WAKAZI WILAYANI TANGANYIKA WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU


Kaimu  Afisa wa Afya wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Bw.Philipo Mihayo amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugojwa wa kipindupindu kwa kufanya usafi wa  chakula na mazingira yote yanayowazunguka.
Bw.Mihayo amesema ni vema  kuchukua tahadhari kwani mikoa jirani ya Rukwa na kigoma inaripotiwa kukubwa kadhia hiyo.
Aidha Mihayo ametoa wito kwa wananchi kuchimba vyoo vya kisasa lakini pia kuhakikisha wanatumia maji safi na salama huku wanaokadi maelekezo akisema watachukuliwa hatua.
Wilaya jirani ya Sumbawanga iliyopo Mkoani Rukwa ilitangaza kuwa katika kipindi cha Mei 11 mpaka 24 watu 7 walikuwa wamefariki dunia huku wengine 166 wakiugua ugonjwa wa kipindupindu na 44 mpaka kufikia Mei 25 walikuwa wakiendelea kupatiwa matibabu.
Kipindupindu husababishwa na bakteria aina ya Vibrio cholerae zinazosababisha kuhara majimaji yenye rangi kama maji ya kupikia mchele ambapo bakteria hao walitambuliwa mwaka 1854 .
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA