Posts

Showing posts from April 16, 2018

WASITISHA SAFARI ZA KUSAFIRISHA ABIRIA KATAVI KWENDA MIKOANI

Miongoni wa wafanyabiashara wa usafirishaji abiria mjini Mpanda wamesitisha huduma kutokana na ubovu wa miundombinu. Hayo yamebainishwa na baadhi ya wahudumu wa kampuni za usafirishaji wanaomiliki mabasi ya mikoani ambazo zinatumia barabara inayoanzia Mpanda kuelekea Tabora tabora. Magari yaliyokuwa yakitumia barabara ya Mpanda-Tabora yamepewa utaratibu wa kutumia barabara ya Mpanda-Kigoma au Mpanda-Mbeya ambapo wafanyabiashara wengine wamesema wanalazimika kuongeza nauli kwa shilingi elfu kumi hadi elfu kumi na tano kwa kila safari kwa kuwa umbali wa safari umeongezeka Hata hivyo kwa mjibu wa wasafirishaji hao wamesema barabara mbadala ya kupitia Uvinza Mkoani Kigoma nayo haipo katika hali nzuri kitendo kinachosababisha ugumu wa safari. Jumamosi ya Aprili 16,2018,mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Rafael Muhuga alitangaza kufungwa kwa barabara ya Mpanda-Tabora baada ya barabara hiyo kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Mwishoni mwa wiki iliyopia mku