Posts

Showing posts from November 7, 2017

MBUNGE WA KATAVI AMETETEA WANANCHI WALIOPO KATIKA MIPAKA YA HIFADHI YA RELI,WAKAZI WA MTAA WA MSASANI,TAMBUKARELI NA ILEMBO WAMEGUSWA

Image
Na.Issack Gerald SERIKALI imesema haina Mpango wa kulipa fidia kwa wakazi waliovamia hifadhi ya reli katika kipindi cha miaka ya 1904. Mh.Roda Kunchela(Chadema) Akiuliza swali bungeni mjini Dodoma,Mh.Roda Kunchela mbunge wa viti maalumu mkoani Katavi,amehoji mkakati wa serikali uliopo kwa sasa kuwalipa fidia wakazi wa mitaa ya Msasani,Tambukareli na Ilembo watakaobomolewa makazi ya hivi karibuni. Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Atashasta Justus Nditiye pamoja na mambo mengine amesema watakaolipwa fidia ni wakazi watakaokutwa na reli katika maeneo yao. Katika hatua nyingine,Naibu Waziri Mhandisi Atashasta Justus Nditiye amesema serikali itawachukulia hatua watumishi wote waliopimi viwanja hifadhi ya reli na kuwaruhusu wananchi kujenga. Wakazi wa mitaa ya Tambukareli na msasani wanatakiwa kupisha maeneo ya hifadhi ya reli kabla ya Mwezi Januari mwaka 2018. Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kujenga mtandao wa reli ya kati kat