Posts

Showing posts from December 9, 2017

MVUA YA LEO MKOANI KATAVI IMELETA MADHARA

Na.Issack Gerald Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Katavi zimesababisha madhara katika makazi ya wakazi wa Mtaa wa Misunkumilo uliopo Manispaa ya Mpanda ukiwemo uharibifu wa miundombinu. Baadhi ya wananchi ambao makazi yao yameharibiwa ikiwemo kufa kwa mifugo kutokana na maji kukosa mwelekeo hali inayosababishwa na kutokuwepo kwa mitaro ya maji wameiomba serikali ichukue hatua. Kwa upande wa Mwenyekiti wa mtaa huo BW Katabi Jona ameutaka uongozi wa Manispaa kuichukulia hatua Kandarasi iliyo husika na ujenzi wa barabara za mtaa huo bila kuweka mitaro. Haya yana jili ikiwa ni siku moja tu tangu mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA kutoa tahadhari juu ya uwepo wa Mvua kubwa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WAZIRI JAFO AMTUMBUA MKURUGENZI MKOANI RUKWA

Na.Issack Gerald Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI Mh.Suleiman Jafo,amemsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Bw.Julius Kaondo. Waziri Jafo katika kikao na Waandishi wa habari,amesema amemsimamisha Bw.Kaondo kutokana na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na kushindwa kusimamia mradi wa maji. Kufuatia hatua hiyo,Waziri Jafo ametoa agizo k wa wakurugenzi watendaji na watumishi wa umma kutojihusisha na vitendo vya rushwa na amewataka wasimamie wajibu wao kama inavyotakiwa katika kutekeleza majukumu anayotakiwa kuyatekeleza kwa mjibu wa miongozo ya nchi. Jafo amesema amechukua hatua hiyo kwa kuzingatia vifungu vya sheria za nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwezi uliopita Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Bukoba na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba walifukuzwa kazi na Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli kwa kushindwa kujibu maswali yake akitaka kujua kiwango cha fed

WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI BADO WANAKABILIWA NA KITISHO CHA HAKI ZAO KUTOPATIWA KIPAUMBELE

Na.Issack Gerald Imebainika watu wenye ulemavu Mkoani Katavi bado wanakabiliwa na kitisho cha haki zao za msingi kutopati wa kipaumbele na hivyo kuchochea unyanyapaa kuendelea kuwa mkubwa dhidi ya makundi hayo. Hayo yamebainishwa leo katika kikao cha kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa wadau wa kupinga ukatiri dhidi ya watu wenye ulemavu na kujadili namna matatizo ya watu wenye ulemavu yanashghulikiwa. Kwa upande wa mratibu wa mradi wa elimu jumuishi Mikoa ya Rukwa na Katavi Bi.Veronica Mavanza pamoja na mratibu wa mradi huo Mkoani Katavi Raphael Fortunatus,wameahidi kuzifanyia kazi changamoto zinazowakumba watu wenye ulemavu katika Mkoa ya Rukwa na Katavi. Mkurugenzi wa Shirika la International Aid Service(IAS) kutoka nchini Denmark Bw.Torben Madsen mara baada ya kikao cha leo,amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu hasa katika sekta ya elimu. Makundi ya Mtandao wa wazazi wenye ulem

RAIS MAGUFULI ATANGAZA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 8157 IMO FAMILIA YA BABU SEYA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli ametangaza msamaha kwa wafungwa 8,157 huku wanaotakiwa kutolewa siku ya leo wakiwa ni 1,828. Papii Kocha na Nguza Viking Rais ametoa msamaha huo leo wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Uhuru wa Tanganyika Mjini Dodoma Leo. Rais Magufuli amesema amezingatia ibara ya 45 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayompatia rais mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa . Miongoni mwa waliotangaziwa kusamehewa ni pamoja na Nguza Viking anayefahamika pia kwa jina la Babu Seya na mwanae Papii Kocha waachiwe huru kuanzia leo. Wakati huo huo wafungwa 61 waliotakiwa kunyongwa hadi kufa wamesamehewa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED