JESHI LA POLISI KATAVI LAWAONYA WATAKAOSABABISHA UVUNJFU WA AMANI SHEREHE ZA EID EL FITR

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi Dhahir Athman Kidavashari akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) akizungumzia suala la kudumisha amani Mkoani Katavi 

JESHI La Polisi Mkoani Katavi limetoa tahadhari kwa watu kutojihusisha na Vitendo vya Uvunjifu wa amani wakati wa Sherehe za Eid el Fitr inayoadhimishwa leo hapa nchini Tanzania.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa  kwa vyombo vya habari imesema Uzoefu unaonesha kuwa kipindi cha Sherehe kama hizi hukumbwa na Matukio mbalimbali na hivyo kuwataka wananchi kuwa Makini na Kuchukua tahadhari ya Kuhakikisha usalama wa nyumba zao.

Miongoni mwa matukio ambayo hujitokeza nyakati kama hizi ni Wizi,ulevi wa Kupindukia na Ubakaji ambapo Jeshi la polisi limejipanga Kukabiliana na Mtu au Kikundi kitakacho husika Kuvunja Sheria ya Nchi.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA