Posts

Showing posts from May 23, 2018

MAHAKAMA KUU YAMWACHIA HURU DIWANI WA CCM KATA YA KATUMBA

Mahakama kuu kanda ya Sumbawanga Mkoani Rukwa ,imemwachia huru diwani wa kata ya Katumba halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mh.Senetor Baraka(ccm) miezi sita baada ya kuhukumiwa kutumikia kifungo cha miaka sita jela. Katika mahojiano na P5TANZANIA LIMITED Mh.Baraka amesema mahakama kuu kanda ya Sumbawanga imemwachia huru mei 18 mwaka huu baada ya kukata rufaani na mahakama kujiridhisha kuwa hana hatia. Hata hivyo amesema kuachiwa kwake huru kusihusishwe na msamaha wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.John Pombe Magufuli. Mwezi Novemba mwaka 2017,mahakama wilayani Mlele Mkoani Katavi ilimhukumu senator Baraka kutumikia kifungo cha miaka sita kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mfugaji wa ng’ombe katika kata ya Katumba ili amruhusu achungie mifugo katika eneo lililozuiliwa na mahakama. Mapokezi ya diwani huyo yamefanyika katika Kijiji cha Msaginya Getini njiapanda ya kwenda Tabora na Mnyaki Katumba. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED