Posts

Showing posts from April 2, 2018

MKE WA ZAMANI WA NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA-FAHAMU HISTORIA YAKE

Image
WINNIE MANDELA ,mke wa zamani wa Nelson Mandela, ambaye pia alipigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini amefariki dunia akiwa na miaka 81. Habari za kifo chake zimethibitishwa na msaidizi wake. Winnie alizaliwa mnamo 26 Oktoba mwaka 1936,na ingawa yeye na mumewe - Nelson Mandela - walitalikiana mapema miaka ya 1990,Winnie Madikizela Mandela kama alivyofahamika rasmi alisalia kutoa mchango katika maisha ya Bw.Mandela. Msemaji wa familia Victor Dlamini amesema kupitia taarifa kuwa:"Amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu, ambapo amekuwa akiingia na kutoka hospitalini mara kwa mara tangu mwanzo wa mwaka na alifariki mapema leo Jumatatu adhuhuri akiwa amezungukwa na familia na wapendwa wake." Kwa mjibu wa shirika la habari la AFP Askofu mstaafu na mshindi wa tuzo ya Nobel Desmond Tutu amemsifu kama "ishara kuu ya vita dhidi ya ubaguzi wa rangi ambapo Winnie alikuwa na miaka 20 hivi akiwa katika siasa. Alisomea kazi ya utoaji huduma za kijamii na

MUFTI ZUBERI AFUNGA MKTANO MKUU WA BAKWATA AWAASA WAISLAMU KUBADILIKA

Image
Mufti Mkuu wa Tanzania,Sheikh Abubakar Zuberi, amesema wakati umefika kwa Baraza Kuu la Waislaam Tanzania,BAKWATA kubadilika ili kuendesha shughuli zake kiuweledi na kuachana na kufanya kazi kwa mazoea. Mufti Zuberi ametoa rai hiyo Mjini Dodoma leo wakati akifunga mkutano mkuu wa siku mbili wa Bakwata. Amesisitiza haja ya baraza hilo kuelekeza nguvu zake katika kuwahudumia waumini wa dini ya Kiislaam nchini ambapo amesema kufanya kazi katika mtindo huo kunalenga kuwaunganisha Waislaam . Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Elimu wa Bakwata, Sheikh Ali Abdallah Ali amesema,mkutano huo umewasilisha mapndekezo ya maazimio 32 kwa lengo la kulijenga baraza hilo. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MWAKA 2018 ATAJA MIKOA INAYOONGOZA KWA UTORO SHULENI

Image
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa amezindua mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2018. Akizindua mbio hizo kitaifa Mkoani Geita,amewataka viongozi wa mikoa ya Tabora,Geita,Mtwara na Shinyanga ambayo inaongoza kwa utoro wa wanafunzi kwa shule za sekondari wahamasishe umuhimu wa elimu na mahudhurio endelevu shuleni. Akizungumzia kuhusu utoro kwa shule za sekondari nchini,Waziri Mkuu amesema mkoa wa Tabora unaongoza kwa utoro kwa kuwa na silimia 9.7,Geita asilimia 8.1,Mtwara asilimia 6.4 na Shinyanga asilimia 6.3. Kuhusu utoro wa wanafunzi wa shule za Msingi nchini, Waziri Mkuu amesema mkoa unaoongoza ni wa Rukwa kwa asilimia 3.2,Geita asilimia 3.1,Tabora asilimia 2.9, Simiyu asilimia 2.0 na Singida asilimia1.9. Aidha Waziri Mkuu amesema dhamira ya Serikali ni kuwashirikisha wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo kuwekeza katika elimu na kuzalisha rasilimali watu yenye ujuzi na stadi zitakazowezesha kuchochea mapinduzi ya viwanda ili nchi iwe ya

RAIS MAGUFULI APUZILIA MBALI WARAKA WA MAASKOFU

Image
Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ameupuuzilia mbali waraka wa maaskofu uliotolewa wakati wa kuanza kwa msimu wa Pasaka akisema hauna msingi wowote ule. Rais Magufuli amesema hayo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa rada za kuongozea ndege jijini Dar es Salaam. Majibu yake kwa waraka wa maaskofu aliyatoa wakati akiwapongeza wasaidizi wake, mawaziri,viongozi wa ulinzi na usalama pamoja na wasaidizi wengine akisema wanaendelea kutimiza vizuri majukumu yao. Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kujibu moja kwa moja waraka uliotolewa na maaskofu wa kanisa la Kilutheri nchini Tanzania siku chache zilizopita ambao pamoja na mambo mengine ulionya juu ya mwenendo wa demokrasia nchini Tanzania. Katika waraka wa ujumbe wa Pasaka uliosomwa katika makanisa ya Kilutheri kote nchini Tanzania na kusambaa katika mitandao ya kijamii,baraza hilo liliorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi hiyo. Walitaja baadhi ya mambo hayo kuwa