DOKTA TITUS KAMAN ADAIWA KUMTELEZA MWANAMKE KATAVI BAADA YA KUMZALISHA MTOTO MWENYE ULEMAVU

Mwanamke mmoja ambaye amejitambulisha kwa jina la Bi.Amina Salumu mkazi wa wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi amedai Dkt.Titus Kamani ambaye amewahi kuwa kiongozi mkubwa hapa nchini amemtelekeza mwanamke huyo baada ya kuona amejifungua mtoto mwenye ulemavu.
Bi.Amina Salumu ametoa malalamiko hayo leo Aprili 14,2018 katika uwanja wa Azimio Mjini Mpanda kupitia mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Kwa mjibu wa Mwanamke huyo,Titus Kamani mbunge aliyeko Dodoma kwa sasa amewahi kuwa Dkt.Mkuu katika Hospitali ya Reft Valley pia mbunge Mkoani Mwanza ambapo.
Mbali na mwanamke huyo wanawake wengine wamedaiwa kutelekezwa,kutishwa maisha na waume waliowazalisha huku wengine wakinyimwa matumizi muhimu ya kifamilia.
Wananchi wengi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi wamejitokeza katika uwanja wa Azimio ili kueleza kero zao kwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi meja jeneral Mstaafu Raphael Muhuga aliwaahidi wananchi kuwa kero zao zote zitajibiwa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com  

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA