BARABARA YA MPANDA—TABOARA YAFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA


Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga ametangaza barabara ya Mpanda–Tabora kufungwa kwa muda usiojulikana kuanzia leo Jumamosi Aprili 14,2018.
Katika picha ni gari lililosombwa na maji 2016 na kuuwa watu
Mkuu wa Mkoa ametoa kauli hiyo leo katika mkutano wa hadhara ambao ameuitisha kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi kupitia mkutano amabo umeitishwa katika uwanja wa Azimio mjini Mpanda.
Muhuga amesema barabara hiyo imefungwa baada ya maji kujaa barabarani kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha na hivyo kuhatarisha maisha ya wasafiri.
Kwa upande wake mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra Mkoani Katavi Amani Mwakalebela amesem kutokana na barabara kuharibika kwa kiasi kikubwa,wenye mabasi watalazimika kusafirisha abiria kupitia mkoani Kioma au Mbeya.
Mwaka 2016 barabara ya Mpanda – Tabora ilifungwa baada ya kukatika kwa daraja la mto Koga ambapo takribani watu 10 walipoteza maisha baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com  


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA