Posts

Showing posts from February 6, 2018

RAIS MAGUFULI AZINDUA KITUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI

Image
Rais Dkt.Magufuli leo   amezindua Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi (Comprehensive Training Center – CTC) kilichopo Mapinga Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani. Kituo hicho kimejengwa kwa msaada kutoka Jeshi la Ukombozi la Watu wa China kwa gharama ya Shilingi Bilioni 67.87 na kitatumika kutoa mafunzo ya kijeshi ya kisasa yatakayowawezesha askari kukabiliana na vitisho vya kisasa vya kiusalama.

DKT.SLAA ASEMA HAKUBALIANI NA KUPIGWA MARUFUKU MIKUTANO YA KISIASA

Image
Aliyekuwa Katibu Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Dkt.Wilbroad Slaa amefunguka baada ya katazo kwa vyama vya siasa kuendesha mikutano ya hadhara. Dkt. Slaa ambaye kwa sasa ni Balozi amekiambia kituo cha runinga cha Clouds kuwa hakubaliana na jambo hilo kwa sababu uwepo wa mikutano hiyo ni kitu ambacho kilipitishwa na bunge. Katika hatua nyingine Dkt. Slaa amesema yeye ni muumini wa Demokrasia na anapenda uwepo wa vyama vingi ila muelekeo wa kisiasa nchini kwasasa haumfurahishi. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

NDEGE MPYA ZA SERIKALI SASA KULETWA MWEZI JULAI 2018.

Image
Ndege mbili moja aina ya Bombardier na nyingine kubwa Boeing 787 yenye uwezo wa kubeba abiria 262 zilizonunuliwa na serikali zinatarajiwa kuwasili nchini Julai mwaka huu. Serikali imenunua ndege hizo ikiwa ni mkakati wa kuimarisha Shirika la Ndege (ATCL) ili limudu ushindani kwenye biashara ya kusafirisha abiria na kujiendesha kwa faida. Akiwasilisha taarifa ya shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwa kipindi cha Januari 2017 hadi jana,Mwenyekiti wa kamati hiyo,Prof.Norman Sigalla, alisema wamejulishwa kuwa pamoja na ndege mbili mpya aina ya Dash 8 Q400,Julai serikali inategemea kupokea ndege zingine mbili ambapo moja ni Dash 8 Q400 na nyingine aina ya Boeing 787. Alisema kwa sasa ATCL ina ndege tatu zinazofanya safari ndani na nje ya nchi. Katika hatua nyingine Prof.Sigalla pia alisema Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) inashauriwa kuhakikisha viwanja vya ndege visivyokuwa na hati vinapimwa kisha kupatiwa hati miliki. Alisema viwanja hivyo pia vinapa

JUMUIYA YA ULAYA (EU) WAMTEMBELEA TUNDU LISSU KUMJULIA HALI

Image
Maofisa watatu wa Jumuiya ya Ulaya (EU) jana  Februari wamemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),Tundu Lissu anayeendelea na matibabu nchini Ubelgiji. Lissu alishambuliwa kwa zaidi ya risasi 30,Septemba 7 mwaka jana na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na siku hiyohiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi alipolazwa hadi Januari 6,mwaka huu alipohamishiwa Ubelgiji katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, anakoendelea na matibabu. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana Februari 5,2018 Lissu amewataja maofisa hao kuwa ni Mkuu wa Idara ya Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki katika Wizara ya Nje ya EU,Patrick Simonnet. Wengine ni Mkuu wa Dawati la Tanzania katika EU,Marta Szilagyi,Vania Bonalbert ambaye ni ofisa wa ubalozi wa EU Tanzania anayeshughulikia masuala ya utawala bora na haki za binadamu na Hortensia May Lyatuu. Amesema ujumbe wa maofisa hao mbali ya kumjulia hali walifanya mazungumzo ya masuala mbali mbali yanayohusu Tanzania. Haba

ZANZIBAR KUADHIMISHA SIKU YA SHERIA

Image
Jaji mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu amesema katika kuadhimisha siku ya sheria Nchini ,mahakama imekusudia kuandaa maonesho maalumu kwa ajili ya kutoa elimu ya sheria kwa wananchi ili kupunguza uvunjifu wa sheria.  Akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na shamrashamra za siku ya Sheria Jaji makungu amesema maonesho hayo yatakayodumu kwa muda wa siku tatu pia yatawapa fursa wafanya bishara kuuza biashara zao. Amesema mbali na Maonesho hayo pia  Kutakuwa na Ufunguzi wa Mahakama ya Wilaya ya mwanakwerekwe baada ya kumalizika kwa ukarabati wa Mahakama hiyo ambayo itafunguliwa na Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Muhammed Shein.  Aidha amesema katika shamrashamra hiyo kutakuwa na matembezi ya siku ya sheria yatayoongozwa na Spika wa baraza la wawakilishi kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujua umuhimu wa kufuata sheria . Akizungumzia mafanikio waliyapata katika uendeshaji wa kesi kwa wananchi hususan kesi za Udhalilishaji amesema mpaka s