Posts

Showing posts from April, 2018

MANISPAA YA MPANDA YATANGAZA KUUWA MIFUGO

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Bw.Michael Francis Nzyungu ametangaza kuwa kuanzia Aprili 25 mwaka 2018 itakuwa ni oparesheni ya kuuwa mifugo inayozurura ovyo mitaani hususani Mbwa. Katika taarifa yake mahususi kwa ajili ya Oparesheni hiyo itakayofanyika eneo lote la manispaa ya Mpanda,amewataka   wafugaji wote katika Manispaa hiyo kufungia mifugo yote ikiwemo Ng’ombe, mbuzi, Kondoo, nguruwe na mbwa. Katika Manispaa ya Mpanda imekuwa hali ya kawaida mifugo kuzurura ambapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakilalamika kuharibikiwa na mazao au mali za nyumbani. Tangazo la Mkurugenzi linakuwa na aina yake kwa kuwa mara nyingi imezoeleka maonyo ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakitolewa na Maafisa watendaji wa mitaa,kata na mitaa bila mafanikio ambapo zaidi wamekuwa wakipigwa faini wenye mifugo.   Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com  

RADI YAUA MWANAFUNZI RUKWA

MWANAFUNZI wa darasa la pili shule ya msingi Kipundu James Kandege (8) amefariki dunia baada ya kupigwa radi juzi jioni akiwa nyumbani kwao na wenzake. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na afisa mtendaji wa kijiji cha Mabatini kata ya Namanyere Ibrahimu Adriano alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi jioni majira ya saa 10 alipokuwa ameketi nyumbani na wenzie walipokuwa wakila chakula cha mchana. Alisema kuwa marehemu akiwa na wenzie sambamba na waza zi wake wakila chakula katika kitongoji cha Katowa kijiji cha Mabatini walipigwa na radi wakiwa ndani ya nyumba yao na mwanafunzi huyo alifariki dunia papo hapo huku wengine wakisalimika. Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kipundu Josephat Laban athibitisha kutokea kwa kifo cha mwanafunzi huyo ambapo alisema kuwa shule hiyo iliwaruhusu Wanafunzi wote walishiriki katika msiba huo sambamba na mazishi huku akidai kuwa shule imempoteza mtu muhimu. Diwani wa kata ya Namanyere Evarist Mwanisawa alisema kuwa Mwanafunzi huyo alikua ni mka

AACHIWA MKE KWA LAKI 8 BAADA YA KUFUMANIWA

MKAZIwa kijiji cha Ntumba kilichpo wilayani Tanganyika katika mkoa wa Katavi,Charles Sabuni (37)  amepwa  viboko 30 hadharani baada ya kushikwa ugoni na mke wa jirani yake Ntema Mwiwela,juzi usiku wa manane kijijini hapo. Kwa mujibu wa Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa adhabu hiyo  alipewa mgoni huyo ili iwefundisho kwake na  kwa wanaume wengine wenye tabia kama hiyo. Akisimulia tukio hilo mwenyekiti wa Kitongoji cha Ntumba Samwel Mbuya alisema lilitokea saa tisa usiku, juzi nyumbani kwa Mwiwela ambaye anaishi jirani na Sabuni. Akifafanua alisema kuwa mchana wa siku hiyo ya tukio hilo Mwiwela alimuaga mkewe kuwa ana safiri ambapo alirejea nyumbani kwake ghfla usiku wa manane na kumkuta Sabuni akiwa amelala chumbani kwake. “Mwenye mke alimthibiti mgoni wake huyo asitoroke huku akimwamuru apige mayowe huku akisema anaomba msaada kwani amefumaniwa na mke wa mtu ….. kele hizo ziliwaamsha wanakijiji wenzake ambao walikimbilia eneo la tukio na  walipigwa na kutwaa kumkut

RAIS MAGUFULI ATEUA MWENYEKITI BODI YA WAKURUGENZI BENKI YA POSTA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt.Edmund Bernard Mndolwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania ( TPB ). Kwa mjibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,Ikulu Gerson Msigwa,Uteuzi wa Dkt.Mndolwa umeanza tarehe 23 Aprili, 2018. Dkt.Mndolwa anachukua nafasi ya Prof.Lettice Rutashobya ambaye amemaliza muda wake. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com   

WANANCHI NSIMBO WAOMBA KUBORESHEWA HUDUMA YA MAJI DIWANI AKATAA KUWEKA WAZI MIPANGO

Wananchi wa kijiji cha Mtakuja kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,wameiomba serikali kushughulikia miundombinu ya huduma ya maji kijijini hapo ili wananchi waondokane na tatizo la kutofanya shughuli za maendeleo kwa sababu ya kupoteza muda mrefu wkifuatilia maji. Wamesema serikali imekuwa ikisema itaongeza mabomba ya maji ambapo mpaka sasa hakuna mipango inayotekelezwa kadri siku zinavyosonga mbele licha ya viongozi mbalimbali wakiwemo Mbunge wa Nsimbo na Diwani wa kata hiyo kutoa ahadi. Mwenyekiti wa kijiji cha Mtakuja Daud Peter Nyasio amekiri hali ya huduma ya maji katika kijiji hicho kuwa mbaya ambapom amesema visima viwili vilivyopo havikidhi idadi ya wananchi zaidi ya elfu tatu wa kijiji hicho wanaotakiwa kuapa maji. Hata hivyo Reward Sichone ambaye Diwani wa Kata ya Kapalala inayojumuisha vijiji vya Mtakuja,Songambele na Kapalala ameiambia Mpanda Radio kuwa hana jambo lolote la kuzungumza na chombo cha habari kuhusu suala la maji katika kata ya Kapal

ACT-WAZALENDO KATAVI WATOA MAAZIMIO MIGOGORO YA ARDHI KATAVI

Chama cha ACT-Wazalendo mkoani Katavi kimeazimia kuishinikiza serikali kuchukua hatua za utatuzi wa migogoro ya ardhi inayowakabili  wananchi katika maeneo mbalimbali mkoani Katavi. Joseph Mona ambaye ni Katibu wa Chama cha ACT Wazalendo mkoani Katavi akizungumza katika mkutano wa chama hicho amesema kikao hicho kilichofanyika jana kililenga kufanya tahimini ya namna ambavyo serikali ya mkoa inavyoshughurikia migogoro ya ardhi inayoendelea kufukuta. Mona ametaja baadhi ya kero za wananchi zimetokana na serikali kuchukua baadhi ya maeneo yaliyokuwa makazi ya wananchi kwa madai kuwa maeneo hayo   yalikuwa katika hifadhi za misitu. Aidha Mona ametaja baadhi ya maeneo yenye migogoro kuwa ni pamoja na vijiji vya Litapunga,Luhafwe,Sitalike,Ugalla, Kanoge na Mpanda Ndogo. Hivi karibuni Chama cha ACT-Wazalendo wakiwa wameambatana na viongozi wa kijiji cha Sitalike pamoja na wananchi wa kijiji cha Sitalike walifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Mu

MGANGA MKUU JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA

MHAKAMA ya  Wilaya ya  Mpanda  Mkoani  Katavi   imemuhukumu mganga mkuu wa  Zahanati ya  Kasekese  Wilaya ya  Tanganyika  Martin  Mwashamba  (27)kifungo cha  miaka  30 jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la mbaka na kumpa  mimba  wanafunzi wa  dasasa la  sita  wa  shule ya  Msingi  Kasekese mwenye  umri wa miaka 15  jina  lake limehifadhiwa. Hukumu  hiyo ilitolewa  jana   na   Hakimu  mkazi wa  Mahakama ya  Wilaya hiyo  Odira  Amwol   baada ya  Mahakama  kuridhika  na  ushahidi  uliotolewa  Mahakamani  hapo  na   upande wa  mashitaka. Awali katika  kesi  hiyo  mwendesha  mashtaka   Mwanasheria wa   Serikali Mkoani Katavi  Gregoli  Mhagwa  alidai   Mahakamani  hapo  kuwa   mshitakiwa  alitenda  kosa  hilo  Julai  2  mwaka  jana   Kijijini  hapo. Alieleza  Mahakamani  hapo siku  hiyo ya  tukio  mshitakiwa  alimbaka   mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa    darasa la  sita wa shule   ya   Msingi  Kasekese mwenye  umri wa  miaka   15 huku  akijua  kufanya  hivyo ni  kosa. Upande

TRA KATAVI KUHAKIKI TIN NAMBA

Image
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoani katavi,imeanza kuhakiki namba za utambuzi(TIN NAMBA) kwa wafanya biashara waliosajiliwa katika biashara zao. Meneja wa TRA mkoani Katavi Enos Mgimba amesema zoezi la uhakiki hili ambalo limeanzia leo Aprili 18,2018 katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda baadaye litaendshwa katika maeneo mengine ya Mkoa. Mgimba ametaja baadhi ya faida ya utambuzi wa TIN   NAMBA kwa TRA kuwa ni pamoja na mamlaka kuwa na taarifa sahihi za wafanyabiashara ili hali kukusanya mapato na kusaidia katika utatuzi wa changamoto mbalimbali za kibiashara. Baadhi ya wafanyabiashara ambao wamefika katika zoezi hilo wamesema zoezi hilo lina faida kwao ikiwemo kutambulika katika biashara anayoifanya. Halmashauri 5 za Mkoa wa Katavi zinazotakiwa kufanyiwa uhakiki ni Manispaa ya Mpanda na Nsimbo zinazopatikana Wilayani Mpanda,Mlele na Mpimbwe zinazopatikana Wilayani Mlele na ,Mpanda inayopatikana Wilayani Tanganyika. Kwa mjibu wa Meneja Enos Mgimba,Jumla ya wafanyabia

WASITISHA SAFARI ZA KUSAFIRISHA ABIRIA KATAVI KWENDA MIKOANI

Miongoni wa wafanyabiashara wa usafirishaji abiria mjini Mpanda wamesitisha huduma kutokana na ubovu wa miundombinu. Hayo yamebainishwa na baadhi ya wahudumu wa kampuni za usafirishaji wanaomiliki mabasi ya mikoani ambazo zinatumia barabara inayoanzia Mpanda kuelekea Tabora tabora. Magari yaliyokuwa yakitumia barabara ya Mpanda-Tabora yamepewa utaratibu wa kutumia barabara ya Mpanda-Kigoma au Mpanda-Mbeya ambapo wafanyabiashara wengine wamesema wanalazimika kuongeza nauli kwa shilingi elfu kumi hadi elfu kumi na tano kwa kila safari kwa kuwa umbali wa safari umeongezeka Hata hivyo kwa mjibu wa wasafirishaji hao wamesema barabara mbadala ya kupitia Uvinza Mkoani Kigoma nayo haipo katika hali nzuri kitendo kinachosababisha ugumu wa safari. Jumamosi ya Aprili 16,2018,mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Rafael Muhuga alitangaza kufungwa kwa barabara ya Mpanda-Tabora baada ya barabara hiyo kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Mwishoni mwa wiki iliyopia mku

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MPYA WA VIONGOZI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Magufuli leo Aprili 15,2018 amefanya uteuzi wa Majaji 10 wa Mahakama Kuu ya Tanzania,Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali,Naibu Mkurugenzi wa Mashitaka,Wakili Mkuu wa serikali na Naibu Wakili Mkuu wa serikali. Aidha,Dkt.Magufuli amesema amefanya uteuzi huo wa Majaji wa Mahakama Kuu kwa lengo la kujaza nafasi za Majaji waliostafu na amefanya uteuzi wa Wakili Mkuu wa serikali na Naibu wake kwa lengo la kuhakikisha ofisi za Mwanasheria Mkuu wa serikali,Mkurugenzi wa Mashitaka na Wakili wa Mkuu wa serikali zinafanya kazi vizuri zaidi katika kushughulikia masuala ya Mahakama. Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com    

DOKTA TITUS KAMAN ADAIWA KUMTELEZA MWANAMKE KATAVI BAADA YA KUMZALISHA MTOTO MWENYE ULEMAVU

Mwanamke mmoja ambaye amejitambulisha kwa jina la Bi.Amina Salumu mkazi wa wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi amedai Dkt.Titus Kamani ambaye amewahi kuwa kiongozi mkubwa hapa nchini amemtelekeza mwanamke huyo baada ya kuona amejifungua mtoto mwenye ulemavu. Bi.Amina Salumu ametoa malalamiko hayo leo Aprili 14,2018 katika uwanja wa Azimio Mjini Mpanda kupitia mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi. Kwa mjibu wa Mwanamke huyo,Titus Kamani mbunge aliyeko Dodoma kwa sasa amewahi kuwa Dkt.Mkuu katika Hospitali ya Reft Valley pia mbunge Mkoani Mwanza ambapo. Mbali na mwanamke huyo wanawake wengine wamedaiwa kutelekezwa,kutishwa maisha na waume waliowazalisha huku wengine wakinyimwa matumizi muhimu ya kifamilia. Wananchi wengi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi wamejitokeza katika uwanja wa Azimio ili kueleza kero zao kwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi meja jeneral Mstaafu Raph

BARABARA YA MPANDA—TABOARA YAFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga ametangaza barabara ya Mpanda– Tabora kufungwa kwa muda usiojulikana kuanzia leo Jumamosi Aprili 14,2018. Katika picha ni gari lililosombwa na maji 2016 na kuuwa watu Mkuu wa Mkoa ametoa kauli hiyo leo katika mkutano wa hadhara ambao ameuitisha kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi kupitia mkutano amabo umeitishwa katika uwanja wa Azimio mjini Mpanda. Muhuga amesema barabara hiyo imefungwa baada ya maji kujaa barabarani kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha na hivyo kuhatarisha maisha ya wasafiri. Kwa upande wake mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra Mkoani Katavi Amani Mwakalebela amesem kutokana na barabara kuharibika kwa kiasi kikubwa,wenye mabasi watalazimika kusafirisha abiria kupitia mkoani Kioma au Mbeya. Mwaka 2016 barabara ya Mpanda – Tabora ilifungwa baada ya kukatika kwa daraja la mto Koga ambapo takribani watu 10 walipoteza maisha baada ya gari walilokuwa wakisafiria

TMA WATOA TAHADHARI YA MVUA KUBWA LEO APRILI 13,2018

Image
Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania TMA imesema vipindi vifupi vya mvua kubwa vinatarajiwa leo Aprili 13,2018. Katika taarifa ya mamlaka hiyo ambayo imetolewa jana Aprili 12,2018 mikoa ambayo inatarajiwa kuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa ni Kagera,Geita, Mwanza,Mara, Shinyanga,Simiyu,Kigoma,Tabora,Katavi,Morogoro, Ruvuma,Dar Es Salaam, Pwani, Tanga Pamoja Na Visiwa Vya Unguja Na Pemba. Aidha TMA imetoa angalizo kwa kusema kuwa Vipindi Vifupi Vya Mvua Kubwa Vinatarajiwa Katika Baadhi Ya Maeneo Ya Mikoa Ya Rukwa, Njombe, Mbeya, Iringa Na Songwe. Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com

RC KATAVI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI KESHO JUMAMOSI APRILI 14,2018

Image
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga kesho siku ya Jumamosi Aprili 14,2018 ameitenga kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi. Kwa mjibu wa kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi,Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na maeneo mengine ya Mkoa wa Katavi kufika katika viwanja vya Azimio Mjini Mpanda kuanzia majira ya saa 4:00 asubuhi ili kueleza kero zao. Muhuga amesema atasikiliza kero za wananchi wote zinazohusu masuala mbalimbali na kuzipatia majibu papo hapo. Hii ni mara ya Kwanza kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga,kusikiliza kero za wananchi katika eneo la wazi linalojumuisha wananchi wote tangu alipoteuliwa mwaka 2016 kuwa Mkuu wa Mkoa kabla ya hapo amekuwa akisikiliza kero za wananchi Ofisini kwake. Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com

RAIS MAGUFULI LEO APRILI 13,2018 KUWAVALISHA VYEO MAOFISA WA JWTZ AKIWEMO MKUU WA WILAYA YA BUHIGWE ANAYEREJESHWA JESHINI

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli leo Aprili 13,2018 anatarajia kuwavalishwa vyeo maofisa mbalimbali wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)   ambao amewapandisha vyeo jana Aprili 12,2018. Kati ya maofisa hao yumo Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Kanali M E Gaguti ambaye sasa anapanda cheo na kuwa Brigedia Jenelari na kurejeshwa Jeshini. Kwa mjibu wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania , Jenelari Venancy Mabeyo amesema maofisa walioteuliwa wanakwenda kuimarisha safu za utendaji kazi kijeshi. ORODHA YA WALIOPANDISHWA VYEO 1.Meja Jenerali Peter Massao aliyepandishwa kuwa Luteni Jenarali. 2.Brigedia Jenerali Henry Kamunde aliyepandishwa na kuwa meja jenerali. 3.D.D.M Mullugu 4.J.J Mwaseba 5.A.S Mwamy 6.R.K Kapinda 7.C.D Katenga 8.Z.S Kiwenge 9.M.A Mgambo 10.A.M Alphonce 11.A.P Mutta 12.A.V Chakila 13.M.G Mhagama 14.V.M Kisiri 15.C.E Msolla 16.S.M Mzee 17. C.J Ndiege 18.I.M Mhona 19.R.C Ng’umbi 20.S.J Mnkande 21

ZITTO ATAKA TAMISEMI IMTAFUTE MWENYEKITI WA HALAMSHAURI ALIYETOWEKA

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT -Wazalendo),Zitto Kabwe amemtaka waziri wa Tamisemi kulitafutia ufumbuzi suala la kutoweka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kakonko, Simon Kangue. Amesema hayo bungeni jana Aprili 12,2018 alipochangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais,yenye wizara za Tamisemi,Utumishi na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2018/2019. “Habari zinazosambaa Kibondo tayari ameuawa. Tunataka maelezo ya mtu huyo,sisi watu wa Kigoma ni Kigoma kwanza kabla ya kuwa Watanzania naomba hilo mlielewe,” amesema. Zitto amesema mara ya mwisho kuonekana mwenyekiti huyo aliitwa kwa mkurugenzi na kukutana na ofisa usalama wa wilaya. Amesema tangu siku hiyo hajulikani alipo mwenyekiti huyo licha ya jitihada za kumtafuta kufanyika. “Familia imechukua hatua mbalimbali,imelalamika na sisi wajumbe wenzake tumehoji kwenye vikao,hakuna maelezo yoyote kutoka serikalini,”alisema Zitto.

RAIS AWAPANDISHA VYEO MAAFISA WA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ)

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli leo Aprili 12,2018 amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) katika vyeo mbalimbali. Taarifa iliyosomwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Salvatory Mabeyo,Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Mhe.Rais Magufuli amempandisha cheo Meja Jenarali Peter Paul Massao kuwa Luteni Jenerali.

WANANCHI KATAVI WATAKA VIONGOZI WA SERIKALI WAMUENZI SOKOINE KWA KUPELEKA HUDUMA MUHIMU ZA JAMII KWA WANANCHI

Wananchi Mkoani Katavi wamewashauri viongozi wa serikali wa serikali ya awamu ya tano kuenzi kifo cha Wazairi Mkuu hayati Edward Moringe Sokoine kwa kupeleka huduma muhimu za kijamii kwa wananchi ikiwemo maji. Wakizungumza na P5TANZANIA kwa nyakati tofauti kuhusu kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo cha waziri mkuu hayati Edward Moringe Sokoine aliyefariki Apriki 12,1984 wamesema kuna maeneo mengi mkoani Katavi ambayo bado yanakosa huduma muhimu kama maji huku hata sehemu zenye zikipata kwa mgao. IAidha wametaka hata miradi ya maji iliyoanzishwa enzi za ukoloni ifufuliwe huku wakisema bado kuna hali ngumu ya kimaisha ambayo serikali inatakiwa iyatatue kama sehemu ya kumuenzi Sokoine. Aidha wamesema ni kiongozi aliyechukia uhujumu uchumi,rushwa,ufisadi huku akishiriki vema kuandaa majeshi wakatio wa vita vya Kagera baina ya Tanzania na Uganda mwaka 1978. Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine aliwahi kuwa Waziri Mkuu mara mbili Februaei 13 mwaka 1977 hadi Novemba 7 mwaka 1980 na   Febr

RAIS MAGUFULI ATAKA WATANZANIA WAMUEZI SOKOINE KWA KUIGA MEMA ALIYOYAFANYA

Image
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli ametoa rai kwa watanzania kumuenzi Waziri Mkuu wa Zamani hayati Edward Moringe Sokoine kwa kujenga umoja,kupiga vita rushwa na kuchapa kazi. Rais ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa twitter ikiwa leo ni Kumbukumbu ya Kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Edward Moringe Sokoine aliyefariki dunia Aprili 12,1984 kwa ajali ya gari. Ajali hiyo ilitokea eneo la Dakawa nje Kidogo ya Mji wa Morogoro wakati akitokea Bumgeni Dodoma Kuelekea Jijini Dar es salaam. Amesema watanzania wanapoazimisha siku hii ya kifo chake, watanzania waige mfano wake kwani alikuwa msema kweli, asiyeogopa,mpiga vita rushwa,ufisadi,unyonyaji,mzalendo wa kweli na aliyechukia rasilimali za watanzania kuibwa. Rais amesema kwa upande wake anamkumbuka kiongozi huyo enzi za uhai wake na mchango wake katika Taifa la Tanzania na anasema alipata taarifa za kifo cha Sokoine   tarehe 12 Aprili 1984 akiwa Mpwapwa JKT nikitumikia jes

SPIKA AAGIZA MWANDISHI NA WAHARIRI WA GAZETI LA RAIA MWEMA WAHOJIWE KWA KULIDHALILISHA BUNGE

Image
Kamati ya Maadili,Haki na Madaraka ya Bunge,inatarajia kuwahoji mwanahabari Paschal Mayallah na wahariri wa gazeti la kila wiki la Raia Mwema kwa madai ya kuchapisha habari inayodhalilisha bunge,Aprili 9 wiki hii. Hayo yameelezwa leo Aprili 12 bungeni na Spika wa Bunge,Job Ndugai aliyesema kuwa habari iliyochapishwa Aprili 9 ilidhamiria kuchafua hadhi ya bunge. Hayo yamekuja baada ya mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga kuomba mwongozo wa Spika juzi Aprili 9, akihoji iwapo habari iliyoandikwa na gazeti hilo yenye kichwa cha habari “Bunge linajipendekeza?”haidhalilishi bunge. Spika Ndugai leo Aprili 12,ameliambia bunge kuwa mwandishi huyo na wahariri watatakiwa kuhojiwa na kamati hiyo ya bunge. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

LEO NI KUMBUKUMBU YA MIAKA 34 YA KIFO EDWARD SOKOINE HISTORIA YAKE IKO HAPA

Image
Edward Moringe Sokoine  ( 1938  -  12 Aprili   1984 ) alikuwa  mwanasiasa  kutoka nchi ya  Tanzania . Aliwahi kuwa  Waziri Mkuu  mara mbili,tangu tarehe  13 Februari   1977  hadi  7 Novemba   1980 ,tena tangu tarehe  24 Februari   1983  hadi  kifo  chake,alipofariki kufuatana na  ajali  ya gari. Uongozi wake ulionekana kuwa wa mfano kwa jinsi alivyokuwa na  uadilifu  na kufuatilia utendaji kazi huku akikemea ulaji  rushwa  na  ubadhirifu  wa  mali za umma . Upande wa  dini ,alikuwa  Mkristo  wa  Kanisa Katoliki ,tena mwanachama wa  Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko . Sokoine alifariki kwa ajali ya gari wakati akitoka kwenye kikao cha  bunge   Dodoma  kuelekea  Dar es Salaam . Wengi wanashuku ajali hiyo kuwa ilipangwa. Kifo chake kilileta majonzi makubwa kwa Watanzania wa kawaida ambao walikuwa wanamtarajia kuwatetea wanyonge na kuinua hali ya maisha yao. Mwili  wa Edward Moringe Sokoine ulizikwa nyumbani kwao  Monduli ,mkoani  Arusha . Chuo cha Kilimo na Mifugo Morogoro  k