MBUNGE WA KATAVI AMETETEA WANANCHI WALIOPO KATIKA MIPAKA YA HIFADHI YA RELI,WAKAZI WA MTAA WA MSASANI,TAMBUKARELI NA ILEMBO WAMEGUSWA

Na.Issack Gerald
SERIKALI imesema haina Mpango wa kulipa fidia kwa wakazi waliovamia hifadhi ya reli katika kipindi cha miaka ya 1904.
Mh.Roda Kunchela(Chadema)
Akiuliza swali bungeni mjini Dodoma,Mh.Roda Kunchela mbunge wa viti maalumu mkoani Katavi,amehoji mkakati wa serikali uliopo kwa sasa kuwalipa fidia wakazi wa mitaa ya Msasani,Tambukareli na Ilembo watakaobomolewa makazi ya hivi karibuni.
Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Atashasta Justus Nditiye pamoja na mambo mengine amesema watakaolipwa fidia ni wakazi watakaokutwa na reli katika maeneo yao.
Katika hatua nyingine,Naibu Waziri Mhandisi Atashasta Justus Nditiye amesema serikali itawachukulia hatua watumishi wote waliopimi viwanja hifadhi ya reli na kuwaruhusu wananchi kujenga.
Wakazi wa mitaa ya Tambukareli na msasani wanatakiwa kupisha maeneo ya hifadhi ya reli kabla ya Mwezi Januari mwaka 2018.
Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kujenga mtandao wa reli ya kati katika kiwango cha kimtaifa cha Standard Gauge yenye urefu wa kilomita 4886 ambapo katika ukanda wa kati ni urefu wa 2561 ikiwa ni kutoka Dar-Isaka-Mwanza,Tabora-uvinza-Kigoma kilomita 411,Kaliua- Mpanda-Karema kilomita 321,Isaka-Rusumo kilomita 371 wakati kilomita 36 ni kutoka Keza-Ruvubu na Uvinza- Kalelema-Msongati kilomita 203.
Ukanda wa Kusini unaojumuisha reli kutoka Mtwara hadi Mbambabay yenye matawi yake ya kuelekea Liganga kwa ajili ya chuma na Mchuchuma kwa ajili ya makaa ya mawe ina urefu wa kilomita 1092 huku ukanda wa Kaskazini unaojumuisha mikoa ya Tanga,Arusha hadi Musoma ikiwa na urefu wa kilomita 1233.
Kikao cha leo ni cha kwanza katika bunge la 11 katika mkutano wa tisa wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania 

          Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA