Posts

Showing posts from January 11, 2018

UHABA WA VYUMBA VYA MADARSA MKOANI KIGOMA WANAFUNZI ZAIDI YA 2000 WAKOSA KUJIUNGA NA SEKONDARI.

Image
Upungufu wa vyumba   vya madarasa wilayani Uvinza Mkoani Kigoma imekuwa sababu ya zaidi ya wanafunzi 2000 kukosa nafasi ya kujiunga na masomoa ya sekondari kwa mwaka 2018. Kutokana na hali hiyo,imewalazimu wakazi wa kijiji cha Nyanganga wilayani humo kuamua kuanza ujenzi wa shule ya sekondari ili wanafunzi waliochaguliwa waanze masomo. Wilaya hiyo ina upungufu wa vyumba vya madaras 73 ambapo hata hivyo wanafunzi wengi wanalzamika kusafiri umbali wa karibu masaa 3 kutoka nyumbani kufuata shule katika vijiji vya jirani na wengine kulazimika kuhama nyumbani kuishi karibu na shule hizo. Kama sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo, Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na watoto Dk.Fustine amechangia mifuko 20 ya saruji na kuwataka wananchi kushirikiana katika miradi mbambali ya maendeleo yao. Nao Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bw.MwanamvuaMlindo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Weja Ngolo wametoa pamoja na kusema kuwa wameweka mikak

RAIS MAGUFULI AMEMTEUA ALIYEKUWA KATIBU MKUU IKULU BW.ALPHAYO KIDATA KUWA BALOZI

Image
Rais John Magufuli ameteua mabalozi wapya wawili ambao ni Alphayo Kidata na Meja Jenerali Mstaafu,Simoni Mumwi. Alphayo Kidata Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu,Gerson Msigwa imesema Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi John Kijazi amesema uteuzi wa Kidata umeanza jana Jumatano Januari 10. Kabla ya uteuzi huo Kidata alikuwa Katibu Mkuu,Ikulu. Taarifa hiyo imeeleza kuwa mabalozi hao wateule watapangiwa vituo vyao vya kazi na kuapishwa baada ya taratibu kukamilika. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

SUALA LA AIRTEL MIKONONI MWA RAIS,WAZIRI WA AFYA NA SHERIA NAO WATEKELEZA MAAGIZO YA RAIS

Image
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Isdor Mpango leo amewasilisha taarifa ya kamati aliyoiunda kuchunguza umiliki wa kampuni ya simu Airtel kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli aliyeagiza kufanyika kwa uchunguzi huo Desemba 20 mwaka jana. Dkt.Philipo Mpango Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo,Dkt.Mpango amesema Serikali imejiridhisha kuwa ubinafsishaji wa Shirika la Simu Tanzania ( TTCL ) kwenda Celtel,baadaye kuhamishiwa Zain na sasa Airtel ulifanyika kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria,kanuni na taratibu. Kufuatia ukiukwaji huo Dkt.Mpango amesema Serikali inayomiliki asilimia 40 ya hisa za kampuni ya Airtel imeamua kufanya mazungumzo na kampuni ya Airtel inayomiliki asilimia 60 ya hisa ili nchi iweze kupata haki yake. Dkt.Ummy Mwalimu Wakati huo huo, Mhe.Rais Magufuli amepokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Novemba 25 mwaka jana wakati wa ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirik

NAIBU WAZIRI AWAKABIDHI SILAHA MADEREVA BODABODA MKOANI KATAVI TAYARI KUPAMBANA NA MIMBA ZA UTOTONI

Image
Na.Issack Gerald Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile,amewataka waendesha pikipiki Mkoani Katavi kushirikiana na serikali ili kutokomeza mimba za utotoni. Dk.Ndugulile ametoa agizo hilo leo wakati akitunuku vyeti kwa waendsha pikipiki 100 wa Manispaa ya Mpanda waliohitimu mafunzo ya kidhibiti Mimba za utotoni huku akiwataka pia watendaji wa wizara mpaka wilaya kote nchini kutatua shida zinazowakabili madereva hao. Wakati huo huo Dk.Ndugulile amekabidhi baiskeli tano kwa wasimamizi wa mashauri ya watoto Manispaa ya Mpanda baiskeli ambazo zimetolewa na shirika la JSI la Marekani ili baiskeli hizo zitumike kuwafikia watoto waishio katika mazingira hatarishi. Kwa upande wake Mwenyekiti wa waendesha pikpiki Mkoani Katavi Mh.Asalile Mwakabafu amesema wao watahakikisha wanashiriki kudhibiti mimba za utotoni huku akisisitiza serikali kusimamia watendaji wake wasioshughulikia matatizo ya waendesha pikipiki Mkoani Katavi. Kwa upan