AJALI YA TRENI KATAVI


Mabehewa 4 ya Treni ya mizigo ambayo ilikuwa ikisafiri kutoka Wilayani Mpanda Mkoani Mpanda Katavi kuelekea Tabora yameacha njia na kuanguka.
Afisa Uhusiano Shirika la Reli Mohamed Mapondela amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema mabehewa hayo yameangukia katika eneo la Shankala mkoani Katavi.
Amesema hakuna mtu aliyejeruhiwa wala uharibifu wa mali na kinachoendelea kwa sasa kutoa mizigo na kuweka sawa njia ya treni ili kuruhusu safari ziendelee kama kawaida.
Kwa upande mwingine Bw.Mapondela hakueleza sababu hasa zilizosababisha ajali hiyo kutokea lakini amesema huenda  ikawa imechangiwa na uchakavu wa njia hiyo ya treni.
Reli hiyo inayotajwa kuwa ni miongoni mwa reli kongwe zilizojengwa nchini enzi za ukoloni miongo kadhaa iliyopita.
 Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA