Posts

Showing posts from February 14, 2018

RAIS MAGUFULI AMTEUA MNADHIMU WA JWTZ APANDISHA VYEO MABRIGEDIA 10 KUWA MAJENERALI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli leo amemteua Meja Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Rais wa Tanzania Mh.Dkt John Pombe Magufuli Pamoja na uteuzi huo,Mhe.Rais Magufuli amempandisha cheo kutoka Meja Jenerali na kuwa Luteni Jenerali. Kwa mjibu wa taarifa ambayo imetolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais ikulu ya Rais,Gerson Msigwa Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa ambaye amestaafu. Aidha,Mhe.Rais Magufuli amewapandisha vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali wafuatao; 1.                          Brig Jen. J.G. Kingu 2.                         Brig Jen. M.S. Busungu 3.                         Brig Jen. R.R. Mrangira 4.                        Brig Jen. B.K. Masanja 5.                         Brig Jen. G.T. Msongole 6.                        Brig

DC ACHARUKA WANANCHI KUTAPELIWA FEDHA ZA MASHINE ZA EFDs

Image
SERIKALI mkoani Katavi imetoa siku 14 kwa makampuni na wafanyabiashara waliochukua fedha kwa ajili ya kuwauzia mashine za EFDs wafanyabishara na mpaka sasa hawajui hatma ya fedha zao. Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lllian   Matinga alitoa siku hizo jana   katika kikao maalumu cha kusikiliza kero za wafanyabiashara wa mkoa huo akimwakilisha mkuu wa mkoa huo Meja jenerali   Mstaafu   Raphae Muhuga. Alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuwepo kwa makampuni yaliyokusanya fedha kutoka kwa wafanyabiashara na kuahidi kuwapelekea mashine za EFDs lakini mpaka sasa hawajapatiwa mashine hizo.

AUAWA KWA KUKANYAGWA NA TEMBO

Image
MWANAMKE   aliyefahamika kwa jina la Maria Sekaye(60) mkazi wa kijijii cha Ilambila wilayani Kalambo   Mkoani Rukwa ameuawa baada ya kukanyagwa na tembo. Tembo hao wanaelezwa kuwa walikuwa njiani wakitokea katika pori la akiba la Lwafu mkoani Rukwa kuelekea katika nchi jirani ya Zambia. Akizungumzia tukio hilo diwani wa kata ya Mkowe Alfred Mpandasharo alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 4 za asubuhi wakati mwanamke huyo akiwa ametoka kutembelea shamba lake lililokuwa limevamiwa na mazao kuliwa na tembo hao.

FAHAMU ASILI NA MAANA HALISI YA SIKU YA WAPENDANAO’’VALENTINE DAY’’

Image
Siku ya Valentines Day asili yake ni kutoka Dola ya Warumi. Ni siku ya kumbukumbu (memoria day) na sehemu nyingine ni (festum) maana yake siku kuu ya daraja la kwanza kwa kumkumbuka Padre Valentine aliyeuawa na utawala wa kirumi kwa Sababu ya kutetea waumini wake kufunga ndoa badala ya kuishi na vimada tu. Lakini sikukuu hiyo imeenea sana katika nchi za magharibi na baadaye karibu sehemu kubwa ya ulimwengu kuisherehekea kama siku yamapenzi kinyume cha dhamira ya Mt.Valentine. Watawala wa dola ya kirumi walikuwa na fikra za kueneza dola ya kirumi duniani kote na hivyo vijana hawakutakiwa kuoa,ili wawe huru muda wote kwenda vitani kupigania nchi kwa sababu kwamba wakioa wasingekuwa na uhuru wa kwenda vitani bali kuwa na famiia zao. Vijana wengi wakawa na mtindo wa kuwa na vimada tu kitu ambacho kanisa lilikukwa linapinga. Padre Valentine ambaye alikuwa Roma akawa anawahimiza vijana kufunga ndoa badala ya kufanya ngono bila ndoa kwani ni dhambi na kitu kisichokubalika mbele

MPANDA RADIO YAONGOZA WANANCHI KATAVI KUSHEREHEKEA VALENTINE DAY KWA KUCHANGIA DAMU SALAMA

Image
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Mh.Salehe Mbwana Muhando,amekipongeza kituo cha matangazo cha Mpanda Radio kwa kuadhimisha siku ya wapendanao kwa kuwaunganisha Watanzania kwa kuchangia damu salama ili kunusuru wagonjwa. Akizindua kampeni hiyo ya uchangiaji damu salama iliyoandaliwa na kuratibiwa na Mpanda Radio Muhando ambaye amemwakilisha Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga,amewataka Watanzania kuwa na moyo wa kujitolea katika mambo mbalimbali ya kijamii ikiwemo uchangiaji damu salama kwa ajili ya watu wenye uhitaji. Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mpanda Radio Bi.Salome Mchawa,amesema Mpanda Radio kama radio ya kijamii itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kujali mahitaji ya jamii huku akiwashukuru na kupongeza watanzania kwa kuunga mkono kampeni ya uchangiaji damu salama iliyoanzishwa na Mpanda Radio kama kushrehekea siku ya wapendanao’’ Valentine Day’’. Kituo cha Matangazo cha Mpanda Radio Fm kilichoanzishwa mwaka 2013 na kuzinduliwa na mwenge wa