Posts

Showing posts from November 20, 2017

HABARI ZA HIVI PUNDE KUTOKA IKULU

Image
Serikali imekanusha taarifa zinazoenezwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt.Laurian Ndumbaro. Kwa mjibu wa taarifa ambayo imetolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ikulu ya rais Bw.Gerson Msigwa amesema taaifa hizo  sio za kweli  na  zipuuzwe . Taarifa hiyo inaeataka wananchi kuendelea kupokea taarifa rasmi kutoka kwenye mamlaka na vyombo rasmi vya Serikali. Wakati huo huo watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekumbushwa kumbushwa kuwa kueneza taarifa za uongo ni makosa kisheria. Hata hivyo,Serikali imesema itawafuatilia wote waliozusha taarifa hizi na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WANAHARAKATI WAMETAKA SHERIA ZINAZOHUSU WATU WENYE ULEMAVU ZIWE HAI

Image
Na.Issack Gerald-Mpanda Wanaharakati wa kutetea haki za watu wenye ulemavu wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wameiomba serikali kusimamia kanuni na sheria za nchi zinazotetea haki za watu wenye ulemavu kama zilivyoainishwa katika katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Wanaharakati hao wakiwemo mtandao wa wazazi,Shivyawata, wajumbe wa baraza la watoto wilayani Mpanda na kamati ya kulea baraza la watoto wenye ulemavu,wametoa kauli hiyo leo katika kikao cha kujadili haki za watoto wenye ulemavu kikao ambacho kimefanyika mjini Mpanda. Kwa upande wake mratibu wa mradi wa Elimu Jumuishi Mkoani Katavi Bw.Raphael  Fortunatus Jumbe pamoja na mambo mengine amesema semina ya leo inalenga kufikisha elimu kwa wanaharakati ili washiriki kupaza sauti katika kutetea haki za watu wenye ulemavu pamoja na kuwafichua watoto waluiofichwa majumbani. Kwa mjibu wa vifungu vya sheria ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mawaziri katika wizara husika wanatakiwa kusimamia misingi yote inayompa