MWENYEKITI WA KIJIJI MKOANI KATAVI AKATAA KUJIUZULU

Na.Issack Gerald

Mwenyekiti wa Kijiji cha Stalike Bwana Christopher Mrisho amesema hayuko tayari kuachia ngazi kwa tuhuma za kuwachangangisha pesa wananchi kinyume na sheria

Bw.Mrisho haoni umuhimu wa kufanya hivyo kwani ni wananchi wenyewe ndio waliomba kuchangisha pesa hizo.

Imedaiwa kuwa Bw.Mrisho  amewachangisha wananchi hao kwa awamu mbili tofauti zaidi ya shilingi milioni moja kwa madai kuwa anaenda kuonana na waziri mkuu wa Tanzania ili kuwasaidia kutatua mgogoro kati ya wananchi hao na mamlaka ya hifadhi za misitu Tanzania.

Mwenyekiti huyo anadaiwa kuwachangisa baadhi ya wananchi wa kijiji hicho ambao waliondolewa na serikali katika makazi hayo ikidaiwa kuwa walivamia hifadhi ya msitu


Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA