Posts

Showing posts from January 8, 2018

RAIS AMUAPISHA NAIBU WAZIRI WA MADINI,AMTENGUA KAMISHNA WA MADINI NA KUTEUA MWINGINE

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt. John Pombe Magufuli leo amemuapisha Mhe.Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini na kuiagiza Wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria kuhakikisha kanuni za sheria mpya ya madini namba 7 ya mwaka 2017 inasainiwa ifikapo Ijumaa tarehe 12 Januari 2018. Mh.Rais Magufuli ametoa agizo hilo muda mfupi baada ya Mhe.Biteko kuapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam na ameelezea kutoridhishwa kwake na namna viongozi na watendaji wa Wizara ya Madini wanavyotekeleza majukumu yao polepole na bila kujali maslahi ya nchi. Amemuagiza Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi kushirikiana na Naibu Mawaziri, Katibu Mkuu na Wakurugenzi wanaohusika katika Wizara ya Madini kuhakikisha kanuni hizo zinasainiwa. Pamoja na maagizo hayo Mh.Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Kamishna wa Madini Mhandisi Benjamin Mchwampaka na amemteua Prof. Shukrani Elisha Manya kuwa Kamishna wa Madini na pia kukaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Kam

RAIS MAGUFULI AIPA SIKU 5 WIZARA YA KILIMO,WAZIRI MTEGONI

Image
Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Kilimo kuhakikisha mbolea inafikishwa katika mikoa yote ya uzalishaji wa chakula ukiwemo Mkoa wa Rukwa ifikapo Ijumaa Januari 12, 2018. Magufuli ameyasema hayo leo wakati akimwapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini Ikulu jijini Dar es Salaam.  Amemuelekeza Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa kufuatilia jambo hilo na amebainisha kuwa endapo mbolea haitafikishwa katika maeneo hayo ifikapo Ijumaa wahusika waachie ngazi. Rais Magufuli amewataka watendaji wote wa Serikali kutekeleza majukumu yao ipasavyo na ameonya kuwa hatosita kumfukuza kazi mtendaji yeyote atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa maslahi ya Watanzania. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MATOKEO YA DARASA LA NNE NA KIDATO CHA PILI YATANGAZWA

Image
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa darasa nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 22 na 23 mwaka jana huku idadi kubwa ya wanafunzi wakifanya vyema katika mitihani hiyo. Akitangaza matokeo hayo leo,Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk.Charles Msonde amesema jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne wamefaulu  kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo. Amesema  wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D wakati wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha. Kuhusu matokea ya upimaji wa kidato cha pili,Dk Msonde  amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa  kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea  na kidato cha tatu. Dk Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili  51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.

WAFANYABIASHARA WILAYANI MPANDA WAGOMA KUFUNGUA MADUKA,DC ATOA KAULI

Image
Na.Issack Gerald Mkuu wa wilaya ya mpanda Liliani Charles Matinga ameamuru masoko yote kufunguliwa  baada ya wafanyabiashara kufanya  mgomo kutokana na ongezeko la tozo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kodi. Amri hiyo ameitoa leo asubuhi wakati akiwa soko kuu  ambapo wafanyabiashara waliogoma  kufungua biashara zao huku akisema kwa anayeshindwa arudishe  chumba cha biashara. Amesema wamekaa na wafanyabiashara kwa ajili ya kupanga ongezeko hilo ambapo hapo awali halimashauri ilipanga laki moja na baada ya hapo  ikapungua hadi elfu sitini. Awali wafanya biashara hao wamesema walishindwa kumudu kodi iliyokuwepo ya shilingi 15000 ambapo wamesema serikali kuwatoza shilingi 60000 ni kuendelea kuwakandamiza. Masoko amabyo wafanyabiashara wamefunga biashara zao ni Soko kuu la Wilaya ya Mpanda na Soko la Buzogwe lenye zaidi ya wafanyabiashara zaidi ya 500 hii ikiwa ni kwa mjibu wa baadhi ya wafanyabiashara. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

KIDATO CHA KWANZA WARIPOTI KWA KASI KATIKA SHULE MBALIMBALI MKOANI KATAVI

Image
Na.Issack Gerald Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha kwanza ambao wameripoti katika shule mbalimbali za sekondari Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wamesema wamejiandaa kusoma kwa bidi ili kuwa na ufaulu mzuri kitaaluma. Miongoni mwa Wanafunzi katika Shule ya Sekondari Mwangaza wamesema wamejiwekea mikakati yao kuhakikisha wanafaulu kwa kiwango kinachotakiwa kitaaluma ambapo wanafunzi hao wanatoka katika shule mbalimbali za msingi zikiwemo Kawanzige,Kakese,Mwangaza,uhuru, Kashato,Kashaulili na Katavi. Kwa upande wake mkuu wa Shule ya Sekondari Mwangaza iliyopo Manispaa ya Mpanda Simon Lubange amesema,mpaka sasa wanafunzi karibu ya 200 kati ya 260 wanaotakiwa kuripoti katika shule hiyo wameripoti ili kuanza masomo. Nao baadhi ya wazazi ambao wamewapeleka shule watoto wao wamesema ni wakati wa kila mzazi kutambua umuhimu wa elimu kwa kila mtoto kwa maisha ya baadaye. Hata hivyo kwa mjibu wa takwimu iliyotolewa mwaka uliopita na Afisa elimu Mkoani Katavi Ernesti Hinju inaonesha z

SERIKALI MKOANI MTWARA KUTOWACHUKULIA WANAFUNZI WAJAWAZITO

Image
Serikali imesema haitawafungulia mashtaka wasichana watano wa shule waliopata ujauzito ambao walikamatwa mwishoni mwa juma lililopita baada ya mkuu wa wilaya kuagiza kukamatwa kwao. Hatua hiyo iliibua mjadala mkali huku wanaharakati wa kijamii wakipinga hatua hiyo ya serikali wakisema kuwa agizo hilo inakandamiza haki za watoto hao. Wanaharakati wanaohusika na utetezi wa haki za watoto na wamesema uamuzi wa kuwakamata wazazi hauwezi kuwa njia pekee ya kutokomeza mimba za utotoni bali serikali inapaswa pia kuangazia visababishi vingine vinavyochangia ongezeko la mimba za utotoni. Afisa katika shirika la kupigania haki za wanawake Tanzania TAMWA Edison Sosten amesema Kuna vikwazo vingi ambavyo mabinti wanakutana navyo katika mazingira ya nyumbani pia wakati akitoka shuleni. Katika suala hilo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byankwa maamuzi hayo yanalenga sio kuwaadhibu wazazi bali kujenga ushirikiano nao kwa sababu wengi wamekuwa wakificha majina ya watu waliowapatia mimba watot
TEHERAN Afisa wa ngazi ya juu katika sekta ya elimu nchini Iran ametaka lugha ya Kiingereza isiendelee kufundishwa katika shule za msingi nchini humo. Katika mahojiano na kituo cha televisheni ya taifa ya Iran jana Jumapili, afisa huyo, Mehdi Navid-Adham ambaye ni kiongozi wa Baraza la Elimu ya Juu amesema Kiingereza ni mkondo wa uvamizi wa kitamaduni wa nchi za Magharibi. Mwaka 2016 Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alitoa mapendekezo kama hayo, baada ya kuarifiwa kuwa baadhi ya shule za chekechea zilikuwa zikiwafundisha watoto kwa lugha ya Kiingereza. Tangazo hilo limekuja wiki moja baada ya maandamano dhidi ya serikali kulalamikia hali ngumu ya uchumi, maandamano ambayo Khamenei alisema yaliratibiwa kutoka nje ya nchi.