Posts

Showing posts from September 16, 2016

WAKAZI WILAYANI TANGANYIKA WAAGIZWA KUONGEZA KASI YA KUJENGA SEKONDARI KILA KATA

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Tanganyika WAKAZI wilayani Tanganyika Mkoani Katavi kwa Kushirikiana na uongozi wa vijiji na kata   katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika,wameagizwa kuweka mikakati ya ujenzi wa shule za Sekondari kila kata ,ili kila mwanafunzi asome bila kuhangaika na badala yake apate elimu bora.                                       Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh Mbwana Mhando akishiriki ujenzi Shule ya sekondari ya Bulamata  kata ya Bulamata(PICHA NA Issack Gerald)Septemba 16,2016                                          Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika akizungumza na wananchi eneo la kijiji cha Busongola kunakojengwa Shule ya Sekondari Bulamata(PICHA NA.Issack Gerald) Septemba 16,2016                                                       Wananchi wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Isubangala kijiji cha Isubangala kata ya Ilangu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya(hayupo pichani)(PICHA NA.iSSACK gERALD) Septemba 16,2016

MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AAGIZA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 200 ZA WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU CHAMA CHA USHIRIKA TAMCOS KULIPWA NDANI YA SIKU 15.

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Tanganyika MKUU wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Bw.Saleh Mbwana Mhando,ameuagiza uongozi wa bodi ya Chama cha Msingi cha Ushirika TAMCOS na Afisa Ushirika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Luxford Mbunda,kuhakikisha wanalipa   zaidi ya Shilingi milioni 200 wanazodai wakulima wa zao la tumbaku wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwa misimu 3 ya kilimo kuanzia mwaka 2011-2015 kabla ya Septemba 30 mwaka huu. Baadhi ya Wakulima wa Zao la Tumbaku wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika(hayupo pichani) katika Ofisi za TAMCOS Mishamo(PICHA NA.Issack Gerald) Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh Mbwana Mhando Aliyesimama akihutubia wakulima wa tumbaku wa chama cha Msingi cha Ushirika TAMCOS Mishamo(PICHA NA.Issack Gerald)                                       Wakulima wa chama cha Msingi cha Ushirika TAMCOS Mishamo wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika(hayupo pichani) katika mkutano wa hadhara uliofanyika Septemba 15,2016 kati