Posts

Showing posts from September 10, 2015

WANAFUNZI WATAKA AHADI YA ELIMU BURE ITEKELEZWE

Na.Issack Gerald-Mpanda BAADHI ya wanafunzi wa darasa la saba wanaohitimu elimu ya msingi Wilayani Mpanda Mkoani Katavi wamewataka wagombea wa nafasi mbalimbali  za uongozi watakaoshinda katika uchaguzi wa mwezi Oktoba kuhakikisha wanatekeleza ahadi ya kutoa elimu bure. Kauli hiyo imetolewa leo na wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi zilizopo katika Manispaa ya Mpanda ikiwemo shule ya Msingi Kashato. Wakati huo huo Msimamizi mkuu wa mitihani katika shule ya Msingi Kashato mwalimu Sekela Mayeji, amesema Jumla ya wanafunzi 108 wamefanya mtihani katika hali ya  utulivu. Katika mtihani huo Jumla ya wanafunzi wapatao laki saba kote nchini wanatarajia kumaliza mitihani ya kuhitimu darasa la saba leo.