JUMUIYA YA ULAYA (EU) WAMTEMBELEA TUNDU LISSU KUMJULIA HALI



Maofisa watatu wa Jumuiya ya Ulaya (EU) jana  Februari wamemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),Tundu Lissu anayeendelea na matibabu nchini Ubelgiji.
Lissu alishambuliwa kwa zaidi ya risasi 30,Septemba 7 mwaka jana na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na siku hiyohiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi alipolazwa hadi Januari 6,mwaka huu alipohamishiwa Ubelgiji katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, anakoendelea na matibabu.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana Februari 5,2018 Lissu amewataja maofisa hao kuwa ni Mkuu wa Idara ya Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki katika Wizara ya Nje ya EU,Patrick Simonnet.
Wengine ni Mkuu wa Dawati la Tanzania katika EU,Marta Szilagyi,Vania Bonalbert ambaye ni ofisa wa ubalozi wa EU Tanzania anayeshughulikia masuala ya utawala bora na haki za binadamu na Hortensia May Lyatuu.
Amesema ujumbe wa maofisa hao mbali ya kumjulia hali walifanya mazungumzo ya masuala mbali mbali yanayohusu Tanzania.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA