WASAINI MKATABA ILI KUANZA UJENZI HOSPITALI YA MKOA WA KATAVI


Serikali ya Mkoa wa Katavi na Shirika la uzalishaji mali la jeshi la kujenga taifa SUMA JKT wamelitiana saini mkataba kwa ajili ya kuanza ujenzi wa ghorofa moja la hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Katavi.
Kaimu katibu tawala Bw.Wilbrod Malandu akizungumza wakati wa kutiliana saini hiyo ofisini kwake,amesema Bodi ya Zabuni imemtunuku zabuni SUMA JKT kutekeleza ujenzi wa ghorofa hilo kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 9 na milioni 798.76 ambapo ghorofa hilo litakuwa na vitanda 76 kwa safu ya chini na 71 kwa safu ya juu.
Aidha Malandu amesema eneo la ujenzi wa Hospitali hiyo lenye ukubwa wa ekari 243 linapatikana Kata ya Kazima ambapo zaidi ya shilingi milioni 468 zimetumika kuwalipa fidia kwa watu 108 ili kupisha ujenzi huku zaidi ya shilingi milioni 722 zikilipwa kwa mshauri mwelekezi  Y and P Architects Tanzania Limited aliyetekeleza taarifa mbalimblai ikiwemo upembuzi yakinifu,andiko la mradi na uainishaji wa athari za kijamii na mazingira.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la uzalishaji mali la jeshi la kujenga taifa SUMA JKT Kanali Andrew Mkinga pamoja na kuipongeza serikali ya mkoa wa Katavi kwa kumpatia zabuni hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa SUMA JKT,ameahidi kujenga kwa weledi na kukamilisha kazi kwa wakati uliopangwa.
Mkoa wa Katavi ulianza Mpango wa ujenzi wa hospitali ya Rufaa tangu mwaka 2014 ambapo katika eneo la ujenzi kunatarajia kuwemo vitengo mbalimbali vikiwemo Chuo cha sayansi na tiba,chuo cha uuguzi na utafiti pamoja na shule,maduka,hotel, stendi ya mabasi na viwanja vya michezo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA