WANAHARAKATI WAMETAKA SHERIA ZINAZOHUSU WATU WENYE ULEMAVU ZIWE HAI

Na.Issack Gerald-Mpanda
Wanaharakati wa kutetea haki za watu wenye ulemavu wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wameiomba serikali kusimamia kanuni na sheria za nchi zinazotetea haki za watu wenye ulemavu kama zilivyoainishwa katika katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Wanaharakati hao wakiwemo mtandao wa wazazi,Shivyawata, wajumbe wa baraza la watoto wilayani Mpanda na kamati ya kulea baraza la watoto wenye ulemavu,wametoa kauli hiyo leo katika kikao cha kujadili haki za watoto wenye ulemavu kikao ambacho kimefanyika mjini Mpanda.
Kwa upande wake mratibu wa mradi wa Elimu Jumuishi Mkoani Katavi Bw.Raphael  Fortunatus Jumbe pamoja na mambo mengine amesema semina ya leo inalenga kufikisha elimu kwa wanaharakati ili washiriki kupaza sauti katika kutetea haki za watu wenye ulemavu pamoja na kuwafichua watoto waluiofichwa majumbani.
Kwa mjibu wa vifungu vya sheria ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mawaziri katika wizara husika wanatakiwa kusimamia misingi yote inayompa haki za msingi mtu mwenye ulemavu anapohitaji kuhudumiwa bila ubaguzi.
Naye mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Mkoani Katavi SHIVYAWATA Bw.Issack Lucas Mlela ambaye pia ni mjumbe wa katamati ya kulea baraza la watoto wenye ulemavu pamoja na mambo mengine amesema sheria namba 9 ya mwaka 2010 inasimamia haki za watu wenye ulemavu huku akisema wakati mwingine unyanyapaa nao unaanzia kwa ndugu wenyewe kumnyanyapaa mwenye ulemavu suala ambalo halikubaliki na halifai kuigwa na jamii.
Baadhi ya ibara zilizopo katika katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 ambazo zinazotakiwa zisimamiwe vizuri ili watu wenye ulemavu wapate haki zao ni pamoja na ibara ya 4,20,26,27,28,31,32 na 34 ambavyo vinaitaka serikali ya Tanzania kutekeleza haki zote za msingi kwa watu wenye ulemavu katika Nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya afya,elimu,ajira na haki nyingine za kibinadamu.
Licha ya ibara hizo pia Tanzania ni miongoni mwa nchi za jumuiya ya madola ambazo zilisaini mikataba mbalimbali kwa ajili ya kusimamia na kutekeleza haki za watu wenye ulemavu.
Katika kipindi cha mwaka 2014 mpaka 2016 jumla ya watu wenye ulemavu 83 wakiwemo watoto wenye umri wa kwenda shule wametetewa na mradi wa elimu jumuishi wilayani Mpanda na kupatiwa haki zao muhimu kama elimu.
Harakati za kutetea,kuibua na kuwezesha haki za watu wenye ulemavu hasa watoto Mkoani Katavi limekuwa likiendshwa na shirika la kimataifa la IFI linaloundwa na washirika 3 ambao ni Free Pentecostal Church Of Tanzania(FPCT),International centre on Disabilities(ICD) na International Aid Services(IAS) ambapo kwa hapa nchini mradi wa elimu Jumuishi upo katika mikoa ya Rukwa na Katavi pekee kati ya mikoa yote ya Tanzania bara.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA