Posts

Showing posts from April 14, 2018

DOKTA TITUS KAMAN ADAIWA KUMTELEZA MWANAMKE KATAVI BAADA YA KUMZALISHA MTOTO MWENYE ULEMAVU

Mwanamke mmoja ambaye amejitambulisha kwa jina la Bi.Amina Salumu mkazi wa wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi amedai Dkt.Titus Kamani ambaye amewahi kuwa kiongozi mkubwa hapa nchini amemtelekeza mwanamke huyo baada ya kuona amejifungua mtoto mwenye ulemavu. Bi.Amina Salumu ametoa malalamiko hayo leo Aprili 14,2018 katika uwanja wa Azimio Mjini Mpanda kupitia mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi. Kwa mjibu wa Mwanamke huyo,Titus Kamani mbunge aliyeko Dodoma kwa sasa amewahi kuwa Dkt.Mkuu katika Hospitali ya Reft Valley pia mbunge Mkoani Mwanza ambapo. Mbali na mwanamke huyo wanawake wengine wamedaiwa kutelekezwa,kutishwa maisha na waume waliowazalisha huku wengine wakinyimwa matumizi muhimu ya kifamilia. Wananchi wengi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi wamejitokeza katika uwanja wa Azimio ili kueleza kero zao kwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi meja jeneral Mstaafu Raph

BARABARA YA MPANDA—TABOARA YAFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga ametangaza barabara ya Mpanda– Tabora kufungwa kwa muda usiojulikana kuanzia leo Jumamosi Aprili 14,2018. Katika picha ni gari lililosombwa na maji 2016 na kuuwa watu Mkuu wa Mkoa ametoa kauli hiyo leo katika mkutano wa hadhara ambao ameuitisha kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi kupitia mkutano amabo umeitishwa katika uwanja wa Azimio mjini Mpanda. Muhuga amesema barabara hiyo imefungwa baada ya maji kujaa barabarani kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha na hivyo kuhatarisha maisha ya wasafiri. Kwa upande wake mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra Mkoani Katavi Amani Mwakalebela amesem kutokana na barabara kuharibika kwa kiasi kikubwa,wenye mabasi watalazimika kusafirisha abiria kupitia mkoani Kioma au Mbeya. Mwaka 2016 barabara ya Mpanda – Tabora ilifungwa baada ya kukatika kwa daraja la mto Koga ambapo takribani watu 10 walipoteza maisha baada ya gari walilokuwa wakisafiria