Posts

Showing posts from January 31, 2018

MBUNGE ALIYESIMAMIA KIAPO CHA RAILA ODINGA AKAMATWA

Image
Mbunge wa Ruaraka Tom J Kajwang’ ambaye jana Jumanne alisimamia “kuapishwa” kwa kiongozi wa muungano wa Nasa Raila Odinga kwenye viwanja vya Uhuru Park Jumanne amekamatwa. Mbunge huyo amekamatwa leo mchana na maofisa wa polisi ambao hawakuwa wamevalia sare nje ya Mahakama ya Milimani jijini Nairobi. Alikamatwa muda mfupi baada ya kuhudhuria katika Mahakama Kuu mbele ya Jaji George Odunga kusikiliza uamuzi wa kesi aliyowawakilisha wabunge wanaopinga kukatwa mishahara yao na posho. Kajwang’ na mwanasheria mwingine Miguna Miguna,ndio walikuwa wasimamizi wakuu wa matukio katika viwanja vya Uhuru Park yaliyomalizikia kwa “kuapishwa” Odinga kama ‘rais wa wananchi’. Wakati wa sherehe za kiapo Kajwang’ alikuwa amevaa vazi na wigi na alishangiliwa sana na wafuasi wa Nasa. Odinga alikula “kiapo” huku Kajwang’ akiwa amesimama nyuma yake japokuwa wajibu wake katika tukio hilo bado haujafahamika. Habari zaidi niP5TANZANIA LIMITED

RAIS MUSEVEN ATOA MILIONI 30 KUFANIKISHA MATIBABU YA RADIO

Image
Rais wa Uganda Yoweri Museven ametoa shilingi Milioni 30 kwa ajili ya  matibabu ya msanii Radio. Msanii Radio ambaye amekuwa akifanya kazi na mwenzake Weasel alipata ajali January 23 mwaka huu na hali yake inaripotiwa kuwa mbaya. Hapo jana taaarifa ilitolewa kupitia ukurasa wa Instagram wa Radio na Weasel ilieleza kuwa February 4 mwaka huu kutafanyika maombi maalumu kwa ajili ya kumuombea Weasel. Habari zaidi niP5TANZANIA LIMITED

RAIS MAGUFULI AMTEMBELEA MZEE MAJUTO HOSPITALI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli amemtembelea muigizaji mkongwe,Mzee Majuto katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam ambako amelazwa akitibiwa. Akizungumza mara baada ya kutembelewa na Rais, Mzee Majuto amefunguka na kudai yeye ndio mtu wa kwanza kutabiri ujio wa Rais Magufuli katika kuongoza nchi ya Tanzania huku akisisitiza kwamba anajisikia faraja kuona ana misimamo iliyokuwa imara. Pamoja na hayo,Mzee Majuto aliendelea kwa kusema ; “sisi wazee tunafarijika sasa hivi,viwanda kila kona vimetapakaa na leo amekuja kutembea hospitalini hapa sijui kama wengine hawajikojolea huko kwa uoga maana hataki masihara. Kwa upande mwingine, Mzee Majuto amesema sio rahisi kupata Rais mwenye misimamo na asiyekuwa na masihara kama Dkt.John Magufuli. Chanzo:Bongo5.com Habari zaidi niP5TANZANIA LIMITED

KUIPATA PASIPOTI ILIYOZINDULIWA NA RAIS NI SH.150,000

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Dkt. Mwigulu Nchemba amesema gharama mpya ya hati ya kusafiria (Pasipoti) ya kielektroniki  iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli ni Shilingi 150,000. Dk Nchemba amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Pasipoti hiyo jijini Dar es Salaam. Amesema Pasipoti hizo zitakuwa na ukurasa zaidi ya mmoja  na mwonekano mpya. Hata hivyo Rais Magufuli amesema gharama ya Shilingi 150,000 ni ya juu kidogo kuliko bei ya sasa huku kieleza kuwa bei hiyo imezingatia ubora wa utengenezaji wa Pasipoti hiyo. Habari zaidi niP5TANZANIA LIMITED