Posts

Showing posts from October, 2017

UHURU KENYATA NA URAIS MWAKA 2017

Image
Rais Uhuru Kenyatta ametangazwa mshindi wa urais wa marudio nchini Kenya akiwa na kura 7,483,895 sawa na 98%. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati amesema kiongozi wa upinzani Raila odinga aliyesusia uchaguzi huo alipata kura 73,228 sawa na asilimia 0.96. Bw Chebukati amesema jumla ya wapiga kura 7,616,217 kati ya jumla ya wapiga kura 19.6 milioni ambao wamejiandikisha kuwa wapiga kura nchini humo walishiriki uchaguzi huo wa Alhamisi wiki iliyopita. Hiyo ni asilimia 38.84. Rais Kenyatta, akihutubu baada ya kutangazwa mshindi, amewashukuru waliompigia kura. Amesema uchaguzi uliomalizika ni ishara ya uthabiti wa demokrasia na uthabiti wa taasisi za Kenya pamoja na Wakenya wenyewe. "Agosti 8, na sitachoka, Wakenya walirauka kupiga kura. Na siku hiyo walinichagua bila shaka. Ushindi wangu ulipopingwa Mahakama ya Juu, kwenye hukumu, mahakama haikupinga ushindi wangu wa 54%. Takwimu hazikupingwa. Kilichokosolewa ni utaratibu uliopelekea ushindi wangu,&quo

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA

Image
Lazaro Nyalandu alizaliwa Agosti 18, 1970 mkoani Singida, hivyo atafikisha miaka 45 Agosti mwaka huu. Kwa sasa yeye ni Waziri wa Maliasili na Utalii. Historia yake Lazaro Nyalandu alizaliwa Agosti 18, 1970 mkoani Singida. Nyalandu alipata elimu ya msingi katika shule za Pohama na Mrumba zilizoko kijijini kwao huko mkoani Singida na kuhitimu mwaka 1987. Aliendelea na masomo ya kidato cha kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Kibaha mkoani Pwani (1988 –1991) na alifaulu vizuri na kujiunga na Shule ya Sekondari Ilboru ambako alisoma kidato cha tano na sita. Wakati akiwa mwanafunzi wa sekondari,Nyalandu alikuwa kiongozi wa juu wa Ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania(Ukwata) 1991–1993 na baadaye alikuwa miongoni mwa vijana wa Kitanzania walioteuliwa kuzuru jiji la Rio De Janeiro,Brazil na kushuhudia mkutano wa Mazingira mwaka 1993. Nyalandu alipata elimu yake ya Chuo Kikuu nchini Marekani ambako alihitimu Shahada ya kwanza ya Sanaa katika Usimamizi wa Biashar

ZITTO AMEMPONGEZA NYALANDU KUJIUDHURU NDANI YA CCM NA KUACHA UBUNGE

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo),Zitto Kabwe amempongeza Mbunge wa Singida Kaskazini(CCM), Lazaro Nyalandu kuwa ameonyesha uongozi uliokomaa. Zitto ametoa maoni yake hayo baada ya Nyalandu kuamua kujiondoa CCM na kuachia nafasi yake ya ubunge. Zitto ameandika, "Lazaro Nyalandu,umeonyesha uongozi. Kwa namna haki za watu zinavyovunjwa na uchumi wa nchi unavyoporomoka, unahitaji roho ngumu sana kuwa CCM.Umefanya maamuzi sahihi,wakati sahihi na kwa sababu sahihi. Kila la kheri." Lazaro Nyalandu leo ametangaza kujivua nafasi zake ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kuandika barua yake ya kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kwa kile alichodai kuwa Chama Cha Mapinduzi na Bunge vimekuwa vikishindwa kuisimamia serikali na badala yake kutumiwa na serikali jambo ambalo yeye anaona halina afya katika maendeleo ya nchi na linadidimiza haki mbalimbali.  Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com  au ukurasa P5Tanzania Limited

WANAFUNZI KIDATO CHA NNE KATAVI WAMESEMA WATAFAULU MTIHANI

Image
Na.Issack Gerald-Katavi Baadhi ya watahiniwa wa mtihani wa kidato cha nne katika shule mbalimbali za manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameeleza matumaini ya kufaulu mtihani wao ulioanza leo nchi nzima. Wakizungumza kwa nyakati tofauti,wanafunzi hao wakiwemo wa shule ya sekondari Mwangaza na Kashaulili wamesema maandalizi yao katika mtihani huo yako vizuri huku wakiwaomba wenzao kuondoa hofu ya mtihani. Kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari Mwangaza Mwl.Simoni Lubange amewataka wanafunzi wake kujiamini na kumtanguliza mungu katika ujibuji wa mitihani yao kwa alichokisema hakuna kitu kigeni watakachokutana nacho. Jumla ya watahiniwa 385,938 wa kidato cha nne nchini wameanza mtihani leo huku baraza la mitihani likitoa onyo kwa na tahadhari kwa wamiliki wa shule watakaofanya udanganyifu. Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com  au ukurasa P5Tanzania Limited

SERIKALI KUFUNGUA UTALII KANDA YA KUSINI

Image
Na.Issack Gerald-Rukwa Serikali imesema imedhamiria kufungua utalii wa Kanda ya Kusini ili kupanua wigo wa vivutio vya utalii nchini na hatimaye kuongeza idadi ya watalii na kipato kwa Serikali na jamii kwa ujumla. Hatua hiyo imeelezwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga katika kijiji cha Kapozwa Wilayani Kalambo Mkoani Rukwa,wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa kina kirefu barani Afrika. Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo benki ya Dunia kupitia mradi wa REGROW imepanga kuboresha miundombinu ya vivutio vya utalii vya Kanda ya Kusini na kuvitangaza,ili kuimarisha sekta hiyo muhimu ambayo inachangia asilimia 25 ya mapato yote ya kigeni na asilimia 17.5 ya pato la taifa. Aidha,ametoa wito kwa wananchi wa kijiji cha Kapozwa wanaoishi jirani na hifadhi kushirikiana na Serikali katika uhifadhi wa uoto wa asili pamoja na kudumisha tamaduni zao. Vivutio vingine ni p

WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI WARIDHISHWA NA HATUA ZA SERIKALI KATIKA KUWAKWAMUA NA UMASKINI

Na.Issack Gerald-Katavi WATU wenye ulemavu Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamesema wameridhika na hatua zinazochukuliwa na Manispaa ya Mpanda katika kushughulikia mahitaji yao ikiwemo suala la mikopo. Hayo yamebainishwa leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika shule ya msingi Azimio ukihusisha watu wenye ulemavu na wataalamu wa idara ya maendeleo ya mjamii Manispaa ya Mpanda kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kupata mikopo na uundaji vikundi vya kijasiliamali. Afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Mpanda Linus Kalindo pamoja na mambo mengine amewataka watu wenye ulemavu kutoona ulemavu ni mwisho wa maisha na badala yake waendelee kufuata nmna wanayoelekezwa ili wapatiwe mikopo. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya watu wenye Ulemavu SHIVYAWATA Mkoani Katavi Issack Mlela amesema watazingatia yote wanayoshauriwa na wataalamu ikiwemo kuunda vikundi,kusajili vikundi na hatimaye kupatiwa mikopo. Hii ni mara ya pili katika kipindi cha mwezi huu w

DAKTARI MTANZANIA AFUTWA KAZI NA MADIWANI

Image
Daktari mmoja wilayani Kisarawe amefutwa kazi baada ya kukutwa na makosa mbalimbali yanayotia hofu juu ya utendaji kazi katika majukumu yake ya kila siku. Uamzi huo wa kumfuta kazi Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mtakayo Emmanuel Shumbusho,umefikiwa na  Baraza la Madiwani halmashauri ya Kisarawe mkoani Pwani. Dkt Emmanuel Shumbusho anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo uzembe,utoro kazini ambapo hajaonekana kazini kwa takaribani siku tisa bila taarifa yoyote kwa mwajiri wake. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamis Dikupatile akitoa maamuzi amesema,wamefikia hatua hiyo baada ya kubaini mapungufu mengi kutoka kwa mtumishi huyo. Madiwani wote kwa pamoja walikubaliana na uamzi huo kutokana na uzembe wa daktari huyo katika suala zima la utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi na kusababisha kuibuka kwa usumbufu mkubwa kutokana na kutopatiwa matibabu kwa wakati.

MADIWANI MANISPAA YA MPANDA WAMETOA TAMKO LA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA UONGOZI WAKE

Na.Issack Gerald-Katavi Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa Mpanda mkoani  Katavi  wamempongeza rais John Magufuli kwa ujasiri aliouonesha wa kulinda  rasilimali za nchi  hasa  katika suala la madini. Pongezi hizo zilitolewa jana kupitia waandishi wa habari ambapo Meya wa Manispaa ya Mpanda Willium Mbogo alizungumza niaba ya madiwani hao. Aidha Mbogo alisema wanawalaani vikali baadhi ya watu ambao wanaobeza jitihada zinazofanywa  na rais  za kulinda rasilimali zetu za  nchi na hasa madini  kwa  ajili ya  manufaa ya Watanzania  wote. Alisema madiwani wa  Manispaa ya Mpanda wanaamini mapato hayo yatakayopatikana  yataongezeka  Serikalini na halmashauri zote zitaongeza uwezo wa kuwahudumia wananchi. Kwa upande wake diwani wa Kata ya makanyagio Haidari  Sumry aliomba jitihada za rais zisiishie kwenye madini tu bali nguvu iongezeke kwenye   maeneo   mengine   iliuchumi wa  nchi ukue na kuongezeka zaidi ya hivi sasa.  Alisema endapo rasilimali za nchi zitasimamiwa vizuri halmas

WAKULIMA WAMESHAURIWA KUWEKA KIPAUMBELE KILIMO CHA MAZAO YA CHAKULA

Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi Wakulima wametakiwa kuyapa kipaumbele mazao ya chakula katika msimu wa huu wa kilimo ili kuwa na uhakika wa chakula Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Bi Lilian. Matinga wakati akihutubia mkutano wa ufunguzi wa msimu wa kilimo ulifanyika leo katika viwanja vya shule ya msingi kakese Bi matinga amesema kuwa ili kuweza kupiga vita njaa wananchi wote hawana budi kulima kwa nguvu zao zote ili kuhakikishia akiba ya kutosha ya chakula mwisho wa msimu Katika hatua nyingine Bi Matinga amewataka maafisa ugani kuwa na mashamba darasa ili yawasidie wakulima kulima kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo cha kisasa Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wameishukuru hatua ya manispaakuzindua mradi huo katika kijiji chao na kuwasogezea huduma za pembejeo za kilimo katika maeneo yao.

WAKAZI KITONGOJI CHA SITUBWIKE WADAIWA KUKAIDI KUONDOKA HIFADHINI

Na.Issack Gerald-Katavi Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga,amewataka wananchi wa Kitongoji cha Situbwike waliovamia Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kuanzisha shughuli za kibinadamu kinyume cha sheria waondoke kwa hiari ndani ya wiki mbili zijazo kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI WAPYA NGAZI YA WIZARA NA MIKOA,ABADILISHA WAKUU WA MIKOA GHAFLA

Image
Na.Issack Gerald-Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha Makatibu Wakuu wapya,Naibu Makatibu Wakuu wapya na Wakuu wa Mikoa wapya sita. Rais Mgaufuli mara baada ya kuwaapisha walioteuliwa ,amewaagiza walioapishwa kutatua matatizo ya wananchi kwa wakati bila kusubiri kusukumwa. Katika hatua nyingine,rais Magufuli amefanya mabadiliko ya ghafla akiwa ikulu wakati akiwaapisha walioteuliwa,ambapo Bi. Christine Solomon Mndeme aliyetakiwa kuwa mkuu wa Dodoma atakuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma. Aidha aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt. Binilith Mahenge,ameteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Dodoma akichukua nafasi ya Christine Solomon Mndeme aliyetakiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Wakati huo huo Rais Magufuli amesema shilingi bilioni 147 alizoidhinisha kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu,zitolewe kama inavyotakiwa kwa wakati na pia kwa wanafunzi wenye sifa. Habari  zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukura

RC KATAVI:UJENZI WA ZAHANATI YA KAKESE UKAMILIKE KABLA YA DESEMBA MOSI MWAKA HUU

Image
Na.Issack Gerald-Katavi MKUU wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya muhuga,ameagiza ujenzi wa wadi ya wazazi katika zahanati ya kata ya Kakese kukamilika kabla ya Desemba Mosi mwaka huu.

CWT NSIMBO WAMEFANYA UCHAGUZI WAWAKILISHI MAHALA PA KAZI,NAFASI YA WENYE ULEMAVU KAMA KAWAIDA

Na.Issack Gerald-Katavi WALIMU wanne akiwemo Onorine Boniface mwakilishi wa walimu wenye ulemavu katika Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi,wamechaguliwa kuwakilisha walimu wenzao katika chama CWT ndani ya halmashauri hiyo wakitoka katika shule wanazofundisha.

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA IMEFUNGUA SEMINA YA USINDIKAJI SAMAKI.

Image
Na.Issack Gerald-Tanganyika IDARA ya uvuvi Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi imezindua mafunzo ya siku kumi ya uvuvi,uchakataji na usindikaji wa mazao ya samaki.

MAJOPKOFU YA KUHIFADHIA MAITI MKOANI RUKWA ZAIDI YA WEZI HAYAFANYI KAZI.

MAJOKOFU ya chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Rukwa yameharibiribika kwa zaidi ya mwezi mmoja mpaka sasa. 

WALIMU WANAUSUBIRI MWEZI NOVEMBA KWA HAMU, MADARAJA, MISHAHARA NA MENGINE KEDEKEDE

Na.Issack Gerald-Nsimbo SERIKALI inatarajia kuanza kulipa madeni,kuajiri na kupandisha madaraja kwa walimu kuanzia mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.

RAIS MAGUFULI KUWAAPISHA VIONGOZI 54 WA WIZARA NA MIKOA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo mchana anatarajia kuwaapisha Makatibu Wakuu wapya, Naibu Makatibu Wakuu wapya na Wakuu wa Mikoa wapya baada ya jana kufanya mabadiliko katika safu ya uongozi wa nyadhifa hizo. WATEULE 1.                    Ofisi ya Rais Ikulu. ·                      Katibu Mkuu – Bw. Alphayo Kidata 2.                  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. ·                      Katibu Mkuu ( Utumishi ) – Dkt. Laurian Ndumbaro ·                      Naibu Katibu Mkuu – Dorothy Mwaluko ( ATAAPISHWA ) 3.                  Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI ). ·                      Katibu Mkuu – Mhandisi Mussa Iyombe ·                      Naibu Katibu Mkuu( Afya ) – Dkt. Zainabu Chaula ·                      Naibu Katibu Mkuu( Elimu ) – Bw. Tixon Nzunda 4.                  Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira. ·                      Katibu Mk