CHADEMA:TAARIFA ZA MNYIKA KUJIVUA UANACHAMA SIYO ZA KWELI ZIPUUZWE

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,kimekanusha Mbunge wa Jimbo la Kibamba na mwanachama wa Chadema John Mnyika kuwa amejivua uanachama.
Mbunge John Mnyika.
Hatua hii imekuja baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mbunge huyo amejivua uanachama kwenye chama chake cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Chama hicho ambacho kimekanusha taarifa kupitia ukurasa wake wa Twitter kimesema habari hizo hazina ukweli wowote za zinapaswa kupuuzwa.
Aidha chama hicho kimesema wanaosambaza habari za Mnyika kujivua uanachama ni walioishiwa hoja na majibu juu ya maisha ya watanzania.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA