Posts

Showing posts from December 16, 2017

MKUU WA JESHI TANZANIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA ZAHANATI YA JESHI LA POLISI MKOANI KATAVI

Image
Na.Issack Gerald Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon,ameweka jiwe la msingi ujenzi wa zahanati ya Jeshi la Polisi Mkoani Katavi. Katika taarifa ya Mkuu wa Polisi Wilayani Mpanda Maria Kwayi,amesema mpaka sasa zaidi ya shilingi milioni 7 zimekwishatumika katika ujenzi ambapo inahitajika zaidi ya shilingi milioni 29 ili jengo likamilike huku changamoto ikiwa ni upungufu wa vifaa vya ujenzi. Kwa upande wake IGP sirro mara baada ya kupokea taarifa hiyo amesema jeshi la polisi litaongeza takribani milioni kumi na Tano ili kuunga juhudi za ujenzi wa zahanati hiyo. Wakati huo huo IGP siro aliyehitimisha ziara yake jana Mkoani Katavi amesema,wafanyabiashara Mkoani Katavi,Jeshi la Polisi Mkao makuu na serikali kuu wataangazia hatua za haraka ili zipatikane nyumba kwa ajili ya polisi ili kutatua uhaba wa nyumba za polisi Mkoani Katavi. IGP Simon Sirro alikuwa na ziara ya kikazi siku mbili juzi na jana Mkoani katavi akitokea Mkoani Kigoma kabla ya kuelekea Mkoani Rukwa. Haba

IGP SIRRO AWAOMBA VIONGOZI WA DINI MKOANI RUKWA KUHUBIRI AMANI ILI UHARIFU UPUNGUE

Image
Na.Issack Gerald Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon amewaomba viongozi wa dini mkoani Rukwa Kuongeza bidii katika kuhubiri amani ili mauaji yanayotokayo na imani za kishirikina na mapenzi yapungue mkoani humo.  IGP Sirro ametoa kauli hiyo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua mikakati ya jeshi hilo katika kukabiliana na mauaji mkoani humo. Amesema jeshi la polisi linajitahidi kukabiliana na mauaji yote yanayotokea nchini lakini katika Mkoa wa Rukwa takwimu zinaonesha kuwa mauaji yanayotokana na ushirikina pamoja na  wivu wa mapenzi yanaongoza mkoani humo. Kamanda Sirro amesema viongozi wa dini wana jukumu kubwa kuhakikisha wanahubiri amani ili mauaji hayo yapungue kwani juhudi hizo zinapaswa kuwa za pamoja kwa kuwa nao wana nafasi kubwa la kuwalea wananchi kiroho. Wakati huo huo IGP Sirro ameahidi kuwa Jeshi hilo kupitia bajeti zake litajenga kituo kipya cha polisi cha Sumbawanga mjini kwa kuwa kilichopo ni kichakavu na majengo yanayotumika yal

WAKULIMA WA TUMBAKU MKOANI KATAVI WAILAUMU SERIKALI KUSHINDWA KUTEKELEZA KAULI YAKE

Image
Na.Issack Gerald Wakulima wa zao la tumbaku wa chama cha msingi cha ushirika Mpanda Kati Mkoani Katavi wameilaumu serikali kushindwa kutekeleza agizo lake la kuhakikisha tumbaku iliyo kosa soko inanunuliwa. Wakulima hao  kwa nyakati tofauti wamesema mpaka sasa hawajui hatima ya ununuzi wa tumbaku yao huku wengine wakisema wameathirika kiuchumi na maisha kwa ujumla. Hivi karibuni,mwenyekiti chama cha msingi cha Ushirika Mpanda Kati Bw.Sosipeter Salvatory ,alisema kuna kiasi cha kilo  elfu ishirini na mbili ambazo hazijanunuliwa kati ya kiasi chote cha tumbaku iliyozalishwa katika msimu wa mwaka  mwaka 2016/2017. Mnamo Novemba 17 mwaka huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiahirisha vikao vya Bunge mjini Dodoma alieleza kuwepo kwa kampuni itakayo nunua Tumbaku iliyosalia pamoja na Mbaazi.   Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED