Posts

Showing posts from March 16, 2018

WALIMU 16 WAFUTWA KAZINI

Image
JUMLA ya walimu 16 wamefukuzwa kazi wilayani Nkasi mkoani Rukwa kwa kipindi cha miaka mitatu na wengine 11 wamepewa onyo kali baada ya kubainika wametenda makosa mbalimbali. Hatua hiyo imethibitishwa jana na Katibu wa tume ya utumishi wa walimu TSC wilayani humo  Richard Katyega mbele ya kamishina wa tume ya Utumishi wa walimu Taifa,Samwel Koroso ambapo alisema  kuwa katika kipindi hicho  walipokea mashauri 23 na kupelekea walimu 16 kufukuzwa kazi,11 kupewa onyo kali na wengine 5 waliondolewa kazini baada ya kubainika kuwa na vyeti bandia. Alisema katika mwaka wa fedha wa 2016,2017 na 2018  tume hiyo imesikiliza mashauri hayo na kuyatolea maamuzi ambapo ilifikia maamuzi hayo baada ya kusikiliza mashauri hayo na pasipo kumuonea mwalimu hata mmoja na kutenda haki kwa mujibu wa sheria. Katyega alisema tume hiyo sambamba na kuchukua maamuzi hayo pia imekua ikiwahamasisha walimu kufuata maadili ya ualimu kwa uhakika ili wasiweze kukumbana na adhabu mbalimbali ikiwemo kufukuzwa kazi

MWENYEKITI WA BAJAJI MANISPAA YA MPANDA ANG’ATUKA

Image
Mwenyekiti wa Chama cha madereva pikipiki za tairi tatu maarufu bajaji halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Bw.Rashid Rashid ametangaza kujiuzuru nafasi hiyo. Katika taarifa yake ambayo ameitoa leo Bw.Rashid amesema, miongoni mwa sababu za kujiuzulu kwake ni pamoja na kukosa ushirikiano kutoka kwa madereva wenzake,ukosefu wa ushirikiano kwa kamati yake na kutotekelezwa kwa mipango mbalimbali wanayoipanga kama chama. Aidha amesema changamoto iliyopo kwa sasa ni mgawanyiko wa wamiliki bajaji upande wa watumishi wa serikali kutozingatia kanuni na taratibu za umiliki wa chombo hicho cha usafiri. Kwa upande wa wamiliki binafsi na madereva wao amesema wamekuwa wakikumbwa na mikasa ya kupelekwa kituo cha polisi pamoja na kulipishwa faini mara kwa mara bila utaratibu. Hata hivyo Bw.Rashid amekanusha kula njama na Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumtra kuwatoza madereva bajaji mpaka kiasi cha shilingi 40,000 kwa ajili ya kujinufaisha. Mapema mwaka h

IFAHAMU TUMBAKU ASILI YAKE,ATHARI KIAFYA,KILIMO MPAKA UVUNAJI NA NCHI ZINAZOONGOZA KILIMO DUNIANI

Image
Tumbaku  (pia  tumbako ) ni majani ( minoga ) makavu ya  mtumbaku  ambayo yanatumiwa na binadamu kwa kuvuta kama sigara,kutafuniwa mdomoni au tumbaku ya kunusa. Tumbaku huwa ndani yake kemikali ya  nikotini  ambayo mwili unazoea haraka sana na kuifanya vigumu kwa wavuta tumbaku kuachana na desturi hii. 1. Asili ya tumbaku 2. Kazi ya nikotini ndani ya tumbaku 3. Hatari za kiafya 4. Kilimo 5. Baada ya mavuno Asili ya tumbaku Asili ya tumbaku ni Amerika ambako  Maindio  wenyeji waliitumia kama dawa ya kidini pia ya burudani. Tangu  Kolumbus  Wahispania walipeleka mtumbaku hadi Ulaya ambako uliangaliwa mwanzoni kama mmea wa kiganga. Matumizi hasa kwa njia ya kuvuta na kutafuna yalienea haraka katika Ulaya na kwa njia ya mabaharia Wareno katika pande zote za dunia. KAZI YA NIKOTINI NDANI YA TUMBAKU Tumbaku inavutiwa hasa kwa sababu nikotini ambayo ni dawa ndani yake inaathiri ubongo na neva ya binadamu na kupunguza uchovu na kusaidia mtu kusikia utulivu na raha

RAIS MAGUFULI AZINDUA KIWANDA CHA SIGARA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli leo amezindua kiwanda cha kutengeneza sigara cha Philips Morris International kilichopo mkoani Morogoro. Rais Magufuli ametembelea kiwanda hicho na kushuhudia namna sigara zinavyotengenezwa kuanzia katika hatua ya kwanza mpaka sigara inapokamilika kwa matumizi au kwa ajili ya kuuzwa.

TUNDU LISSU AFANYIWA OPARESHENI YA 19 AWASHUKURU WANAOMUOMBEA

Image
Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya (CHADEMA) Tundu Lissu amefunguka na kuwashukuru Watanzania kwa maombi yao kwake kufuatia oparesheni nyingine ya 19 ambayo amefanyiwa katika mguu wake.  Tundu Lissu juzi alifanikiwa kufanyiwa oparesheni hiyo katika mguu wake wa kulia na kuisha salama,madaktari waliamua kufanya oparesheni hiyo kufuatia kugundua moja ya mfupa wake ulikuwa ukichelewa kuunga na kudai kuwa kama wasingefanya upasuaji na kurekebisha mfupa huo ungeweza kuchelewa zaidi na kuja kuvunjika baadae.  Hata hivyo Watanzania mbalimbali wameendelea kumuombea Tundu Lissu ili aweze kupona haraka na kurudia tena katika hali yake ya zamani ili aweze kurudi nyumbani Tanzania na kuendelea na majukumu yake ya kila siku.  Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi mnano Septemba 7, 2017 na watu wasiojulikana akiwa mjini Dodoma na kisha baadae kupelekwa nchini Kenya kwa matibabu ambapo huku alifanyiwa oparesheni kadhaa katika mwili wake na baadae alikwenda nchino Beljium kwa matibabu