MPANDA.
WAZAZI
na Walezi mkoani Katavi wametakiwa kutambua umhimu wa haki za watoto na kuepuka
Mazingira yanayopelekea ukatili na unyanyasaji kwa watoto hao.
Akizungumza
na P5 TANZANIA MEDIA na Mpanda Rdaio Mwenyekiti wa Asasi ya Faraja
na Urafiki kwa Wanandoa na Ushauri kwa
Vijana (FUNUVI ) Bi. Neema Kidima amesema Maelewano mabaya katika ndoa na
kutalikia ni miongozni mwa vyanzo vinavyopelekea kutotambua haki za watoto na kusabaisha
mazingira ya ukatili na unyanayasaji.
Bi.
kidima ameomba Wadau wanaojihusisha na
kupinga ukatili ,Haki za binadamu, pamoja na serikali kushirikiana kutoa elimu
katika jamii juu ya haki za watoto.
Desemba
18 Mwaka huu, watoto 62 wakiwemo
wawili wenye ulemavu wa ngozi (albino) walifichuliwa Wilayani Mpanda na kamati ya baraza la watoto, wakiwa katika
mazingira yanayowanyima haki zao ikiwemo kupatiwa elimu, kwa kipindi cha mwezi Juni hadi
Desemba.
Posted By:Issack Gerald
| At:Monday, December 21, 2015
NA:OFISI YA WAZIRI MKUU -DAR ES SALAAM
SERIKALI imekwishatenga kiasi cha
sh. bilioni 137 kwa ajili ya kugharamia utoaji wa elimu ya bure kuanzia Januari
hadi Juni, mwakani.
Kauli hiyo imetolewa jana jioni
(Jumapili, Desemba 20, 2015) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumza
na mamia ya wananchi waliofika kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye uwanja wa uwanja wa mikutano wa Likangala wilayani Ruangwa, mkoani
Lindi.
“Kazi ya utumbuaji majipu imezaa
matunda kwani tumeweza kupata fedha za kugahrimia elimu ya bure ambayo
iliahidiwa na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli wakati wa kampeni. Fedha hiyo
tunayo, na tumeshaanza kuisambaza kwa sababu tunataka shule zikifunguliwa
Januari, 2016 watoto waanze kufaidika,” alisema huku akishangiliwa.
“Atakayezigusa fedha hizi na
kuzitumia vibaya ni lazima tutamtumbua tu! Tumeshawapa maelekezo Wakurugenzi wa
Halmashauri pamoja na Maafisa Elimu wao na kuwaonya kuhusu matumizi ya fedha
hizo,” alisema.
“Hatuhitaji mwanafunzi achangishwe
hela ya mitihani, na zile shilingi 10,000/- kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma
Sekondari nazo pia tutazipeleka. Na huu ni mpango wa dharura ambao haukuwemo
katika bajeti ya mwaka 2015/2016, kwa hiyo tutalazimika kuziombea kibali,”
alisema.
Waziri Mkuu Majaliwa alisema
Serikali imekwishafanya hesabu za kubaini kiasi kinachohitajika kwa ajili ya
milo ya watoto shuleni kwa wale walioko bweni na wale wa kutwa. Hesabu tunazo
na tumebaini kuwa tutazimudu,” alisema huku akishangiliwa.
“Serikali ilitoa ahadi kwa wananchi
na sisi tumedhamiria kuzitekeleza. Tuliahidi elimu bure nasi tutaitekeleza,”
alisema.
Naye Waziri wa Habari, Utamaduni,
Wasanii na Michezo, Bw. Nape Nnauye amewataka madiwani wa jimbo la Ruangwa
kuhakikisha wanamsaidia Waziri Mkuu Majaliwa kusimamia kazi za jimboni ili
aweze kuwa huru kutekeleza majukumu ya kitaifa.
“Madiwani wa jimbo hili msaidieni
Waziri Mkuu kusimamia shughuli za maendeleo ili wakati yeye anaendelea
kutekeleza majukumu ya kitaifa, ya jimbo naye yawe shwari. Msaidieni kusimamia
fedha za umma ziende kwenye miradi iliyokusudiwa ili wakati akitumbua majipu
huko kwingine na huku pia yasiote,” aliongeza.
WAZIRI MKUU ASEMA HANA KINYONGO NA MTU YEYOTE,ASEMA ITIKADI ZA SIASA ZILIISHIA OKTOBA 25
Posted By:Issack Gerald
| At:Monday, December 21, 2015
Na.OFISI YA WAZIRI MKUU.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema hana kinyongo na mtu yeyote kwa sababu alitangaza
msamaha siku aliyokabidhiwa cheti kuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa na kusisitiza
kuwa siasa ziliisha tangu Oktoba 25, mwaka huu.
Ametoa kauli hiyo jana jioni wakati
akizungumza na mamia ya wananchi waliofika kumsikiliza kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mikutano wa Likangala wilayani Ruangwa,
mkoani Lindi.
“Sina kinyongo na mtu yeyote na roho
yangu iko huru, hivi ndiyo nilivyo. Nilikwishatangaza msamaha kwa hiyo
ninawaomba wale niliowakwaza nao pia wanisamehe… lakini ninawasihi kuwa milango
iko wazi, wawe huru kurudi wakati wowote,” alisema huku akishangiliwa na
wananchi hao.
“Ninawataka twende pamoja ili tulete
maendeleo ya Ruangwa, huku nikisisitiza kaulimbinu yangu ya kampeni kwamba
Ruangwa kwa Maendeleo Inawezekana. Wao warudi tu, nitawahudumia wote bila
kujali itikadi zao.”
Aliwaeleza wakazi hao wa Ruangwa na
vitongoji vyake kwamba amekuja kuwashukuru kwa kumchagua na kumpa kura nyingi
la sivyo asingefanikiwa kuwa mbunge wao. “Kikubwa ninamshukuru Mungu
aliyemuongoza Mheshimiwa Rais pamoja na Makamu wake hadi wakanipa jukumu hili,”
alisema.
“Kipekee ninamshukuru Mungu aliyemuongoza
Mheshimiwa Rais na kutupa sisi wana Ruangwa tusaidiane kulibeba jukumu hili.
Ninawahakikishia kuwa pamoja na jukumu hili la kitaifa, sitawaacha wala
sitawaangusha. Nitakwenda mikoa mingine hapa nchini ili kuwasikiliza na
kuwahudumia Watanzania huku nikijua kwamba mpo salama,” alisema.
Aliwaeleza wananchi hao kwamba bila
kujali itikadi za vyama, ameunda timu ya madiwani 22 kutoka kata zote za jimbo
hilo ambayo atafanya nayo kazi kwa karibu ili kuhakikisha matarajio ya
wana-Ruangwa yanatimia. Madiwani wanane kati hao 22 wanatoka UKAWA na 14
wanatoka Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akigusia mipango ya maendeleo kwa
jimbo hilo, Waziri Mkuu alisema ameamua kuweka umeme wa nishati ya jua kwenye
shule zote na zahanati zote ambazo hazitafikiwa na umeme wa gridi ya Taifa kwa
sababu ziko pembezoni mwa jimbo hilo.
“Nafanya hivi kwa sababu sipendi
watoto wetu wakose masomo ya jioni kwa sababu ya kukosa umeme au washindwe
kufanya mafunzo kwa vitendo (practicals) kwa vile wamekosa umeme,” alisema.
Mapema, akiwa njiani kuelekea Ruangwa,
Waziri Mkuu alisimama kwa muda kijijini kwao Nandagala katika kata ya Mnacho,
na kuwasalimia wananchi waliojitokeza kumpokea kwa nderemo na hoihoi kibao.
Katika mkutano wa hadhara
ulioandaliwa kijijini hapo, Waziri Mkuu alikabidhiwa zawadi mbalimbali yakiwemo
mavazi ya kimila pamoja na silaha za jadi.
Aliwataka wakazi hao wamvumilie kwa
sababu ratiba sasa itabadilika na hawatamuona mara kwa mara kama ilivyokuwa
awali kwa vile anapaswa awahudumie Watanzania wote. “Zile safari za jimboni
zitapungua sana lakini mjue ni kwa sababu niko kwa ajili ya Watanzania wote wa
nchi hii,” alisema.
“Ninaomba dua zenu ili niendelee
kuwa mwadilifu na muwajibikaji,” aliwaomba na kususutiza kwamba waendelee
kumuombea yeye pamoja na viongozi wengine wa kitaifa ili waweze kutimiza yale
ambayo Watanzania wanatamani yatokee.
Posted By:Issack Gerald
| At:Tuesday, December 22, 2015
Na.Meshack
Ngumba-MPANDA
SERIKALI
imeombwa Kuharakisha Mchakato wa Kuibadilisha hospitali ya Wilaya Kuwa
hospitali ya halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ili Kusogeza huduma za afya kwa
wakazi wa Manispaa hiyo.
Ombi
hilo limetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda ambaye pia ni diwani wa
Kata ya Majengo Mh,William Philip Mbogo Katika Mahojiano maalum na Mpanda Radio
na P5 TANZANIA MEDIA
Katika
hatua nyingine Mh Mbogo ameahidi Kushirikiana na Madiwani wa Kata zote za
Manispaa ya Mpanda Kutatua Kero za wananchi ikiwemo Kusimamia Miradi ya
Maendeleo inayoanzishwa Kwa Maslahi ya wananchi.
Mh,Mbogo
anakuwa Meya wa Kwanza wa Manispaa ya Mpanda Kihistoria tangu halmashauri ya
Mpanda ilipopandishwa daraja Kutoka halmashauri ya Mji mwezi July mwaka huu.
MKURUGENZI HALMSHAURI YA WILAYA YA KALAMBO,ASIKITISHWA NA HALI YA ELIMU MKOANI RUKWA
Posted By:Issack Gerald
| At:Tuesday, December 22, 2015
Na.Issack
Gerald-SUMBAWANGA
MKURUGENZI Mtendaji wa
Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa Bw. Bensoni Kilagi,amesema
hajaridhishwa na matokeo ya darasa la nne na darasa la saba kwa mwaka 2015
mkoani humo.
Akizungumza
na P5 TANZANIA MEDIA Kwa njia ya
simu,Bw. Kilagi amesema matokeoa
yameendelea kuwa mabaya ambapo kwa mwaka
2014 ufaulu ulikuwa asilimia thelathini huku mwaka 2015 ufaulu huo
ukipanda kwa salimia 10 na kufikia asilimia 40.
Aidha
amesema ili kunusuru hali ya elimu Mkoani humo,wamekusudia kuitisha vikao vya
mara kwa mara vinavyohusisha wadau wa elimu wakiwemo wazazi,walezi,watendaji na
wataalamu wengine wa masuala ya elimu ili kuongeza kiwango cha ufaulu.
Hata
hivyo Bw.Kilangi amezitaja baadhi ya changamoto zinazopelekea kufanya vibaya
katika suala zimala elimu ni kutofanya
mazoezi ya mitihani mara kwa mara ,madawati pamoja na nyumba za walimu.
Posted By:Issack Gerald
| At:Wednesday, December 23,
2015
Na.OFISI
YA MAWASILIANO YA IKULU.
Rais
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli amemsimamisha kazi
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RAHCO),
Benhadard Tito.
Rais
Magufuli amesema,amemsimamisha Bw. Tito kupisha uchunguzi wa kina kutokana na
ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi, yaliobainika katika mchakato wa
utoaji wa zabuni ya ujenzi wa Reli ya Kati.
Kwa
mujibu wa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Dk Magufuli,amefikia uamuzi
huo baada ya kuitisha kikao cha wataalamu kutoka wizara na taasisi mbalimbali
za serikali, ambazo zinahusika katika utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya
Kati kwa kiwango cha kisasa.
Aidha
Rais Magufuli ameivunja Bodi ya Rahco baada ya kujiridhisha kuwa haikutekeleza
ipasavyo wajibu wake katika kusimamia mchakato wa zabuni hiyo na badala yake
imeonekana kutetea kilichofanyika.
Posted By:Issack Gerald
| At:Wednesday, December 23,
2015
Na.Ofisi
ya Waziri-DAR ES SALAAM.
Kaimu
mkurugenzi wa taasisi ya saratani ya Ocean Road Dk.Diwani Msemo amesimamishwa
kazi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu amesema,Dk.Msemo
amesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi pamoja na mambo mengine ikiwa ni
pamoja na kubaini kama kuna mgongano wa kimaslahi ambao umeathiri utendaji
chini ya Kaimu Mkurugenzi.
Wakati
huo huo Mh.Ummy,ameiagiza bodi ya taasisi ya saratani ya Ocean Road kuteua
mkurugenzi atakayekaimu nafasi ya Mkurugenzi mtendaji.
Katika
hatua nyingine,watendaji wote wa serikali katika sekta ya afya wakiwemo
wafamasia,wauguzi na waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma,wameagizwa
kukiri kwa maandishi ikiwa wanamiliki zahanati,vituo vy afya,kliniki na maduka
ya dawa ndani ya siku 21 kuanzia leo Desemba 23.
Amesema
kuwa agizo hili,halimwondolei wajibu kiongozi yeyote wa serikali ambaye
anapaswa kujaza tamko la viongozi wa Umma kuhusu rasilimali na madeni kwa mjibu
wa kifungu namba 9 na 11 cha sheria ya maadili ya viongozi wa Umma namba 13 ya
mwaka 1995 na namba 5 ya mwaka 2001
Posted By:Issack Gerald
| At:Wednesday, December 23,
2015
Na. OFISI YA
WAZIRI MKUU,
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa, Wakuu
wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa wanaongeza
udhibiti na usimamizi wa migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao husika.
Ametoa agizo hilo leo mchana
(Jumatano, Desemba 23, 2015) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Lindi
kwenye Ikulu ndogo mara baada ya kuwasili akitokea jimboni kwake Ruangwa.
“Ardhi ni mali ya Serikali
lakini maeneo yanayotwaliwa kwa sababu mbalimbali za maendeleo yasiwe chanzo
cha migogoro na wananchi tunaowaongoza,” alisema.
Akitoa mfano, Waziri Mkuu
alisema anatambua kuna mgogoro wa eneo la mgodi katika wilaya ya Ruangwa baina
ya wananchi na wawekezaji wa kampuni ya Uranex. Na hii ni kwa sababu wao ndiyo
waliamua kufanya tathmini (evaluation) ya eneo hilo. Yale ni makosa kwa sababu
aliyepaswa kufanya tathmini ni Halmashauri na siyo mwekezaji,” alisema.
Alisema wawekezaji wanaruhusiwa
kisheria kufanya tathmini lakini sheria waliyoitumia ni sheria namba 8 peke
yake. “Kama Halmashauri ingefanya kazi hiyo ni lazima wangetumia sheria ya
ardhi ya vijiji pamoja na sheria ya madini na wananchi wangepata thamani halisi
ya ardhi yao,” alisema.
“Ninaagiza Halmashauri ya
Wilaya ya Ruangwa ikahakiki lile eneo na kubaini kama ni la kilimo au la madini
na kama ni la kilimo, wananchi wamelima mazao gani na kwa muda gani kisha
wafanye tathmini upya. Yuko valuer wa Halmashauri mwenye dhamana hiyo na siyo
wao,” alisema.
“Nasisitiza tena ni vema
Wakurugenzi wote, Wakuu wa Wilaya chini ya uongozi wa Wakuu wa Mikoa
mjiridhishe kuwa hakuna migogoro kwenye maeneo yenu. Kama ipo, imalizeni kwa
kukaa mezani na kuzungumza na pande husika, inawezekana kabisa,” alisisitiza.
Posted By:Issack Gerald
| At:Thursday, December 24, 2015
Na.Issack
Gerald-MPANDA
Miundombinu
mibovu ya barabara hususani kipindi hiki cha masika imeathiri uchumi wa
waendesha pikipiki katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Matavi.
Hayo
yamebainishwa na waendesha pikipiki hao wakati wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA na mpanda redio
ambapo wamesema kuwa barabara nyingi hasa vijijini hazipitiki kutokana na
mabonde hali inayowafanya kufanya shughuli hiyo
mjini pekee.
Katika
hatua nyingine madereva hao wamesema,katika kuzua ajali za barabarani hasa
kipindi hiki cha msimu wa sikukuu wamejipanga kuendesha pikipiki kwa umakini
mkubwa kutokana ongezeko la vyombo vingi vya moto barabarani.
Takwimu
zinaonyesha kuwa katika kipindi cha sikukuu matukio ya ajali huongezeka
kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo madereva kuendesha kwa mwendokasi pamoja
na ulevi.
Posted By:Issack Gerald
| At:Thursday, December 24, 2015
Na.Issack Gerald-Mpanda
Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina Mateo Robert(33) mchimbaji mdogo mkazi wa
Mbeya-Songwe,amefariki dunia baada ya kuangukiwa na lundo la udongo akiwa
kwenye shimo (LONG BASE) wakati akichimba madini ya dhahabu.
Kamanda wa polisi Mkoani Katavi Dhahiri
Kidavashari amesema kuwa tukio hilo limetokea Mnamo tarehe 23.12.2015 majira ya
saa 09:00 kwenye Machimbo ya dhahabu ya wachimbaji wadogo ya Nsimbo yaliyopo
kijiji cha Katuma, Kata ya Katuma, Tarafa ya Mwese Wilaya ya Mpanda Mkoa wa
Katavi.
Kamanda
amesema kuwa marehemu akiwa na wenzake wawili ambao ni Edson David Akiba(25
mchimbaji Mkazi wa Kigoma pamoja na Tungu Thomas(30) mchimbaji Mkazi wa mkoa wa
Shinyanga walielekea mgodini hapo kufanya shughuli zao za uchimbaji kama ilivyo
kawaida yao ambapo wakati wa uchimbaji huo marehemu na mwenzake aitwaye Tungu
Thomas walikuwa wameingia shimoni na nje shimo walimuacha mwenzao ambaye ni Edson
David Akiba ambapo baada ya muda mfupi kilisikika kishindo kutoka ndani ya
shimo.
Kutokana
na hali hiyo Edson David alijaribu
kuwaita wenzake waliokuwa shimoni hawakuitika ndipo harakati za kuwasaidia
zilipofanyika kwa kuwaita wachimbaji wengine wa maeneo jirani ambapo baada ya
kuingia marehemu alikutwa kafunikwa na udongo akiwa tayari kafariki dunia huku
mwenzake Tungu Thomas akiwa amejeruhiwa kichwani.
Aidha
Kamanda Kidavashari amesema,kwa mujibu wa uchunguzi wa kitabibu kifo cha
marehemu kilitokana na majeraha aliyoyapata kichwani (HEAD INJURY) na mwili
wake ulikabidhiwa kwa ndugu zake kuendelea na taratibu zingine za mazishi, huku
Tungu Thomas akipatiwa matibabu katika
hospitali ya Katuma na kuruhusiwa kwenda kujiuguzia nyumbani.
Hata
hivyo si mara ya kwanza matukio kama haya kutokea ikizingatiwa kuwa hivi
karibuni wachimbaji wadogo walifukiwa katika mgodi wa Nyangalata uliopo
Wilayani Kahama.
Posted By:Issack Gerald
| At:Thursday, December 24, 2015
Na.Issack Gerald-Mpanda
Jeshi
la polisi Mkoani Katavi linamtafuta mtu mmoja aliyekimbia akikwepa kukamatwa na
polisi kutokana na kumiliki silaha aina ya gobore kinyume na sheria.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amethibitisha mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Malugumba Nzinza kukamatwa na silaha aina ya gobore
ambayo imepatikana ikiwa imefichwa katika nyumba yake.
Kamanda
kidavashari amesema mtu huyo alikamatwa,mnamo tarehe 12.12.2015 majira ya saa
12:00 katika kijiji cha Mpembe Kata na
Tarafa ya Mwese Wilayani Mpanda Mkoa wa
Katavi.
Kamanda
amesema kuwa katika tukio hilo,Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na askari wa
wanyama pori (TANAPA) walipata taarifa toka kwa raia wema kuwepo kwa mtu
anayehisiwa kumiliki silaha kinyume na utaratibu.
Mpaka
sasa mtuhumiwa bado hajakamatwa na misako mbalimbali inaendelea katika
kuhakikisha mtuhumiwa anatiwa nguvuni na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma
inayomkabili.
Posted By:Issack Gerald
| At:Thursday, December 24, 2015
NA.Mwandisi
wetu-MWANZA
Askari
mmoja wa jeshi la Polisi mkoani Mwanza jana amefyatua risasi na
kumuua asikari mwenzake kisha nayeye kujipiga risasi na kufariki dunia katika
lindo la benki ya posita jijini mwanza huku chanzo cha tukio hilo kikiwa hakija
julikana.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza kamishina msaidizi wa Polisi Justus Kamugisha
amethibitisha kutokea kwa tukio na kwamba limetokea majira ya saa nane na nusu
mchana katika lindo la Banki ya Posta tawi la Pamba jijini Mwanza.
Kamanda
Kamugisha amewataja askari hao kuwa ni Konstebo H 852 Daud Masunga Elisha
aliyempiga risasi Pc Petro Simoni Matiko H5950 eneo la begani na baadae Pc
Masunga kujipiga risasi eneo la paji la uso na kufariki pao hapo, wote ni askari
wa wilaya ya Nyamagana
Aidha
Kamanda Kamgisha amesema jeshi la Polisi lina endelea na uchunguzi juu ya tukio
hilo ili kubaini chanzo cha mauaji hayo.
Posted By:Issack Gerald
| At:Friday, December 25, 2015
Na.Issack Gerald-Mpanda
Jeshi
la polisi Mkoani Katavi linawashikilia watu watatu kutokana na kukamatwa na
nyara za serikali ambazo wamezipata kinyume na sheria.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amewataja wanaoshikiliwa na polisi
kuwa ni Leonard Mbegele(38) mkazi wa Migazini na Anastazia Bernad(38) mkazi wa
kichangani ambao walikamatwa mnamo tarehe 22.12.2015 majira ya saa 13:00 maeneo
ya Mikocheni Tarafa ya Kashaulili Wilayani Mkoani Katavi wakiwa na nyama ya
Kongoni kilo moja.
Kamanda
amesema kuwa Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema
lilifanya upekuzi nyumbani kwa Anastazia Bernard ambapo nyama hiyo ilikutwa
ikiwa imewekwa kwenye Hotpot iliyokuwa ndani ya kabati.
Katika
upelelezi wa awali wa tukio hiliAanastazia alidai kuwa nyama hiyo ni ya Malack
Jonas ambapo hata hivyo Jonas naye aliikana nyama hiyo.
Mpaka
sasa watuhumiwa wote wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi na watafikishwa
mahakamani baada ya Upelelezi kukamilika.
Wakati
huo huo Leornard Mbegele (38) Mkazi wa migazini Kata ya Nsemulwa, Tarafa ya
Kashaulili, Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Mnamo tarehe 22.12.2015 majira ya
saa 14:00 anashikiliwa na alikamatwa
akiwa na nyama ya Kongoni kilo 15.
Mtuhumiwa
anatarajiwa kufikishewa mahakamani upelelezi utakapokamilika.
KUKAMILIKA KWA IDADI YA MAWAZIRI WANAOUNDA BALAZA LA MAWAZIRI.
RAIS John Magufuli amemalizia kujaza nafasi za uteuzi wa
Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza wakati akitangaza Baraza la Mawaziri la
Kwanza katika awamu ya tano ya utawala wake.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,
Ikulu, Gerson Msigwa kwa vyombo vya habari, Dar es Salaam jana, katika uteuzi
wake Rais Magufuli amemteua Profesa Jumanne Maghembe kuwa Waziri wa Maliasili
na Utalii.
Aidha, Dk Philip Mpango aliyekuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.
Amemteua kuwa Mbunge na kumteua pia kuwa Waziri.
Rais Magufuli pia amemtangaza Profesa Makame Mbarawa kuwa
Waziri mpya wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, akimhamisha kutoka Wizara ya
Maji na Umwagiliaji. Naibu Waziri wa zamani wa Ujenzi, Gerson Lwenge ameteuliwa
kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
Aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Ufundi ni Dk Joyce Ndalichako ambaye mapema jana aliteuliwa kuwa Mbunge. Dk
Ndalichako aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza na Mitihani la Taifa (NECTA).
Katika uteuzi wake mwingine, Rais Magufuli amemteua Hamad
Masauni kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Waziri wake ni Charles
Kitwanga. Rais Magufuli, Desemba 9 mwaka huu alitangaza kuunda wizara 18 zenye
mawaziri 19. Mawaziri hao na wizara zao kwenye mabano ni George Simbachawene na
Angela Kairuki (Ofisi ya Rais-Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora) wakati Naibu
wa wizara hiyo na Selemani Jaffo.
Wengine ni Mwigulu Nchemba (Kilimo, Mifugo na Uvuvi) na Naibu
wake ni William ole Nasha, Jenista Mhagama (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu), Balozi Augustine Mahiga (Mambo ya Nje na Afrika Mashariki). Naibu
wake ni Dk Suzan Kolimba.
William Lukuvi (Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi) ambaye Naibu wake ni Angelina Mabula, Ummy Mwalimu (Waziri wa Afya,
Jinsia, Wazee na Watoto) na Naibu wake ni Dk Hamisi Kigwangalla.
Waziri wa Nishati na Madini ni Profesa Sospeter Muhongo
ambaye Naibu wake ameteuliwa Dk Medard Kalemani. Waziri wa Katiba na Sheria ni Dk
Harison Mwakyembe na Waziri wa Ulinzi ni Dk Hussein Mwinyi.
Aidha, Nape Nnauye aliteuliwa kuwa Waziri wa Habari na
Michezo na Naibu wake ni Anastazia Wambura. January Makamba aliteuliwa Waziri
katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) na Naibu wake ni Luhaga
Mpina.
Katika uteuzi wa awali, Rais Magufuli alimteua Charles
Mwijage kuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Wengine walioteuliwa
kuwa Naibu Mawaziri, wakati wizara zao zikisubiri mawaziri kamili ni Edwin
Ngonyani (Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano), Ashantu Kijaji (Wizara ya Fedha),
Ramo Makani (Maliasili na Utalii) na Stella Manyanya (Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi).
Naibu Waziri mwingine ni Isack Kamwela wa Maji na
Umwagiliaji. Wakati huo huo, Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, Alphayo Kidata ameteuliwa kuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA.
“Mbali ya kukamilisha uteuzi wa Baraza lake la Mawaziri, Rais
Magufuli pia amewatakia heri Watanzania wote katika Sikukuu za Maulid, Krismasi
na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu,” ilieleza taarifa
hiyo ya Ikulu.
Comments