NKASI KINARA WA MIMBA KWA WANAFUNZI MKOANI RUKWA

Afisa serikali za mitaa mkoani Rukwa Bw.Albinus Mgonya amesema halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani humo ndiyo inayoongoza kwa wanafunzi kupata ujauzito mkoani Rukwa.
Mgonya amebainisha hali hiyo kupitia kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika juzi katika halmashauri hiyo.
Katika kipindi cha miezi tisa jumla ya wanafunzi 74 wamekatiza masomo kutokana na kupata ujauzito ambapo kwa mjibu wa katika takwimu hiyo,wanafunzi 36 ni wanafunzi wa shule za msingi na wanafunzi 38 wa sekondari waliopata ujauzito huo kuanzia Julai mwaka jana mpaka Aprili mwaka huu.
Alisema kulingana na takwimu hizo,wanafunzi wanaopata ujauzito ni sawa na kuwa kila mwezi wanafunzi  wanne wa shule za msingi  wanapata ujauzito sambamba na wanne wa sekondari wanapata ujauzito.
Kutokana na hali hiyo,Mgonya ameiagiza halmashauri ya wilaya Nkasi kuandaa taarifa itakayoainisha idadi ya Watoto wenye mimba,mahali walipo wazazi  wao ikiwa ni pamoja na viongozi wa maeneo yao hasa Watendaji wao wa vijiji na kata ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Halmashauri nyingine za Mkoa wa Rukwa ni pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Vijijini,Nkasi, Kalambo na Manispaa ya Sumbawanga.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA