Posts

Showing posts from May 29, 2018

NKASI KINARA WA MIMBA KWA WANAFUNZI MKOANI RUKWA

Afisa serikali za mitaa mkoani Rukwa Bw.Albinus Mgonya amesema halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani humo ndiyo inayoongoza kwa wanafunzi kupata ujauzito mkoani Rukwa. Mgonya amebainisha hali hiyo kupitia kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika juzi katika halmashauri hiyo. Katika kipindi cha miezi tisa jumla ya wanafunzi 74 wamekatiza masomo kutokana na kupata ujauzito ambapo kwa mjibu wa katika takwimu hiyo,wanafunzi 36 ni wanafunzi wa shule za msingi na wanafunzi 38 wa sekondari waliopata ujauzito huo kuanzia Julai mwaka jana mpaka Aprili mwaka huu. Alisema kulingana na takwimu hizo,wanafunzi wanaopata ujauzito ni sawa na kuwa kila mwezi wanafunzi   wanne wa shule za msingi   wanapata ujauzito sambamba na wanne wa sekondari wanapata ujauzito. Kutokana na hali hiyo,Mgonya ameiagiza halmashauri ya wilaya Nkasi kuandaa taarifa itakayoainisha idadi ya Watoto wenye mimba,mahali walipo wazazi   wao ikiwa ni pamoja na viongozi wa maeneo yao hasa Watendaji wao wa vijiji na kata

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

Image
Abdulrahman Kinana alizaliwa mwaka 1952 mkoani Arusha Arusha Kaskazini mwa Tanzania. Kinana ni mwanasiasa aliyeshika nyadhifa mbalimbali serikalini. Alihitimu shahada yake katika Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani akibobea kwenye masuala ya mikakati. Alikuwa Waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga taifa ,naibu Waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimatafa na Waziri wa ulinzi. Kinana aliwahi kufanya kazi na Jeshi la wananchi la Tanzania kwa miaka 20 kabla ya kusaafu akiwa na cheo cha ukanali mwaka 1972. Abdulrahman Kinana pia aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Afrika mashariki mwaka 2001 mpaka mwaka 2006. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WAKAZI WILAYANI TANGANYIKA WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU

Kaimu   Afisa wa Afya wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Bw.Philipo Mihayo amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugojwa wa kipindupindu kwa kufanya usafi wa   chakula na mazingira yote yanayowazunguka. Bw.Mihayo amesema ni vema   kuchukua tahadhari kwani mikoa jirani ya Rukwa na kigoma inaripotiwa kukubwa kadhia hiyo. Aidha Mihayo ametoa wito kwa wananchi kuchimba vyoo vya kisasa lakini pia kuhakikisha wanatumia maji safi na salama huku wanaokadi maelekezo akisema watachukuliwa hatua. Wilaya jirani ya Sumbawanga iliyopo Mkoani Rukwa ilitangaza kuwa katika kipindi cha Mei 11 mpaka 24 watu 7 walikuwa wamefariki dunia huku wengine 166 wakiugua ugonjwa wa kipindupindu na 44 mpaka kufikia Mei 25 walikuwa wakiendelea kupatiwa matibabu. Kipindupindu husababishwa na bakteria aina ya  Vibrio cholerae  zinazosababisha kuhara majimaji yenye rangi kama maji ya kupikia  mchele ambapo bakteria hao walitambuliwa mwaka  1854  . Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

BARABARA YA MPANDA-TABORA SASA RUKSA KWA MAGARI YOTE

Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mhuga hatimaye ametangaza rasmi kuwa magari yote makubwa kwa madogo yanaruhusiwa kusafiri kwa kutumia barabara ya Mpanda --Tabora kupitia Mto Koga wilayani Mlele Mei 30,2018. Kwa mjibu wa Bw.Aman   Mwakalebela ambaye ni Afisa Mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu SUMTRA amesema hali ya barabara hiyo ni nzuri na inaruhusu magari ya aina zote kupita. Hata hivyo Mwakalebela amewataka abiria waliotoa nauli ya mzunguko wa barabara kupitia Kigoma au Mbeya kwa ajili ya kwenda Tabora kudai kurejeshewa kiasi cha   nauli iliyozidi kiwango cha fedha kutoka Mpanda-Tabora na kusafiri kwa gharama halisi. Mei 26 mwaka huu Mkuu wa mkoa wa katavi Meja Jenerali Mstaafu Rapahael Muhuga alitangaza kuruhusu magari yasiyozidi tani 3 huku ukarabati wa barabara hiyo ukiendelea. Aprili 14 mwaka huu,Muhuga alitanagaza kuifunga barabara hiyo kutokana na kujaa maji katika daraja la mto koga hali iliyokuwa ikihatarisha usal

WASAINI MKATABA ILI KUANZA UJENZI HOSPITALI YA MKOA WA KATAVI

Serikali ya Mkoa wa Katavi na Shirika la uzalishaji mali la jeshi la kujenga taifa SUMA JKT wamelitiana saini mkataba kwa ajili ya kuanza ujenzi wa ghorofa moja la hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Katavi. Kaimu katibu tawala Bw.Wilbrod Malandu akizungumza wakati wa kutiliana saini hiyo ofisini kwake,amesema Bodi ya Zabuni imemtunuku zabuni SUMA JKT kutekeleza ujenzi wa ghorofa hilo kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 9 na milioni 798.76 ambapo ghorofa hilo litakuwa na vitanda 76 kwa safu ya chini na 71 kwa safu ya juu. Aidha Malandu amesema eneo la ujenzi wa Hospitali hiyo lenye ukubwa wa ekari 243 linapatikana Kata ya Kazima ambapo zaidi ya shilingi milioni 468 zimetumika kuwalipa fidia kwa watu 108 ili kupisha ujenzi huku zaidi ya shilingi milioni 722 zikilipwa kwa mshauri mwelekezi   Y and P Architects Tanzania Limited aliyetekeleza taarifa mbalimblai ikiwemo upembuzi yakinifu,andiko la mradi na uainishaji wa athari za kijamii na mazingira. Kwa upande wake Naibu Mkurugenz