WAKULIMA WA TUMBAKU MKOANI KATAVI WAILAUMU SERIKALI KUSHINDWA KUTEKELEZA KAULI YAKE

Na.Issack Gerald

Wakulima wa zao la tumbaku wa chama cha msingi cha ushirika Mpanda Kati Mkoani Katavi wameilaumu serikali kushindwa kutekeleza agizo lake la kuhakikisha tumbaku iliyo kosa soko inanunuliwa.

Wakulima hao  kwa nyakati tofauti wamesema mpaka sasa hawajui hatima ya ununuzi wa tumbaku yao huku wengine wakisema wameathirika kiuchumi na maisha kwa ujumla.
Hivi karibuni,mwenyekiti chama cha msingi cha Ushirika Mpanda Kati Bw.Sosipeter Salvatory ,alisema kuna kiasi cha kilo  elfu ishirini na mbili ambazo hazijanunuliwa kati ya kiasi chote cha tumbaku iliyozalishwa katika msimu wa mwaka  mwaka 2016/2017.
Mnamo Novemba 17 mwaka huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiahirisha vikao vya Bunge mjini Dodoma alieleza kuwepo kwa kampuni itakayo nunua Tumbaku iliyosalia pamoja na Mbaazi. 
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA