Posts

Showing posts from October 28, 2017

DAKTARI MTANZANIA AFUTWA KAZI NA MADIWANI

Image
Daktari mmoja wilayani Kisarawe amefutwa kazi baada ya kukutwa na makosa mbalimbali yanayotia hofu juu ya utendaji kazi katika majukumu yake ya kila siku. Uamzi huo wa kumfuta kazi Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mtakayo Emmanuel Shumbusho,umefikiwa na  Baraza la Madiwani halmashauri ya Kisarawe mkoani Pwani. Dkt Emmanuel Shumbusho anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo uzembe,utoro kazini ambapo hajaonekana kazini kwa takaribani siku tisa bila taarifa yoyote kwa mwajiri wake. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamis Dikupatile akitoa maamuzi amesema,wamefikia hatua hiyo baada ya kubaini mapungufu mengi kutoka kwa mtumishi huyo. Madiwani wote kwa pamoja walikubaliana na uamzi huo kutokana na uzembe wa daktari huyo katika suala zima la utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi na kusababisha kuibuka kwa usumbufu mkubwa kutokana na kutopatiwa matibabu kwa wakati.

MADIWANI MANISPAA YA MPANDA WAMETOA TAMKO LA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA UONGOZI WAKE

Na.Issack Gerald-Katavi Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa Mpanda mkoani  Katavi  wamempongeza rais John Magufuli kwa ujasiri aliouonesha wa kulinda  rasilimali za nchi  hasa  katika suala la madini. Pongezi hizo zilitolewa jana kupitia waandishi wa habari ambapo Meya wa Manispaa ya Mpanda Willium Mbogo alizungumza niaba ya madiwani hao. Aidha Mbogo alisema wanawalaani vikali baadhi ya watu ambao wanaobeza jitihada zinazofanywa  na rais  za kulinda rasilimali zetu za  nchi na hasa madini  kwa  ajili ya  manufaa ya Watanzania  wote. Alisema madiwani wa  Manispaa ya Mpanda wanaamini mapato hayo yatakayopatikana  yataongezeka  Serikalini na halmashauri zote zitaongeza uwezo wa kuwahudumia wananchi. Kwa upande wake diwani wa Kata ya makanyagio Haidari  Sumry aliomba jitihada za rais zisiishie kwenye madini tu bali nguvu iongezeke kwenye   maeneo   mengine   iliuchumi wa  nchi ukue na kuongezeka zaidi ya hivi sasa.  Alisema endapo rasilimali za nchi zitasimamiwa vizuri halmas

WAKULIMA WAMESHAURIWA KUWEKA KIPAUMBELE KILIMO CHA MAZAO YA CHAKULA

Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi Wakulima wametakiwa kuyapa kipaumbele mazao ya chakula katika msimu wa huu wa kilimo ili kuwa na uhakika wa chakula Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Bi Lilian. Matinga wakati akihutubia mkutano wa ufunguzi wa msimu wa kilimo ulifanyika leo katika viwanja vya shule ya msingi kakese Bi matinga amesema kuwa ili kuweza kupiga vita njaa wananchi wote hawana budi kulima kwa nguvu zao zote ili kuhakikishia akiba ya kutosha ya chakula mwisho wa msimu Katika hatua nyingine Bi Matinga amewataka maafisa ugani kuwa na mashamba darasa ili yawasidie wakulima kulima kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo cha kisasa Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wameishukuru hatua ya manispaakuzindua mradi huo katika kijiji chao na kuwasogezea huduma za pembejeo za kilimo katika maeneo yao.

WAKAZI KITONGOJI CHA SITUBWIKE WADAIWA KUKAIDI KUONDOKA HIFADHINI

Na.Issack Gerald-Katavi Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga,amewataka wananchi wa Kitongoji cha Situbwike waliovamia Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kuanzisha shughuli za kibinadamu kinyume cha sheria waondoke kwa hiari ndani ya wiki mbili zijazo kabla ya kuondolewa kwa nguvu.