Posts

Showing posts from July, 2015

WATUMISHI WA UMMA MPANDA WATAKIWA KUTOJIHUSISHA NA SIASA WAKATI WA KAZI

Image
Watumishi wa umma wakiwa katika Ukumbi wa shule ya Sekondari St.Mary's Mpanda katika semina iliyoendeshwa na Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Mpanda Vicenti Kayombo Watumishi mbalimbali katika manispaa ya Mpandaa katika Semian ukumbi wa Shule ya Sekondari St.Mary's Manispaa ya Mpanda katika kikao cha utum,ishi wa umma kikendeshwa Kaimu Mkurugenzi Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda Vicenti Kayombo Na. Mark Ngumba-MPANDA WATUMISHI Wa Umma wametakiwa Kutojihusisha na Maswala ya Siasa wakati wa Kazi na badala yake wahakikishe wanatimiza wajibu wao wa  Kuwahudumia wananchi Katika Maeneo yao ya Kazi.

JESHI LA POLISI KATAVI LAWATAKA WANANCHI KUWA MAKINI MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU BVR

Na.Mark Ngumba-MPANDA JESHI La polisi Mkoani Katavi limewataka wananchi Kuwa Makini na Ujumbe unaosambazwa  Katika Mitandao  ya Simu kwa Madai ya Kuhakiki taarifa za watu waliojiandikisha Kupiga kura Kwa Kutumia mashine za Kimtandao BVR.

OFISI ZA MFUKO WA BIMA YA AFYA NHIF ZAFUNGULIWA KATAVI

Image
  Na.Issack Gerald-Katavi Wanachama wa Mfuko wa hifadhi ya afya ya jamii NHIF  Mkoani Katavi wanatarajia kunufaika na  huduma hiyo itakayo kuwa ikitolewa Mkoani hapa badala ya Sumbawanga Mkoani Rukwa kama  ilivyokuwa awali.

JARIBIO LA KUUA KWA IMANI ZA USHIRIKINA WATU SITA WASHIKILIWA

 Na.Issack Gerald-Katavi Watu sita wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Katavi kwa tuhuma za kutaka kuvamia na kufanya mauaji ya watu wanaodhaniwa kuwa ni wachawi.

UWT KATAVI WAFANYA UTEUZI WA WAGOMBEA UBUNGE VITI MAALUMU

Na.Issack Gerald-Katavi MKUTANO Wa umoja wa wanawake wa CCM (UWT)Mkoani Katavi   umewateua Taska Restituta Mbogo na Anna Richad Lupembe   kuwa Wagombea wa nafasi ya Ubunge Vitimaalum kwa Mkoa wa Katavi.

MTOTO ATUPWA NA KUCHOMWA MOTO- KATAVI

NA.Meshack Ngumba-Mpanda MTOTO anayekadiliwa kuwa na umri wa Miezi 6 hadi 7 ametupwa na Kisha kuchomwa  moto Usiku wa Kuamkia Leo  Katika Mtaa wa Maridadi Kata ya kashaulili Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.

SAKATA LA WATU KULA VYAKULA WAKIWA KWENYE VYANDARUA,MKURUGENZI MANISPAA YA MPANDA ANG'AKA WAKAZI KUTUPA TAKA SEHEMU ZILIZOZUIWA

Na.Issack Gerald-Katavi Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Suleiman Lukanga amesema eneo linalolalamikiwa na wakazi wa Mtaa wa Kashaulili kutumika kama Dampo la kutupa taka na kusababisha Nzi kuzagaa katika makazi yao lilishapigwa marufuku.

MWENYEKITI WA MTAA MANISPAA YA MPANDA AZUSHIWA KUJIDHURU,MTUHUMIWA AKANA KUHUSIKA

 NA.Issack Gerald-Katavi Mwenyekiti wa Mtaa wa Kachoma uliopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Mwarabu Kestokecha amewalalamimkia baadhi ya watu akiwemo aliyekuwa diwani wa kata ya Makanyagio katika Manispaa hiyo Iddi Nziguye kwa kusambaza taarifa za kupotosha wananchi kuwa amejiudhuru uenyekiti wa mtaa huo.

WALAZIMIKA KULA VYAKULA WAKIWA NDANI YA NETI WAKIWAKIMBIA NZI

Image
Moja ya madampo ya taka yanayotoa taka Mpanda mtaa wa Kashaulili NA.Meshack Ngumba-Katavi WAKAZI wa Mtaa wa Kashaulili  Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi hulazimika Kula chakula wakiwa ndani ya Neti kutokana na eneo hilo kuwa na inzi wengi.

MPANDA GIZA NENE SUAL LA UMEME,TANESCO YASEMA UMEME KUTENGAMAA MIEZI MITATU IJAYO

Image
  Mafundi wakiwa katika matengenezo ya mitambo ya Tanesco Mpanda  NA.Issack Gerald-Mpanda Katavi SHUGHULI Za Uchumi Mkoani Katavi zimesimama kwa siku sita sasa Kutokana na Kukosekana kwa nishati ya Umeme.

KATAVI KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA MIPAKA YAKE YA UTAWALA

Na.Issack Gerald-Katvi SERIKALI Mkoani Katavi imedhamilia Kumaliza Migogoro ya Aridhi kwa Kuweka utaratibu Utakaoishirikisha Jamii ambayo ndiyo huathiriwa Zaidi na Migogoro hiyo pale inapokuwa imetokea.

WAZIRI MKUU PINDA AKATAA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KATAVI,AWAACHIA WENGINE KUCHUKUA JIMBO HILO

Image
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda NA.Issack Gerald-Mlele Katavi WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekataa ombi la wananchi wa jimbo lake la uchaguzi la kumtaka agombee tena ubunge katika jimbo hilo ili kuendeleza mipango mbalimbali ya maendeleo aliyoianzisha.

KATIBU MWENEZI CHADEMA RUKWA NA KATAVI AHAMIA CCM

NA.Issack Gerald-Katavi Aliyekuwa Katibu mwenezi kupitia chama cha Demkrasia na Maendeleo Mikoa ya Rukwa na Katavi John Matongo ametangaza rasmi kujiondoa katika chama hicho na kujiunga na Chama cha Mpainduzi CCM.

WATOTO KATAVI WATAKIWA KULELEWA MAADILI YA KUITUMIKIA TANZANIA

Image
Waislam katika sgerehe za Eid Elfitri Mjini Mpanda Wa nne kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi akishiriki Ibada ya Eid Elfitri Msikiti Mkuu wa Ijumaa Mjini Mpanda NA.Issack Gerald-Katavi Jamii Mkoani Katavi imetakiwa kuwalea watoto wao katika maadili mema ili kuwatumikia watanzania katika utumishi wa umma wanapokuwa wakubwa.

MIL.40 KUOKOA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI IGALULA WANAOSOMEA NJE WILAYANI MPANDA

Image
Wanafunzi Shule ya Msibgi Igalula chini ya Mti wakitumia mti huo kama darasa Juma Khatibu Chum akizindua vyumba vya madarasa Shule ya Msini Igalula ilyopo Wilayani Mpanda Wanafunzi wa Chekechea Igalula Wilayani Mpanda wakiwa darasani NA.Theressia Lwanji- Katavi Ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Igalula unatarajia kupunguza adha ya uhaba wa madarasa katika shule hiyo na kuondoa adha hiyo inayowapata wanafunzi shuleni hapo.

JESHI LA POLISI KATAVI LAWAONYA WATAKAOSABABISHA UVUNJFU WA AMANI SHEREHE ZA EID EL FITR

Image
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi Dhahir Athman Kidavashari akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) akizungumzia suala la kudumisha amani Mkoani Katavi  JESHI La Polisi Mkoani Katavi limetoa tahadhari kwa watu kutojihusisha na Vitendo vya Uvunjifu wa amani wakati wa Sherehe za Eid el Fitr inayoadhimishwa leo hapa nchini Tanzania.

YATIMA MPANDA WAPATA MSAADA,CHANGAMOTO YA FEDHA HALMSHAURI YA WILAYA YASEMA BADO KIKWAZO KUWASAIDIA YATIMA WENGI

Image
Baadhi ya watoto katika picha ambao wamepatiwa msaada Yatima wakisalimiwa na kupew zawadi ndogondogo NA.Theressia Lwaji-MPANDA KATAVI WATOTO yatima 12 kati 32  katika kijiji cha ifukutwa kata ya mpanda ndogo wa halmashauri ya wilaya ya mpanda mkoani katavi  wamepatiwa misaada ya magodoro,vyandarua na blanket.

JAMII HALMSHAURI YA WILAYA NSIMBO YATAKIWA KUWA KARIBU NA WATOTO KATIKA MALEZI

Image
Baadhi ya viongozi katika Msafara wa mwenge wa Uhuru  wakizuru mandari ya Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo wakati mwenge wa uhuru ulipofika katika halmshauri hiyo NA.Issack Gerald-Nsimbo Katavi Jamii katika Halmashauri ya Wilaya  ya  Nsimbo Mkoani Katavi imetakiwa kuwa na ukaribu kimalezi kwa  watoto wao ili kubaini kwa haraka vitendo vya ukatili wakati vinapotokea kwa watoto.

MGOMO DARADARA MPANDA NAULI KUPUNGUZWA,SUMATRA YASEMA WASIOTAKA NAULI ILIYOPANGWA NA SUMATRA WAPAKI MAGARI

Image
Baadhi ya daradara mjini Mpanda zikiwa zimepaki baada ya madereva  kusitisha safari  Na.Issack Gerald-Katavi Madereva wa daradara zinazosafirisha abiria kutoka Mpanda Mjini kuelekea kata ya Kakese leo wamegoma na kumlalamikia Meneja wa mamlaka ya uasafiri wa majini na nchi kavu Sumatra Mkoani Katavi kwa kushusha viwango vya nauli.

KIONGOZI MBIO ZA MWENGE MPANDA - ACHENI KUTOA NA KUPOKEA RUSHWA KUPATA VIONGOZI BORA

Image
Na.Issack Gerald-Katavi JAMII mkoani Katavi imetakiwa kuwafichua wagombea wanaotoa rushwa kupata uongozi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba mwaka huu, ili wapatikane viongozi bora watakaojali maslahi yao.

MKUU WA MKOA WA KATAVI AFUTURISHA,MAMIA KADA MBALIMBALI ALIOWAARIKA WAHUDHURIA AWAASA KUDUMISHA AMANI

Image
Mkuu wa Mkoa akizungumza na kada mbalimbali aliowaarika kushiriki kwa pamoja katika Ikulu ndogo Mjini Mpanda Mkuu wa Mkoa katikakti wakifuturu Mkuu wa Mkoa wa Katavi wa NNE kutoka kulia katika picha wakiswali  Na.Issack Gerald-Katavi MKUU wa Mkoa wa Katavi Dk. Ibrahim Hamisi Msengi amesisitiza kuwepo kwa amani, upendo na ushirikiano na kusema kuwa  ni fursa nzuri kwa watu kufanya shughuli za maendeleo.

WANANCHI WILAYANI MLELE WATAKIWA KUFICHUA WANAOFANYA VITENDO VYA UKATIRI

Image
Katikati ni mkuu wa Wilaya ya Mlele Issa Njiku akifafanua jambo NA.Issack Gerald-Mlele Wakazi kata ya Kibaoni Wilayani Mlele Mkoani Katavi wametakiwa kushirikiana na vyombo vya dora kutoa taarifa za vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.

WALIMU WAPYA MPANDA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA WELEDI,KUTOJIHUSISHA NA ANASA KAZINI

Image
Walimu wapya wakiwa katika warsha ya pamoja na maafisa elimu mjini Mpanda Na.Amosi Venance-Mpanda Katavi WALIMU wa sekondari wilayani Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuwa na maadili na kufuata weledi katika utendaji kazi ili kuboresha kiwango cha elimu mkoani Katavi.

ZAIDI YA MILIONI TANO ZATUMIKA KUNUNUA VIFAA MAABARA NSIMBO ,WAZAZI WATAKIWA KUTOWAZUIA WATOTO KUSOMA SAYANSI

Image
  Moja ya vyumba vya maabara Shule ya Sekondari Machimboni Na.Issack Gerald -Nsimbo Katavi Wazazi na walezi katika Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi   wametakiwa kutowazuia watoto wao kupata fursa ya elimu.

KATAVI YATANGAZA VITA DHIDI YA MAUAJI YA WATU WENYE UALBINO TENA

Image
Remi  Luchumi(30) mkazi wa Mwamachoma   Tarafa ya Mamba Wilaya ya Mlele akiwa hospitali ya Wilaya ya Mpanda baada ya kukatwa mkono mwezi juni mwaka huu Na.Issack Gerald-Katavi HALMASHAURI ya wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeweka mikakati ya kukomesha mauaji dhdi ya watu wenye albino.

WAGOMA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO MPAKA WASOMEWE MAPATO NA MATUMIZI

Image
NA.Issack Gerald-Nsimbo Katavi Wakazi wa kijiji cha Magamba kilichopo kata ya Magamba Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi wamesema hawatashiriki shughuli mbalimbali za maendeleo zikiwemo  za ufyatuaji tofali za kijiji ikiwa hawatasomewa taarifa ya mapato na matumizi iliyo sahihi.

MTOTO MIAKA 17 AFA MAJI MPANDA

Image
Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi MTOTO aliyefahamika kwa jina la Stanslaus Christopher mwenye umri wa miaka (17) Mkazi wa Mtaa wa Mpadeco Kata ya Makanyagio Wilayani Mpanda Mkoani Katavi, amekufa maji baada ya kutumbukia mtoni katika daraja la Kachoma.

RAIS KIKWETE AVUNJA BUNGE,AELEZA MAFANIKIO NA CHANGAMOTO KIPINDI CHA UONGOZI WAKE

Image
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania hii leo amehutubia rasmi bunge la 10 la nchi hiyo na kulivunja rasmi.

WALEMAVU MPANDA WAOMBA MAADHIMISHO KUFANYIKA NGAZI YA HALMASHAURI

Image
NA.Issack Gerald-Mpanda Katavi Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imesema inasubiri mwongozo wa serikali kuu ya Mkoa wa Katavi ili kuona kama kuna uwezekano wa kuandaa maadhimisho siku ya walemavu duniani mwaka huu.

NSIMBO YAANZA MAANDALIZI SIKUKUU ZA NANENANE KITAIFA,UWANJA UTAKAOTUMIA WAWA CHANGAMOTO

Image
Na.Issack Gerald-Nsimbo,Katavi Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi imeanza maandalizi ya sikukuu ya Wakulima nane nane huku ikikabiliwa na changamoto ya uwanja kwa ajili ya maadhimisho hayo.

BALAZA LA MADIWANI MPANDA MJI LAMALIZA MUDA WAKE,KAMATI YA UKIMWI YAONGOZA MAPAMBANO YA UKIMWI

Image
Na.Alinanuswe Edward-Mpanda Katavi BARAZA La Madiwani Katika halmashauri ya Mji wa Mpanda jana limemaliza Muda wake wa Kipindi cha Miaka mitano ya kuwa madarakani.

WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMA YA WILAYA MPANDA KWA VITENDO VYA RUSHWA

Na.Theressia Lwanji-Mpanda Katavi WATU Wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa kosa la  Kujihusisha na Vitendo Vya kutoa na Kupokea Rushwa Kinyume cha Sheria.

USALAMA KAMBI YA WAKIMBIZI KATUMBA RAIA WAPYA TANZANIA YAENDELEA KUIMARIKA

Image
Na.Issack Gerald-Nsimbo Katavi HALI YA USALAMA imeendelea   kuimarishwa zaidi katika kambi ya wakimbizi ya Katumba iliyopo Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi.

BALAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO MKOANI KATAVI LAVUNJWA

Image
  Na.Issack Gerald-Nsimbo,Katavi BARAZA la Madiwani Katika halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi  limevunjwa jana kwa Mjibu wa kanuni za baraza hilo ambalo humaliza muda wake wa kuwa   madarakani Kila baada ya Kipindi cha Miaka mitano.

ASKARI 15 KATAVI WATUNUKIWA VYETI VYA HESHIMA POLICE FAMILY DAY,WAPANGA MIKAKATI YA KUKOMESHA UHARIFU

Na.Lutakilwa-Lutobeka-Katavi MAAFISA 15 wa jeshi la polisi mkoani Katavi wametunukiwa vyeti maalum vya utendaji kazi katika maadhimisho ya siku ya polisi yaliyofanyika leo mjini Mpanda.

NSIMBO YAKUBALI KUJENGA SEKONDARI URUWIRA

Image
Na Alinanuswe  Edward Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi imeridhia kuanza ujenzi wa shule ya sekondari ya kata katika kata ya Uruwira