Posts

Showing posts from April 13, 2018

TMA WATOA TAHADHARI YA MVUA KUBWA LEO APRILI 13,2018

Image
Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania TMA imesema vipindi vifupi vya mvua kubwa vinatarajiwa leo Aprili 13,2018. Katika taarifa ya mamlaka hiyo ambayo imetolewa jana Aprili 12,2018 mikoa ambayo inatarajiwa kuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa ni Kagera,Geita, Mwanza,Mara, Shinyanga,Simiyu,Kigoma,Tabora,Katavi,Morogoro, Ruvuma,Dar Es Salaam, Pwani, Tanga Pamoja Na Visiwa Vya Unguja Na Pemba. Aidha TMA imetoa angalizo kwa kusema kuwa Vipindi Vifupi Vya Mvua Kubwa Vinatarajiwa Katika Baadhi Ya Maeneo Ya Mikoa Ya Rukwa, Njombe, Mbeya, Iringa Na Songwe. Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com

RC KATAVI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI KESHO JUMAMOSI APRILI 14,2018

Image
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga kesho siku ya Jumamosi Aprili 14,2018 ameitenga kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi. Kwa mjibu wa kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi,Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na maeneo mengine ya Mkoa wa Katavi kufika katika viwanja vya Azimio Mjini Mpanda kuanzia majira ya saa 4:00 asubuhi ili kueleza kero zao. Muhuga amesema atasikiliza kero za wananchi wote zinazohusu masuala mbalimbali na kuzipatia majibu papo hapo. Hii ni mara ya Kwanza kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga,kusikiliza kero za wananchi katika eneo la wazi linalojumuisha wananchi wote tangu alipoteuliwa mwaka 2016 kuwa Mkuu wa Mkoa kabla ya hapo amekuwa akisikiliza kero za wananchi Ofisini kwake. Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com

RAIS MAGUFULI LEO APRILI 13,2018 KUWAVALISHA VYEO MAOFISA WA JWTZ AKIWEMO MKUU WA WILAYA YA BUHIGWE ANAYEREJESHWA JESHINI

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli leo Aprili 13,2018 anatarajia kuwavalishwa vyeo maofisa mbalimbali wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)   ambao amewapandisha vyeo jana Aprili 12,2018. Kati ya maofisa hao yumo Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Kanali M E Gaguti ambaye sasa anapanda cheo na kuwa Brigedia Jenelari na kurejeshwa Jeshini. Kwa mjibu wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania , Jenelari Venancy Mabeyo amesema maofisa walioteuliwa wanakwenda kuimarisha safu za utendaji kazi kijeshi. ORODHA YA WALIOPANDISHWA VYEO 1.Meja Jenerali Peter Massao aliyepandishwa kuwa Luteni Jenarali. 2.Brigedia Jenerali Henry Kamunde aliyepandishwa na kuwa meja jenerali. 3.D.D.M Mullugu 4.J.J Mwaseba 5.A.S Mwamy 6.R.K Kapinda 7.C.D Katenga 8.Z.S Kiwenge 9.M.A Mgambo 10.A.M Alphonce 11.A.P Mutta 12.A.V Chakila 13.M.G Mhagama 14.V.M Kisiri 15.C.E Msolla 16.S.M Mzee 17. C.J Ndiege 18.I.M Mhona 19.R.C Ng’umbi 20.S.J Mnkande 21

ZITTO ATAKA TAMISEMI IMTAFUTE MWENYEKITI WA HALAMSHAURI ALIYETOWEKA

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT -Wazalendo),Zitto Kabwe amemtaka waziri wa Tamisemi kulitafutia ufumbuzi suala la kutoweka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kakonko, Simon Kangue. Amesema hayo bungeni jana Aprili 12,2018 alipochangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais,yenye wizara za Tamisemi,Utumishi na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2018/2019. “Habari zinazosambaa Kibondo tayari ameuawa. Tunataka maelezo ya mtu huyo,sisi watu wa Kigoma ni Kigoma kwanza kabla ya kuwa Watanzania naomba hilo mlielewe,” amesema. Zitto amesema mara ya mwisho kuonekana mwenyekiti huyo aliitwa kwa mkurugenzi na kukutana na ofisa usalama wa wilaya. Amesema tangu siku hiyo hajulikani alipo mwenyekiti huyo licha ya jitihada za kumtafuta kufanyika. “Familia imechukua hatua mbalimbali,imelalamika na sisi wajumbe wenzake tumehoji kwenye vikao,hakuna maelezo yoyote kutoka serikalini,”alisema Zitto.