MKURUGENZI HALMSHAURI YA WILAYA YA KALAMBO,ASIKITISHWA NA HALI YA ELIMU MKOANI RUKWA


Na.Issack Gerald-SUMBAWANGA
MKURUGENZI  Mtendaji wa  Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa Bw. Bensoni Kilagi,amesema hajaridhishwa na matokeo ya darasa la nne na darasa la saba kwa mwaka 2015 mkoani humo.
Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Kwa njia ya simu,Bw. Kilagi  amesema matokeoa yameendelea kuwa mabaya ambapo kwa mwaka  2014 ufaulu ulikuwa asilimia thelathini huku mwaka 2015 ufaulu huo ukipanda kwa salimia 10 na kufikia asilimia 40.
Aidha amesema ili kunusuru hali ya elimu Mkoani humo,wamekusudia kuitisha vikao vya mara kwa mara vinavyohusisha wadau wa elimu wakiwemo wazazi,walezi,watendaji na wataalamu wengine wa masuala ya elimu ili kuongeza kiwango cha ufaulu.
Hata hivyo Bw.Kilangi amezitaja baadhi ya changamoto zinazopelekea kufanya vibaya katika suala zimala elimu  ni kutofanya mazoezi ya mitihani mara kwa mara ,madawati pamoja na nyumba za walimu.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA