Posts

Showing posts from April 10, 2018

AJALI YA TRENI KATAVI

Image
Mabehewa 4 ya Treni ya mizigo ambayo ilikuwa ikisafiri kutoka Wilayani Mpanda Mkoani Mpanda Katavi kuelekea Tabora yameacha njia na kuanguka. Afisa Uhusiano Shirika la Reli  Mohamed Mapondela  amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema mabehewa hayo yameangukia katika eneo la Shankala mkoani Katavi. Amesema hakuna mtu aliyejeruhiwa wala uharibifu wa mali na kinachoendelea kwa sasa kutoa mizigo na kuweka sawa njia ya treni ili kuruhusu safari ziendelee kama kawaida. Kwa upande mwingine Bw.Mapondela hakueleza sababu hasa zilizosababisha ajali hiyo kutokea lakini amesema huenda   ikawa imechangiwa na uchakavu wa njia hiyo ya treni. Reli hiyo inayotajwa kuwa ni miongoni mwa reli kongwe zilizojengwa nchini enzi za ukoloni miongo kadhaa iliyopita.   Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com

MKOANI KATAVI AHUKUMIWA JELA KWA KUMILIKI RISASI ZA SILAHA YA KIVITA

Image
Mahakama ya wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imetoa hukumu dhidi ya Bw.Kigalu Huba(25) mkazi wa kijiji cha Kambuzi wilayani Mpanda Mkoani Katavi aliyekuwa akituhumiwa kwa kosa la kukutwa na risasi 12 za silaha AK-47 ya kivita ambapo mahakama hiyo imemuhukumu kwenda jela miaka 20. Hakimu mkazi wa mahakama   hiyo Mh.Chiganga Tengwa akitoa hukumu hiyo leo amesema mahakama imejiridhisha bila kuacha shaka kuwa alitenda kosa hilo baada ya kusikiliza shadi wa pande zote ambazo ni mtuhumiwa na upande wa Jamhuri ambao ni serikali. Awali upande wa Jamhuri ambayo ni serikali wamesema Bw. Kigalu Huba   alikutwa na risasi hizo Machi 19,2018 ambapo ni kinyume na kifungu cha sheria namba 7 ya mwaka 2015 kinachohusu umiliki wa silaha   huku wakiiomba Mahakam itowe adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe wenye tabia kama hiyo. Kwa upande wake Bw.Huba akitoa utetezi wake mahakamani hapo ameiomba mahakama kumpunguzia adhabu aliyopewa akisema kuwa anategewa ana mke na watoto watatu na asipopunguziwa adhab