MWENDESHA BODABODA AMEMUUA BODABODA MWENZAKE,ASAKWA NA POLISI PANDE ZOTE

Mwendesha bodaboda maarufu mpaka wa Sirari na Isebania, Kenya,Kiongera Nchagwa (27) mkazi wa Kijiji cha Gwitiryo, Tarime Mara anasakwa na Polisi wa pande zote mbili, akituhumiwa kumuua mwenzake,Jeremia Omera (22) kwa kumchoma kwa kisu kifuani.
Mwenyekiti wa Haki za Binadamu Wilaya ya Kurya West ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Isebania, Peter Masaithe amesma tukio hilo limetokana na ugomvi wa kunyang’anyana mizigo ya abiria aliyetaka kuvuka mpaka kuingia nchini Tanzania akitokea Nairobi Kenya.
Masaithe amekemea bodaboda kutembea na visu,kunywa pombe za viroba ambavyo baada ya kupigwa marufuku sasa vimehamia Isebania hali inayochangia uhalifu na kuziomba serikali za nchi hizo mbili kuchukua hatua kali ukiwemo msako wa viroba na bangi ili kuokoa vijana.
Polisi wa Isebania wamethibitisha kifo cha Jeremia na wamewasiliana na wenzao wa Sirari kumsaka mtuhumiwa kujibu tuhuma ambapo pia Polisi wa Sirari wamekiri kupokea taarifa ya mauaji.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Sokoni Sirari,Benson Makanya amesema waendesha bodaboda Sirari na Isebania wamekuwa wakitembea na silaha kama visu na kuchangia uhalifu hapo. Mama mlezi wa Jeremia,mkazi wa Sirari Moraha Roman amesikitishwa na kifo chake na kusema alikulia kwao.
Ameiomba Serikali imfuatilie mtuhumiwa kwa madai mara nyingi akifanya matukio hutorokea Mugumu Serengeti kwa ndugu zake na kurejea baada ya muda.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Ombo Migori ukisubiri ndugu kutoka Soneka Kisii

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA