Posts

Showing posts from October 20, 2017

WAZIRI LUKUVI MKOANI RUKWA NA MASUAL AYA MIGOGORO YA ARDHI

Image
Uzembe na utendaji kazi wa kimazoea kwa baadhi ya watendaji wa serikali wakati wa ubinafsishaji wa shamba la Mlonje Dafco lenye ukubwa wa hekta 10,000 na kumpa mwekezaji Tasisiya Efatha Ministry umewagharimu wananchi na kuibua migogoro ya mara kwa mara baina ya mwekezaji huyo na vijiji jirani vinavyozunguka shamba hilo.

TPA MKOANI RUKWA IMETOA MSAA WA SHUKA 1245 KATIKA IDARA YA AFYA

Image
MAMLAKA ya bandari nchini(TPA) imetoa msaada wa mashuka 1245 yenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa halmashauri ya wailaya ya Nkasi kwaajili ya idara ya afya wilayani humo. Mkurugenzi wa bandari nchini Desderius Kakoko alisema kuwa msaada huo wanatoa katika halmashauri ambazo zina bandari kote nchini ikiwa ni sehemu ya kutoa ahasante wa halmashauri hizo. Alisema kuwa mamala ya bandari nchini inachangia nusu ya makusanyo ya taifa kwa mwezi ambayo ni shilingi bilioni Mia 5.5 ambapo inatumika katika matumizi ya serikali.  Kakoko alisema kuwa kutokana na wilaya ya Nkasi kuwa na mahitaji katika idara ya afya mamlaka hiyo imeamua kuchangia mashuka ikiwa ni katika jitihada za kupunguza matatizo kwa wananchi.  Alisema nchi ya tanzania inapakana na nchi nane ambazo hazina bandari nazinategemea bandari zilizopo hapa nchini hivyo basi nifursa nzuri ya kuhakikisha kuwa uchumi unakua nakuongeza pato la taifa. Akishukuru kwa msaada huo mbunge jimbo la Nkasi Kaskazini Ally Kessy alisema

SERIKALI KUSHGHULIKIA HAKI ZA WALIMU

Image
SERIKALI imesemna itaendelea kushughulikia haki za walimu pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili walimu ikiwa ni pamoja na kushirikiana na chama cha walimu Tanzania ili walimu waendelee kufanya kazi katika mazingira rafiki kwa manufaa yao na taifa.

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA ASKOFU

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania ( TEC ) Mhashamu Tercisius Ngalalekumtwa kufuatia kifo cha Askofu wa Jimbo Katoliki la Tunduru Masasi Mhashamu Castory Msemwa, kilichotokea jana tarehe 19 Oktoba, 2017 nchini Oman.

BARAZA LA MITITHANI LATANGAZA MATOKEO DARASA LA SABA

Image
Baraza la Mitihani Taifa NECTA limetangaza matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2017, na kusema kuwa ufaulu umeongezeka kwa 2.4% ukilinganisha na ule wa mwaka jana 2016.