Posts

Showing posts from December 4, 2017

MTOTO MCHANGA WILAYANI MPANDA MKOANI KATAVI AOKOTWA NA WATOTO AKIWA AMETELEKEZWA NA MAMA YAKE

Na.Issack Gerald Mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na umri kati ya mwezi mmoja mpaka mitatu Wilayani Mpanda Mkoani Katavi ameokotwa akiwa ametelekezwa na mama yake mzazi ambaye hata hivyo hajatambulika. Kuokotwa kwa mtoto huyo wa jinsi ya kike kumethibitishwa na Afisa ustawi wa jamii Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Bi.Redigunga Mayorwa ambaye amesema mtoto huyo ameokotwa na w atoto waliokuwa wakicheza katika mtaa wa Airtel kata ya uwanja wa Ndege. Bi.Mayorwa amesema watoto waliomuokota akiwa amefunikwa majani ambapo walimpeleka kwa wazazi wao na hatimaye wazazi hao kumpeleka mtoto katika kituo cha polisi Wilayani Mpanda . Kwa mjibu wa Bi.Mayorwa mpaka sasa mtoto aliyeokotwa Desemba 1 mwaka huu akiwa hana majeraha wala tatizo lolote la kiafya,yupo katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda kwa uangalizi maalumu na anaendelea na afya njema. Ametoa wito kwa mama wa mtoto huyo kufika hosptali ya Manispaa ya Mpanda kumchukua ili ampatie malezi yanayostahili. Tukio hilo linatokea ik

KAULI YA SERIKALI MANISPAA YA MPANDA IMEWASIKITISHA WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI

Image
Na.Issack Gerald Watu wenye ulemavu Mkoani Katavi,wameeleza kusikitishwa na kauli ya serikali kuwa haina pesa za kuwawezesha kufanya maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani. Masikitiko hayo wameyatoa leo katika kikao cha kupanga tarehe nyingine ya maadhimisho ambapo wamepanga yafanyike Desemba 19 mwaka huu. Kwa upande wake Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu SHIVYAWATA Mkoani Katavi Issack Mlela amesema serikali kutowawezesha kufanya maadhimisho ni kutowatendea haki wakati serikali inasema mapato yameongezeka serikalini. Juzi Afisa maendeleo ya jamii Bi.Marietha Mlozi na Afisa Ustawi wa jamii Bi.Agness Bulaganya wote wa Manispaa ya Mpanda walikuwa wameiambia Mpanda Radio kuwa maadhimisho ya siku ya Watu wenye ulemavu yangefanyika Desemba 3 ambayo hata hivyo yameahirishwa baada ya ukosefu wa pesa. Haki za watu wenye ulemavu zinasimamiwa na sheria mbalimbli ikiwemo sheria namba 9 ya mwaka 2010 inayitaka serikali na jamii kuhakikisha watu wenye u

WAENDESHA VYOMBO VYA MOTO WAMETAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA BARABARANI KUELEKEA MWISHONI MWA MWAKA.

Image
Na.Issack Gerald Katika kuelekea siku kuu za mwishoni  mwa mwaka Waendesha vyombo vya moto Mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia sheria za usalama bararani. Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoani Katavi Bw.Nassoro Alfi ambapo amesema madereva wanatakiwa kuwa makini ikiwa pamoja na kufuata alama za barabarani. Aidha mwenyekiti huyo ameuomba uongozi wa manispaa ya Mpanda kuweka vibao vya alama za usalama barabarani katika manispaa ili kupunguza ajali barabarani. Katika hatua nyingine Bw. Alfi amesema Maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani mwaka 2017  kimkoa wa katavi yanatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 17 hadi 20 mwezi. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

CWT MKOANI KATAVI WAMEANZA KUCHARUKA KUHUSU MADAI YA WALIMU

Image
Na.Issack Gerald Chama cha Walimu mkoa wa katavi CWT kinakusudia kuchukua hatua zaidi kutokana na fedha za walimu  manispaa ya Mpanda za makato katika mfuko wa Jamii PSPF kwa  2008 kutofikishwa. Hatua hiyo imebainishwa na Katibu wa chama cha walimu mkoani Katavi Hamisi Chinahova ambapo amesema suala hilo halijapatiwa ufumbuzi mpaka sasa. Katika hatua nyingine amelitaja suala la kukithiri kwa madai mbali mbali ya walimu kuwa kikwazo katika utendaji kazi ikiwemo kufikia Malengo ya kitaifa. Mwaka 2015 yaliibuka madai haya na kupelekea baadhi ya walimu kufanya maandamano ya amani mpaka ofisi ya mkuu wa mkoa ili kushinikiza malipo ya madeni zikiwemo stahiki mbali mbali. Mwezi uliopita Rais Magufuli alisema madai yote ya watumishi wa umma yangelipwa mwezi uliopita.   Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MWENDESHA BODABODA AMEMUUA BODABODA MWENZAKE,ASAKWA NA POLISI PANDE ZOTE

Image
Mwendesha bodaboda maarufu mpaka wa Sirari na Isebania, Kenya,Kiongera Nchagwa (27) mkazi wa Kijiji cha Gwitiryo, Tarime Mara anasakwa na Polisi wa pande zote mbili, akituhumiwa kumuua mwenzake,Jeremia Omera (22) kwa kumchoma kwa kisu kifuani. Mwenyekiti wa Haki za Binadamu Wilaya ya Kurya West ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Isebania, Peter Masaithe amesma tukio hilo limetokana na ugomvi wa kunyang’anyana mizigo ya abiria aliyetaka kuvuka mpaka kuingia nchini Tanzania akitokea Nairobi Kenya. Masaithe amekemea bodaboda kutembea na visu,kunywa pombe za viroba ambavyo baada ya kupigwa marufuku sasa vimehamia Isebania hali inayochangia uhalifu na kuziomba serikali za nchi hizo mbili kuchukua hatua kali ukiwemo msako wa viroba na bangi ili kuokoa vijana. Polisi wa Isebania wamethibitisha kifo cha Jeremia na wamewasiliana na wenzao wa Sirari kumsaka mtuhumiwa kujibu tuhuma ambapo pia Polisi wa Sirari wamekiri kupokea taarifa ya mauaji. Mwenyekiti wa Kijiji cha Sokon

CHADEMA:TAARIFA ZA MNYIKA KUJIVUA UANACHAMA SIYO ZA KWELI ZIPUUZWE

Image
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,kimekanusha Mbunge wa Jimbo la Kibamba na mwanachama wa Chadema John Mnyika kuwa amejivua uanachama. Mbunge John Mnyika. Hatua hii imekuja baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mbunge huyo amejivua uanachama kwenye chama chake cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Chama hicho ambacho kimekanusha taarifa kupitia ukurasa wake wa Twitter kimesema habari hizo hazina ukweli wowote za zinapaswa kupuuzwa. Aidha chama hicho kimesema wanaosambaza habari za Mnyika kujivua uanachama ni walioishiwa hoja na majibu juu ya maisha ya watanzania. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MAKAMU WA RAIS ATAKA WATU WENYE ULEMAVU KUTOACHWA NYUMA KATIKA MAENDELEO

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan ameitaka jamii kutowaacha nyuma watu wenye ulemavu katika nyanja zote za maendeleo. Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo katika mkusanyiko wa wananchi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Watu wenye ulemavu duniani ambayo yamefanyika shule ya Uzini mkoani Kusini Unguja. Wakati huo huo amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwashughulikia kikamilifu waharifu na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria ikiwemo mahakamani na kutoa adhabu kali dhidi ya wale watakaobainika wakiwanyanyasa watu wenye ulemavu. Maadhimisho ambayo ambayo huifanyika Desemba 3 ya kila mwaka,yamefanyika kitaifa mkoani Simiyu na kushindikana kufanyika kimkoa mkoani Katavi yanabeba kaulimbiyu inayosema ’Badilika tunapoelekea jamii Jumuishi na imara kwa watu wote’’.

RC RUKWA : VIONGOZI WA DINI MUOMBEENI RAIS MAUGUFULI NA WATENDAJI WAKE

Na.Issack Gerald MKUU wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaomba viongozi wa dini mkoani humo kuendelea kumuombea rais John Magufuli pamoja na watendaji wengine  wa serikali ili waongoze wananchi kwa kuzingatia misingi ya haki usawa na kuwaletea maendeleo  endelevu. Wanagabo ametoa ombi hilo maalumu huo wakati akichangia shilingi milioni moja kwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa lengo la kusaidia ujenzi wa kituo cha afya cha Waislamu kinachoendelea kujengwa katika Tarafa ya Kirando Kata ya Kirando Wilayani Nkasi mkoani humo. Amesema rais na watendaji wa serikali ya awamu ya tano wanahitaji kuombewa daima kwani kufanya kazi ya kuwaongoza wananchi ni jukumu zito linalohitaji msaada wa Mwenyezi Mungu. Waka huo huo amesema taasisi za kidini kwa muda mrefu zimekuwa zikisaidia juhudi za serikali katika kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi jambo ambalo pia linasaidia utekelezaji wa Ilani ya chama tawala inayoongoza serikali. Ametoa mchango huo kwa lengo la k

MWENYEKITI WA KIJIJI MKOANI KATAVI AKATAA KUJIUZULU

Na.Issack Gerald Mwenyekiti wa Kijiji cha Stalike Bwana Christopher Mrisho amesema hayuko tayari kuachia ngazi kwa tuhuma za kuwachangangisha pesa wananchi kinyume na sheria Bw.Mrisho haoni umuhimu wa kufanya hivyo kwani ni wananchi wenyewe ndio waliomba kuchangisha pesa hizo. Imedaiwa kuwa Bw.Mrisho  amewachangisha wananchi hao kwa awamu mbili tofauti zaidi ya shilingi milioni moja kwa madai kuwa anaenda kuonana na waziri mkuu wa Tanzania ili kuwasaidia kutatua mgogoro kati ya wananchi hao na mamlaka ya hifadhi za misitu Tanzania. Mwenyekiti huyo anadaiwa kuwachangisa baadhi ya wananchi wa kijiji hicho ambao waliondolewa na serikali katika makazi hayo ikidaiwa kuwa walivamia hifadhi ya msitu Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WATOTO WALIOKUWA WAMEPOTELEA MSITUNI MKOANI KATAVI WAMEPATIKANA WAKIWA HAI.

Na.Issack Gerald Baadhi ya wakazi wa Kata ya Katumba Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,wamekipongeza kituo cha Mpanda Radio kwa kusaidia juhudi za kupatikana kwa watoto wawili waliokuwa wamepotea katika mazingira ya kutatanisha. Wakazi hao wakiwemo Bw.Alex Gezaho,wamesema siku chache baada ya Mpanda Radio Kutangaza upotevu wa watoto hao wanaojulikana kwa majina ya Rama na Vitisho walipatikana porini wakiwa na afya njema. Kwa mjibu wa taarifa zilizokuwa zimetolewa na viongozi wa Kijiji cha Mnyaki,watoto hao walikuwa wamepotea wakati wakiwinda ndege porini kwa manati karibu wiki mbili zilizopita. Kumekuwa na matukio ya upotevu wa watoto kata ya Katumba ambapo kwa mjibu wa viongozi wa serikali ya Kijiji cha Mnyaki pamoja na wananchi,mtoto mmoja aliyepotea miaka mitano iliyopita hakupatikana mpaka sasa hatua ambayo kupatikana kwa watoto Rama na Vitisho limepokelewa kwa furaha. Source: Issack Gerald,Editor:Issack Gerald

MLIPUKO WA KIPINDUPINDU WILAYANI TANGANYIKA MKOANI KATAVI

Image
Na.Issack Gerald Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Salehe Muhando,amethibitisha kipindupindu kuingia katika wilaya hiyo. Muhando amesema mpaka kufikia jana Desemba 3,2017 wagonjwa 3 wameripotiwa kulazwa katika zahanati ya Isengule kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo. Aidha Muhando amesema wanaendelea kufuatilia maeneo mbalimbali ya wilaya ya Tanganyika kwa kuwa inasemekana tatizo lipo maeneo mengi ya Wilaya ya  Tanganyika. Kufuatia hatua hiyo,Mkuu wa Wilaya amewataka wakazi wa Wilaya ya Tanganyika kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo ikiwemo kuhakikisha kunakuwepo na usafi wa mazingira. Kwa kawaida binadamu hupata ugonjwa wa kipindupindu kwa kula kinyesi kibichi cha binadamu ambacho kwa kiasi kikubwa husambazwa na nzi. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WAKAZI WAOMBA TOZO ZA ZIMAMOTO ZISITISHWE MPAKA WAPATE UMEME NA BARABARA IMARA,KAMANDA AJIBU.

Na.Issack Gerald Wakazi wa Kata ya Katumba Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wameliomba jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoani Katavi,kutowatoza tozo za tahadhari ya majanga mpaka wapatiwe huduma ya umeme na kuboreshewa miundombinu ya barabara. Wametoa ombi hilo na kusema kwa sasa hawaoni umuhimu wa kutozwa tozo hiyo,wakati nyumba zao hazina umeme na barabara hazipitiki kiurahisi. Kwa upande wake kamanda wa jeshi hilo Mkoani Katavi Abdallah Maundu amesema,tozo wanazotoza ni kwa mjibu wa sheria ya nchi na wanatoa huduma katika majanga ya moto pia katika ajali. Maeneo mengi ya Mkoa wa Katavi yana tatizo la miundombinu ya barabara isiyopitika hasa msimu wa masika,jambo ambalo jeshi la zimamoto na uokoaji linatakiwa kujipanga namna litakavyotoa huduma kwa wakazi waishio katika maeneo ya miundombinu mibovu ya barabara. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED